Matokeo ya Taifa Stars Vs DR Congo Leo 15/10/2024 | Matokeo ya Taifa Stars Leo Dhidi ya DR Congo
Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars leo itakutana uso kwa uso na DR Congo katika mchezo wa marudiano wa kuwania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON 2025) utakaopigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam. Mchezo huu unatarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua huku Taifa Stars ikiwa na kibarua cha kulipiza kisasi cha kufungwa bao 1-0 katika mchezo wa kwanza uliopigwa Kinshasa.
Stars inajitupa dimbani ikiwa na ari ya kujiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu kwa fainali hizo zitakazofanyika nchini Morocco mwakani. Ushindi katika mchezo huu utaipeleka Stars kileleni mwa Kundi H na kujihakikishia nafasi ya kucheza fainali hizo kwa mara ya nne.
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Hemed Suleiman ‘Morocco’, amekiandaa kikosi chake vilivyo huku akisisitiza umuhimu wa safu ya ushambuliaji kutumia vyema nafasi watakazopata. Katika mchezo uliopita, Stars ilicheza vizuri lakini ilishindwa kutumia nafasi nyingi za kufunga.
Mashabiki wa soka nchini wametakiwa kujitokeza kwa wingi kuishangilia Taifa Stars ili kuwapa wachezaji hamasa na kuongeza morali ya kupambana. Wadau wa soka wamesisitiza umuhimu wa mashabiki kuwa mchezaji wa 12 na kuisaidia timu kupata ushindi.
Hali ya Kundi la aifa Stars Katika Michuano ya Kufuzu AFCON 2025
Kundi H linajumuisha timu nne: Tanzania, DR Congo, Ethiopia, na Guinea. Hadi sasa, DR Congo inaongoza kundi hilo ikiwa na pointi 9, ikifuatiwa na Taifa Stars yenye pointi 4, Guinea pointi 3, na Ethiopia ikiwa na pointi 1. Ushindi kwa Taifa Stars leo utawafanya wafikishe pointi 7, hatua itakayowapa nafasi kubwa ya kufuzu katika fainali za AFCON 2025 zitakazofanyika Morocco.
Iwapo Taifa Stars itashinda, watakuwa wamejiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu kwa mara ya nne kushiriki AFCON. Hata hivyo, kushindwa kwao leo kunaweza kuwaweka kwenye presha kubwa watakapoelekea mechi zao zijazo dhidi ya Ethiopia na Guinea.
Ushindi kwa Taifa Stars utaifanya ifikishe pointi saba na kujiweka katika mazingira mazuri ya kusonga mbele. Ikumbukwe kwamba timu mbili za kwanza katika kila kundi ndizo zitakazofuzu kwa fainali za AFCON 2025.
Matokeo ya Taifa Stars Vs DR Congo Leo 15/10/2024
Taifa Stars | 0-2 | DR Congo |
Hiki Apa Kikosic cha Taifa Stars Kilicho Anza Dhidi ya DR Congo Leo
- Ally Salim (Gk)
- Lusajo Mwaikenda
- Mohamed Hussein
- Ibrahim Abdulla
- Dickson Job
- Adolf Mtasingwa
- Kibu Dennis
- Mudathir Yahya
- Feisal Salum
- Mbwana Samatta (C)
- Clement Mzize
Wachezaji wa Ziada: Yona Jofrey, Zuberi Foba, Abdallah Said, Himid Mao, Pascal Msindo, Bakari Mwamnyeto, Cyprian Thobias, Khalid Habibu, Ibrahim Ame, Nassoro Saadun, Suleiman Mwalimu
Mapendekezo ya Mhariri: Tanzania Taifa Stars vs Congo Leo 15/10/2024 ni saa ngapi?
Leave a Reply