Matokeo ya Simba vs JKT Tanzania Leo 24/12/2024 | Matokeo ya Simba leo Dhidi ya JKT Tanzania
Kikosi cha Simba kitakua dimbani leo kuwakabili wageni wao JKT Tanzania katika mechi muhimu ya Ligi Kuu Bara, inayotarajiwa kuchezwa kuanzia saa 10:15 jioni katika Uwanja wa KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam. Hii ni mechi ya kiporo kufuatia ajali iliyotokea wakati kikosi cha JKT Tanzania kilikuwa kikirejea kutoka Dodoma.
Simba, ambayo inahitaji pointi tatu muhimu, inaingia uwanjani kwa lengo la kuendeleza wimbi la ushindi na kujiimarisha zaidi katika msimamo wa ligi. Kocha Msaidizi wa Simba, Selemani Matola, alisisitiza kuwa timu yao itakuwa na malengo makubwa ya kuchukua ushindi ili kuongeza kasi ya kujiweka katika nafasi nzuri kuelekea mzunguko wa kwanza wa ligi. Aliongeza kuwa wataingia dimbani wakiwa na mpango wa kubadilisha mfumo wao wa uchezaji kulingana na jinsi JKT Tanzania watakavyocheza.
“Tutabadilisha mfumo wetu kadri wapinzani wetu watakavyokuwa wanabadilika. Hii itawachanganya, kwa sababu kile ambacho walikifanyia mazoezi, hatutaki kuwa na mfumo ule ule,” alisema Matola. Hata hivyo, kocha huyo alikiri kuwa mechi hii itakuwa ngumu kwa sababu ya kiwango kizuri cha JKT Tanzania, ingawa timu hiyo haijapata matokeo bora hivi karibuni. Matola pia alizungumzia suala la timu yao kuruhusu mabao mepesi, akieleza kuwa wamefanya kazi kubwa mazoezini ili kuhakikisha hali hiyo haijirudii tena katika mchezo huu.
Kwa upande wa JKT Tanzania, Kocha Mkuu Ahmad Ally alisema timu yake imejiandaa vyema kwa ajili ya mechi hii, huku akitaja Simba kama moja ya timu bora katika ligi. Ally alitaja kwamba timu yake imejizatiti hasa katika maeneo ya ulinzi na mashambulizi, na walijua kuwa mchezo huu utakuwa mgumu kutokana na uwezo wa Simba.
“Simba ni timu bora, ina wachezaji wengi wenye uzoefu na kocha mzuri. Hata hivyo, sisi kama JKT Tanzania tumefanya maandalizi yetu kwa umakini mkubwa. Tunajua mchezo huu utakuwa na changamoto kubwa, lakini tunataka kuwa wa kwanza katika kila tukio,” alisema Ally.
JKT Tanzania, ingawa imeshindwa kushinda michezo mitatu mfululizo ya ligi, inajiandaa vyema ili kupata matokeo bora dhidi ya Simba. Kocha Ally alisisitiza kuwa muhimu ni jinsi timu yao itakavyocheza wakati wa kumiliki mpira na wakati wa kutokuwa na mpira, akieleza kuwa mpango wao ni kuhakikisha wanazuia mashambulizi ya Simba na kufanya mashambulizi ya haraka wakati wa kupata mpira.
Matokeo ya Simba vs JKT Tanzania Leo 24/12/2024
Simba Sc | 1-0 | JKT Tanzania |
- 🏆 #NBCPremierLeague
- ⚽️ Simba SC🆚JKT Tanzania
- 📆 24.12.2024
- 🏟 KMC Complex
- 🕖 10:15 Jion
Mapendekezo ya Mhariri:
Leave a Reply