Matokeo ya Simba Vs Tanzania Prisons Fc Leo 22/10/2024

Tanzania Prisons vs Simba SC Leo 22 10 2024 Saa Ngapi

Matokeo ya Simba Vs Tanzania Prisons Fc Leo 22/10/2024 | Matokeo ya Simba leo Vs TZ Prisons

Leo ni siku ya burudani ya mpira wa miguu kwenye Ligi Kuu ya NBC, ambapo miamba wa soka nchini Tanzania, Simba SC, watakutana na Tanzania Prisons FC kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya. Mchezo huu wa kusisimua unatarajiwa kuanza saa 10:00 jioni huku mashabiki wakiwa na shauku kubwa ya kushuhudia matokeo ya mpambano huu.

Baada ya mchezo wa dabi ya watani wa jadi dhidi ya Yanga SC, ambao Simba walitoka na kipigo cha bao 1-0, Kocha Mkuu wa Simba, Fadlu Davids, amesisitiza kuwa timu yake imejipanga vizuri kuhakikisha wanapata pointi tatu muhimu kwenye mechi hii dhidi ya Tanzania Prisons. Licha ya changamoto wanazokumbana nazo wanapocheza Mbeya, Fadlu amesema kuwa wamejifunza kutokana na michezo ya nyuma na wamefanya maandalizi ya kutosha kuhakikisha wanarudi kwenye mbio za ubingwa.

Katika mahojiano yake, Fadlu alitilia mkazo umuhimu wa waamuzi kuchezesha kwa haki na kuhimiza matumizi ya teknolojia ya VAR ili kuepusha makosa ya maamuzi ambayo mara nyingi yamekuwa na athari kwenye matokeo ya michezo mikubwa.

“Tunafahamu kwamba michezo dhidi ya Tanzania Prisons imekuwa migumu kila mara, lakini tumekuja kuchukua pointi tatu. Tunahitaji maamuzi sahihi ili kila timu ipate haki yake,” alisema Fadlu.

Matokeo ya Simba Vs Tanzania Prisons Fc Leo 22/10/2024

Tanzania Prisons Fc VS Simba Sc

Matokeo ya Simba Vs Tanzania Prisons Fc Leo 22/10/2024

Historia ya Mechi za Simba SC na Tanzania Prisons FC

Katika msimu uliopita, Simba SC ilipoteza dhidi ya Tanzania Prisons kwenye uwanja huu wa Sokoine kwa mabao 2-1, jambo ambalo limewafanya wachezaji wa Simba, wakiongozwa na nahodha Mohamed Hussein “Tshabalala”, kujiandaa vizuri zaidi ili kuhakikisha hawaruhusu bao tena katika mechi ya leo. Tshabalala alikiri kwamba Uwanja wa Sokoine umekuwa wenye changamoto kwao, lakini akabainisha kuwa timu imejipanga vyema kwa pambano hili.

“Tumepata changamoto nyingi tukiwa hapa Mbeya, lakini safari hii tunajua nini cha kufanya, na tutahakikisha haturuhusu bao lolote,” alisema Tshabalala.

Kwa upande wa Tanzania Prisons, kocha wao Mbwana Makata alieleza kuwa wanaingia kwenye mechi hii kwa tahadhari kubwa baada ya kutazama mchezo wa Simba dhidi ya Yanga. Tanzania Prisons inashikilia nafasi ya 12 kwenye msimamo wa ligi, ikiwa na pointi saba baada ya mechi saba. Kocha Makata alikiri ubora wa Simba lakini alisisitiza kuwa wamejipanga kukabiliana nao kwa mpango maalum.

“Tunafahamu ubora wa Simba, lakini tumefanya maandalizi ya kutosha kukabiliana nao. Tunaheshimu uwezo wao, lakini nasi tuna mipango yetu kuhakikisha tunawazuia,” alisema Makata.

Msimamo wa Simba SC

Simba SC kwa sasa wanashika nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara wakiwa na pointi 13 baada ya kucheza michezo sita. Ushindi wa leo unatarajiwa kuwa muhimu kwa Simba ili kurejesha hali ya kujiamini na kuendelea kushindania nafasi ya juu kwenye ligi.

Huku mashabiki wa Simba wakitarajia ushindi, ni wazi kuwa mechi hii itakuwa na ushindani mkubwa kutokana na historia ya matokeo magumu wanayopata dhidi ya Tanzania Prisons, hususan wakiwa ugenini Mbeya. Matokeo ya mechi hii yanasubiriwa kwa hamu kubwa.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Msimamo Ligi Kuu NBC 2024/2025 Tanzania Premier League
  2. Ratiba ya Mechi za Ligi Kuu ya NBC Leo Oktoba 22, 2024
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo