Matokeo ya Taifa Stars Vs Ethiopia Leo September 4 2024 | Matokeo ya Taifa Stars Leo Dhidi ya Ethiopia Kufuzu AFCON 2025 | Matokeo ya Timu ya Taifa ya Tanzania VS Ethiopia Leo
Katika mchezo wa kuwania kufuzu kwa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 unaotarajiwa kua wakukatana shoka, timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, inakutana na Ethiopia katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam. Mchezo huu unatarajiwa kuanza majira ya saa 1:00 usiku na ni hatua muhimu kwa Taifa Stars katika harakati za kufuzu michuano hiyo inayotarajiwa kufanyika Morocco.
Kocha Msaidizi wa Taifa Stars, Juma Mgunda, ameweka wazi kuwa maandalizi ya timu hiyo yamefanyika kwa ufanisi mkubwa. Kwa mujibu wa Mgunda, wachezaji wako tayari kwa asilimia 80 kushuka dimbani na kuipigania jezi ya Tanzania kwa udi na uvumba. Katika mazoezi yaliyofanyika, wachezaji wameonyesha ari na nidhamu ya hali ya juu, jambo linaloleta matumaini kwa mashabiki wa soka nchini.
Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Cliford Ndimbo, amehamasisha mashabiki kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu yao. Ndimbo amesema kuwa sapoti ya mashabiki ni muhimu sana katika kuongeza morali ya wachezaji na kuhakikisha ushindi dhidi ya Ethiopia. Mchezo huu ni wa kwanza kwa Taifa Stars katika kundi H, ambalo pia linajumuisha timu za DR Congo na Guinea.
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Hemed Suleiman, ameteua kikosi cha wachezaji 23 kwa ajili ya mechi hii. Ingawa baadhi ya wachezaji maarufu kama Mbwana Samatta na Simon Msuva hawajaitwa kwenye kikosi hiki, kocha ameeleza kuwa amechagua wachezaji ambao wako tayari na wana uwezo wa kutekeleza mbinu alizozipanga kwa ajili ya mchezo huu. Hemed ameongeza kuwa Watanzania wanapaswa kuwa na umoja na kuiunga mkono timu yao katika kipindi hiki cha kufuzu.
Angalia Hapa Kikosi cha Taifa Stars Vs Ethiopia Leo September 4 2024
Matokeo ya Taifa Stars Vs Ethiopia Leo September 4 2024
Tanzania | 0-0 FT | Ethiopia |
- 📍Tanzania Vs Ethiopia
- 🏟 Benjamini Mkapa
- ⏰ Saa 1:00 Usiku
Picha Za Matukio Kutoka Dimbani Kwenye Mechi ya Taifa Stars Vs Ethiopia Leo
Kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania kikipasha misuli tayari kwa mchezo wa kufuzu AFCON 2025 dhidi ya Ethiopia
Kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania kikipasha misuli tayari kwa mchezo wa kufuzu AFCON 2025 dhidi ya Ethiopia
Kikosi cha Timu ya Taifa @TaifaStars_ 🇹🇿💪🏾@TaifaStars_ pic.twitter.com/fQ80Hovbn4
— TFF TANZANIA (@Tanfootball) September 4, 2024
Historia na Matumaini ya Taifa Stars
Taifa Stars inatarajia kushiriki michuano ya AFCON kwa mara ya nne, ikiwa imewahi kufuzu mwaka 1980, 2019, na 2023. Katika kampeni hii ya kufuzu, mchezo dhidi ya Ethiopia ni muhimu sana kwani utatoa mwelekeo wa nafasi ya Tanzania katika kundi H. Timu mbili zitakazoongoza kundi hilo ndizo zitakazofuzu kucheza AFCON 2025 huko Morocco.
Hamasa Kutoka Klabu za Ndani
Maofisa habari wa klabu za Yanga, Simba, na Azam FC wamewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanjani ili kuipa nguvu Taifa Stars. Kwa mujibu wa Ally Kamwe wa Yanga, Ahmed Ally wa Simba, na Hasheem Ibwe wa Azam FC, ushindi wa mechi hii utategemea sana sapoti ya mashabiki. Hasheem Ibwe hata ameahidi kutoa tiketi za bure kwa mashabiki ili kuhakikisha uwanja unajaa.
Tathmini ya Kundi H (Kundi la Taifa Stars)
Kundi H linajumuisha timu za Tanzania, DR Congo, Guinea, na Ethiopia. DR Congo ndiyo timu yenye viwango vya juu zaidi katika kundi hili kwa mujibu wa viwango vya FIFA, ikishika nafasi ya 60. Ethiopia ipo nafasi ya 143, Tanzania ni ya 113, na Guinea ipo nafasi ya 77.
Hata hivyo, katika soka, chochote kinaweza kutokea, na kwa mashabiki wa Tanzania, matumaini ni makubwa kwamba Taifa Stars itapata ushindi katika mchezo huu wa nyumbani.
Mapendekezo ya Mhariri:
Leave a Reply