Matokeo ya Simba vs Fountain Gate Leo 06 Februari 2025 | Matokeo ya Simba Leo Dhidi ya Fountain Gate
Wekundu wa Msimbazi Simba SC leo watakuwa ugenini katika dimba la Tanzanite Kwaraa, Babati, kuvaana na wenyeji wao Fountain Gate FC katika mchezo muhimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Mechi hii ina umuhimu mkubwa kwa Simba kwani ushindi utaendelea kuwaimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi msimu wa 2024/2025.
Mchezo huu unatarajiwa kuwa mgumu kwa timu zote mbili kutokana na rekodi zao za msimu huu. Simba imeonyesha ubora mkubwa kwenye safu ya ushambuliaji, huku ikiwa na wastani wa mabao mawili kwa kila mchezo katika mechi 16 zilizopita za ligi, na kufunga jumla ya mabao 34. Kwa upande wa Fountain Gate, wamefunga mabao 24, ikiwa ni wastani wa bao 1.5 kwa kila mchezo.
Katika mchezo wa kwanza wa msimu huu baina ya timu hizi, Simba waliibuka na ushindi mnono wa mabao 4-0 kwenye Uwanja wa KMC Complex. Hata hivyo, Fountain Gate hawajawahi kushinda mechi yoyote dhidi ya Simba katika historia ya Ligi Kuu, huku wakiwa wamefungwa mara nne na kupata sare moja katika mechi tano walizokutana awali.
Simba inaingia katika mchezo huu ikiwa na morali ya hali ya juu baada ya kushinda mechi zake 10 za mwisho mfululizo kwenye ligi. Kwa upande mwingine, Fountain Gate wamekuwa wakisuasua, wakishinda mechi mbili pekee kati ya 10 zilizopita, huku wakitoka sare moja na kupoteza zingine.
Kocha wa Simba, Fadlu Davids, amesisitiza kuwa kikosi chake kimejipanga vizuri kuhakikisha wanashinda mechi hii na kuendelea kuongoza ligi. Amesema kuwa mashabiki wa Simba walioko mikoani wamekuwa msaada mkubwa kwa timu yao, kwani wamekuwa wakijitokeza kwa wingi na kuwapa nguvu wachezaji wao wanapocheza ugenini.
Kwa upande wa Fountain Gate, kocha wao mpya Robert Matano, amesisitiza kuwa timu yake ipo tayari kwa mchezo huu na watahakikisha wanatoa upinzani mkali kwa Simba. Matano amesema, “Tunajua Simba ni timu kubwa na tunawaheshimu, lakini sisi pia tumejiandaa kikamilifu.”
Matokeo ya Simba vs Fountain Gate Leo 06 Februari 2025
Fountain Gate | VS | Simba SC |
Simba Bila Denis Kibu?
Simba inaweza kumkosa winga wao tegemeo Denis Kibu, ambaye aliumia kwenye mechi iliyopita. Ingawa hali yake inaendelea vizuri, uwepo wake kwenye mchezo huu haujathibitishwa kikamilifu. Daktari wa timu, Edwin Kagoba, amesema kuwa bado wanamfanyia tathmini ya mwisho kuona kama anaweza kucheza au la.
Kwa upande wa uongozi wa Simba, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu hiyo, Mohamed Dewji (Mo), amesisitiza kuwa Kibu hatouzwa kwa MC Algers ya Algeria, kwani Simba bado inamuhitaji kwa michuano ya ndani na kimataifa.
Matarajio ya Matokeo
Ikiwa Simba itashinda mechi hii, watafikisha pointi 46 na kuimarisha nafasi yao kileleni mwa msimamo wa ligi. Kwa Fountain Gate, ushindi utawafanya wafikishe pointi 23 na kuendelea kushikilia nafasi ya sita.
Kwa kuzingatia rekodi za timu zote, Simba inaonekana kuwa na nafasi kubwa ya kushinda, lakini Fountain Gate watatumia fursa ya kucheza nyumbani kujaribu kupata matokeo mazuri. Mchezo unatarajiwa kuwa wa ushindani mkubwa na wenye msisimko wa hali ya juu.
Mapendekezo ya Mhairiri:
Leave a Reply