Matokeo ya Tabora united vs Yanga Leo 02/04/2025

Tabora United VS Yanga Leo 02 04 2025 Saa Ngapi

Matokeo ya Tabora united vs Yanga Leo 02/04/2025 | Matokeo ya Yanga Leo Dhidi ya Tabora united Ligi Kuu ya NBC

Tabora United leo itawakaribisha mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya NBC, Yanga SC, katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora, kwa mchezo wa ligi kuu msimu wa 2024/2025. Huu ni mchezo wa marudiano baada ya Yanga kupokea kipigo cha mabao 3-1 katika mzunguko wa kwanza, matokeo yaliyosababisha kuondoka kwa aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Miguel Gamondi.

Timu zote mbili zinaingia kwenye mchezo huu zikiwa chini ya makocha wapya. Yanga, ambayo kwa sasa inanolewa na Miloud Hamdi kutoka Ufaransa na Algeria, ina rekodi nzuri chini ya kocha huyo, ikishinda michezo minne kati ya mitano ya ligi na kutoka sare moja. Wakati huo huo, Tabora United kwa sasa iko chini ya kocha mzimbabwe Genesis Mang’ombe, aliyemrithi Anicet Kiazayidi Makiadi kutoka DR Congo.

Yanga inaingia katika mchezo huu ikiwa inaongoza msimamo wa ligi kwa alama 58 na ikisaka pointi tatu ili kuendelea kujikita kileleni. Timu hiyo imeonyesha safu kali ya ushambuliaji kwa kufunga mabao 58 katika michezo 22 ya ligi, ikiwa na wastani wa mabao matatu kwa kila mechi. Kwa upande mwingine, Tabora United inashika nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 37.

Licha ya kuwa na mwenendo mzuri, timu hiyo imeruhusu mabao 28 katika mechi 23, jambo linaloonyesha udhaifu wa safu yake ya ulinzi. Kocha Mang’ombe amesisitiza kuwa wana kazi kubwa ya kurekebisha safu ya ulinzi ili kuepuka kuruhusu mabao mengi dhidi ya Yanga.

Matokeo ya Tabora united vs Yanga Leo 02/04/2025

Matokeo ya Tabora united vs Yanga Leo 02/04/2025

Tabora United  VS Yanga Sc

Presha kwa Tabora United na Historia ya Mchezo wa Awali

Tabora United inakumbuka ushindi wao wa mzunguko wa kwanza dhidi ya Yanga, lakini mchezo wa leo unatarajiwa kuwa tofauti kwa sababu Yanga ina kocha mpya mwenye mbinu tofauti. Mbali na hilo, timu hiyo imetoka kuondolewa kwenye Kombe la FA baada ya kufungwa na Kagera Sugar kwa mikwaju ya penalti 5-4, hali inayoweza kuwaathiri kisaikolojia.

Kwa upande wa Yanga, wanatafuta kulipa kisasi na kujiimarisha zaidi kwenye msimamo wa ligi. Rekodi yao nzuri ya kufunga mabao mengi chini ya Hamdi ni ishara kwamba wataingia uwanjani kwa kasi wakitafuta ushindi muhimu.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Kikosi cha Yanga VS Tabora united Leo 02/04/2025
  2. Viingilio Mechi ya Tabora united Vs Yanga SC Leo 02/04/2025
  3. Tabora United VS Yanga Leo 02/04/2025 Saa Ngapi?
  4. Real Madrid Yaweka Dau la Pauni Milioni 90 Kumnasa Bruno Fernandez
  5. Kagera Sugar Yagonga Mwamba Usajili wa George Mpole
  6. Ratiba ya Nusu Fainali Kombe la FA 2024/2025 England
  7. Timu Zilizofuzu Nusu Fainali Kombe la FA Uingereza 2024/2025
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo