Matokeo ya Tp Mazembe VS Yanga Leo 14/12/2024

Matokeo ya Tp Mazembe VS Yanga Leo

Matokeo ya Tp Mazembe VS Yanga Leo 14/12/2024 | Matokeo ya Yanga leo Dhidi ya TP Mazembe

Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi inaendelea leo ambapo wawakilishi kutoka Tanzania, Yanga SC, watakuwa dimbani dhidi ya TP Mazembe ya DR Congo. Mchezo huu unatarajiwa kupigwa saa 10:00 jioni katika Uwanja wa TP Mazembe Stadium, ikiwa ni mechi ya tatu kwenye hatua ya makundi. Timu zote zinahitaji ushindi ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kufuzu robo fainali ya michuano hii mikubwa ya vilabu barani Afrika.

Kocha Mkuu wa Yanga, Sead Ramovic, ameweka wazi kuwa timu yake itapambana kwa kila hali kuhakikisha inapata ushindi wa ugenini. Kwa mujibu wa kocha huyo, maandalizi ya mchezo yamezingatia mbinu maalum za kumiliki mpira, kurudisha mipira inayopotea, na kushambulia kwa kasi.

“Tunacheza dhidi ya timu yenye uzoefu mkubwa na inayopenda soka la moja kwa moja. Tumeandaa mfumo wa kukabiliana na changamoto hizi. Lengo letu ni kuhakikisha tunarudi nyuma haraka tunapopoteza mpira na kushambulia kwa kasi,” alisema Ramovic.

Hadi sasa, Yanga haijakusanya pointi yoyote katika hatua ya makundi baada ya kupoteza mechi zake mbili za awali dhidi ya Al Hilal (2-0) na MC Alger (2-0). Hata hivyo, matumaini yao ya kufufua nafasi ya kufuzu bado yapo, huku wachezaji wakionyesha dhamira ya kupambana kwa nguvu zote.

Matokeo ya Tp Mazembe VS Yanga Leo 14/12/2024

TP Mazembe vs Yanga Sc

🔰Taarifa Kuhusu Mechi🔰

  • 🏆 #CAFCL
  • ⚽️ TP Mazembe🆚Young Africans SC
  • 📆 14.12.2024
  • 🏟 Stade TP Mazembe
  • 🕖 3pm🇨🇩4pm🇹🇿

Matokeo ya Tp Mazembe VS Yanga Leo 14/12/2024

Historia ya Yanga Dhidi ya TP Mazembe

Yanga SC na TP Mazembe wana historia ya kukutana mara kadhaa, ikiwemo michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika mwaka jana (2023). Katika msimu huo, Yanga iliwafunga TP Mazembe mabao 3-1 kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, na kisha kushinda bao 1-0 kwenye Uwanja wa TP Mazembe Stadium.

Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Maxi Nzengeli, alieleza kuwa uzoefu wa kushinda dhidi ya TP Mazembe mwaka jana utakuwa nyenzo muhimu kwao. “Tulipitia changamoto kubwa kutokana na matokeo mabaya hivi karibuni, lakini tunajiamini kwa sababu wachezaji waliopo ni wale wale waliopata ushindi dhidi ya TP Mazembe mwaka jana,” alisema Nzengeli.

Hali ya Kundi A

Kundi A linaendelea kuwa changamoto kwa timu zote zinazoshiriki. TP Mazembe, kama wapinzani wa Yanga leo, wana pointi moja tu baada ya kutoka sare na MC Alger. Hali hii inazifanya timu zote mbili kupigania ushindi wa lazima ili kuweka hai matumaini ya kufuzu.

Mechi nyingine ya kundi hili itazikutanisha MC Alger na Al Hilal usiku wa leo saa 4:00 kwa saa za Afrika Mashariki. Matokeo ya mechi hizi mbili yatatoa taswira ya nafasi za timu kufuzu katika hatua ya robo fainali.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Kikosi cha Yanga vs Tp Mazembe Leo 14/12/2024
  2. Yanga vs Tp Mazembe Leo 14/12/2024 Saa Ngapi?
  3. Miguel Cardoso Akabidhiwa Mikoba ya Ukocha Mamelodi
  4. Viingilio Mechi ya Simba VS CS Sfaxien 15/12/2024
  5. Timu Zinazoshiriki Mapinduzi cup 2025
  6. Ndoa Ya Coastal na Ley Matampi Yavunjika Rasmi
  7. Mapinduzi Cup 2025 Kuchezwa na Timu za Taifa Badala ya Vilabu
  8. Kocha Ramovic Aeleza Sababu za Yanga Kushindwa Mbele ya Waarabu
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo