Matokeo ya Stellenbosch VS Simba SC Leo 27 April 2025

Stellenbosch VS Simba SC Leo 27 April 2025

Matokeo ya Stellenbosch VS Simba SC Leo 27 April 2025 | Matokeo ya Simba Leo Dhidi ya Nusu Fainali Stellenbosch Kombe la Shirikisho | Matokeo ya Mechi ya Simba vs Stellenbosch leo

Wekundu wa Msimbazi, Simba SC, leo wanashuka dimbani kuivaa Stellenbosch FC katika mchezo muhimu wa marudiano wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika msimu wa 2024/2025. Mchezo huu unaotarajiwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Moses Mabhida mjini Durban, Afrika Kusini kuanzia saa 10 jioni kwa saa za Afrika Mashariki, ndio utakaotoa mwanga wa timu ipi itakayosonga mbele hadi fainali, huku Simba wakiwa na faida ya ushindi wa bao moja walilopata katika mechi ya awali iliyopigwa Zanzibar.

Katika mchezo wa kwanza uliochezwa katika Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar, Simba walijihakikishia ushindi wa 1-0 kupitia bao la Jean Charles Ahoua aliyefunga kwa mkwaju wa faulo dakika ya 45+2. Faida hii inaipa Simba nafasi nzuri, lakini pia inawataka kuwa makini, kwani bao moja tu la wapinzani linaweza kulazimisha mchezo kuamuliwa kwa mikwaju ya penalti.

Kocha wa Simba SC, Fadlu Davids, ameweka wazi kuwa mkakati wao katika mchezo wa leo ni kutafuta bao la mapema ili kuvuruga hesabu za Stellenbosch. Davids amesisitiza kuwa Simba haitacheza kwa kujilinda wala kwa hofu, bali watashambulia kutafuta ushindi wa moja kwa moja. Kwa mujibu wa mkakati huo, dakika 10 za mwanzo zitakuwa muhimu katika kutafuta bao ambalo litawatia nguvu zaidi.

Katika maandalizi ya mechi hii muhimu, Davids alisema,

“Tunakwenda kwenye mchezo wa marudiano tukiwa na lengo moja tu kutafuta bao la mapema na kumaliza kazi. Hatutacheza kwa kujilinda. Hatutacheza kwa woga. Hatutaki sare. Tunataka ushindi.”

Kwa msisitizo huo, Simba inaonyesha dhamira ya kushinda si kwa lengo la kujilinda tu, bali kuendelea kuonyesha ukubwa wao kwenye soka la Afrika.

Kwa upande wa Stellenbosch, Kocha Steve Barker ameahidi kupambana kwa nguvu zote ili kugeuza matokeo. Barker alieleza kuwa, licha ya kushindwa katika mchezo wa kwanza, ana matumaini makubwa kutokana na kiwango kizuri walichoonyesha ugenini. Alisema,

“Nina imani sana kwamba mechi ya pili tutafunga na kuingia fainali.”

Barker ameonesha dhamira ya kuamuru mashambulizi ya mapema, akiamini kuwa Simba wanaweza kufungika kirahisi.

Katika mtazamo wa jumla, mechi hii inatarajiwa kuwa ya kasi na ushindani mkali katika dakika 45 za kwanza, huku kila timu ikisaka bao la kuamua hatima ya mchezo.

Matokeo ya Stellenbosch VS Simba SC Leo 27 April 2025

Matokeo ya Stellenbosch VS Simba SC Leo 27 April 2025

Stellenbosch vs Simba SC

Wachezaji Hatari Wa Kuzingatiwa: Jean Charles Ahoua

Jean Charles Ahoua ameendelea kuwa nguzo muhimu kwa Simba katika safari yao ya Kombe la Shirikisho. Mshambuliaji huyo, ambaye anaongoza kwa mabao ndani ya timu msimu huu, ameifungia Simba mabao matatu muhimu katika mashindano haya. Kila alipofunga, Simba walishinda kwa 1-0, ikiwa ni dhidi ya Bravos do Maquis, CS Sfaxien, na Stellenbosch.

Zaidi ya hapo, Ahoua pia ameng’ara katika Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu, akifunga jumla ya mabao 12. Ni nadra kwa Simba kuruhusu bao wanapomtegemea Ahoua kufunga, na katika michezo mingi aliyoifungia, kikosi kiliweza kumaliza dakika 90 bila kuruhusu bao.

Kwa rekodi hizi, Ahoua anabeba matumaini makubwa ya Simba kuendeleza mafanikio yao katika uwanja wa Moses Mabhida.

Hali za Vikosi

Kwa upande wa Stellenbosch, kipa wao na nahodha Sage Stephens anatarajiwa kurejea golini baada ya kukosa mchezo wa kwanza kutokana na majeraha. Katika mchezo wa leo, Stellenbosch itawakosa wachezaji wawili muhimu, Lehlohonolo Mojela na Ashley Cupido, ambao bado ni majeruhi.

Kikosi kinachotarajiwa kwa Stellenbosch kinajumuisha wachezaji: Sage Stephens, Enyinnaya Godswill, Fawaaz Basadien, Thabo Moloisane, Ismael Olivier Touré, Genino Palace, Sihle Nduli, Thato Khiba, Devin Titus, Lesiba Nku, na Andre de Jong.

Kwa Simba SC, taarifa kutoka kambini zinaonyesha kuwa Chamou Karaboue, ambaye alikuwa na majeraha madogo katika mechi iliyopita, sasa yuko fiti na yuko tayari kuisaidia timu. Hakuna taarifa ya mchezaji yeyote kukosekana miongoni mwa wale waliocheza mechi ya awali.

Kikosi cha Simba SC kinatarajiwa kuwa: Moussa Camara, Shomari Kapombe, Mohamed Hussein, Abdulrazack Hamza, Chamou Karaboue, Fabrice Ngoma, Yusuph Kagoma, Kibu Denis, Jean Charles Ahoua, Elie Mpanzu, na Steven Mukwala.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Stellenbosch VS Simba SC Leo 27 April 2025 Saa Ngapi?
  2. Mayele Aipeleka Pyramid Fainali Klabu Bingwa Afrika CAF
  3. Al Ahly Yamtimua Kocha Marcel Koller Baada ya Kutolewa Klabu Bingwa Afrika
  4. Mtibwa Sugar Yarejea Ligi Kuu NBC 2025/2026
  5. Timu Zilizofuzu Nusu Fainali Kombe la Muungano 2025
  6. JKU Yaiondoa Singida Black Stars Kombe la Muungano
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo