Matokeo ya Simba vs Coastal Union Leo 04/10/2024

Simba vs Coastal Union Leo 04 10 2024 Saa Ngapi

Matokeo ya Simba vs Coastal Union Leo 04/10/2024 | Matokeo ya Simba Sc Leo Dhidi ya Coastal union

Wekundu wa Msimbazi Simba leo watakua dimbani kuwakabili wagosi wa Kaya Coastal union katika mchezo wa ligi kuu ya NBC Tanzania msimu wa 2024/2025. Mechi hii itaanza kutimua vumbi majira ya saa 10:15 jioni katika uwanja wa KMC complex Mwengi jijini Dar es salaam. Mchezo huu unatarajiwa kua mgumu na wenye mvuto kwa mashabiki kutokana na ubora wa timu zote mbili.

Simba SC, licha ya kuwa na wachezaji wengi wapya, wameanza msimu kwa mafanikio makubwa, wakishinda michezo yao yote minne ya awali bila kuruhusu bao lolote. Safu yao ya ulinzi inayoongozwa na mlinzi kutoka Cameroon, Che Malone Fondoh, imekuwa ngome imara, jambo linaloongeza matumaini ya mashabiki wao kuelekea mchezo wa leo. Katika michezo minne waliyocheza hadi sasa, Simba wamekusanya jumla ya pointi 12, wakifunga mabao 10 bila kuruhusu hata moja.

Kampeni ya Simba Sc ligi kuu ya 2024/2025 ilianza rasmi tarehe 18 agosti ambapo waliufungua msimu kwa ushindi mnono wa magoli 3-0 didi ya Tabora united kabla ya kuwararua Fountain Gate Fc jumla ya magoli 4-0 katika mchezo wao wa pili wa ligi. Mchezo wa tatu, Simba walishinda goli 2-0 dhidi ya wana rambaramba Azam Fc na mwisho kuwachapa Dodoma Jiji 1-0 katika uwanja wao wa nyumbani.

Kwa upande wa Coastal Union, wanakabiliwa na changamoto kubwa, lakini mshambuliaji wao nyota, Maabad Maulid, ametoa kauli yenye matumaini, akieleza kuwa amejiandaa vizuri kupambana na mabeki wa Simba.

Maabad, ambaye ameanza msimu huu kwa kishindo kwa kufunga mabao mawili na kutwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Mechi dhidi ya Pamba Jiji, anatarajiwa kuwa tegemeo kubwa la Coastal Union katika harakati za kutafuta ushindi leo. Amesema kuwa ana mkakati maalum wa kuwapenya mabeki wa Simba, akisisitiza kuwa anayo “dawa” ya kufanikiwa dhidi ya ulinzi huo imara.

Matokeo ya Simba vs Coastal Union Leo 04/10/2024

Simba Sc VS Coastal Union

🏆 #NBCPremierLeague
⚽️ Simba SC🆚Coastal union Fc
📆 04.10.2024
🏟 KMC Complex
🕖 16:15PM(EAT)

Angalia Hapa Kikosi cha Simba vs Coastal Union Leo 04/10/2024

Matokeo ya Simba vs Coastal Union Leo 04/10/2024

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Msimamo wa Ligi kuu NBC Tanzania 2024/2025
  2. Ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara 2024/2025
  3. Wafungaji Bora Ligi Kuu ya NBC Tanzania 2024/2025

Maneno ya Makocha Kuelekea Mechi ya Simba Vs Coastal union

Kocha Mkuu wa Simba, Fadlu Davids, ameeleza matumaini yake ya ushindi mkubwa katika mchezo wa leo, akisema timu yake imekuwa ikifanya mazoezi ya ziada ili kuhakikisha wanatumia vizuri nafasi wanazozipata uwanjani. Katika mechi zilizopita, kumekuwa na changamoto ya kupoteza nafasi nyingi za wazi, hasa kwa winga wao Leonel Ateba, ambaye alikosa mabao kadhaa dhidi ya Dodoma Jiji. Fadlu amesisitiza kuwa wamefanyia kazi tatizo hilo na wanatarajia kuboresha ufanisi wao wa kufunga magoli.

Hata hivyo, Kaimu Kocha Mkuu wa Coastal Union, Joseph Lazaro, ameonesha imani kuwa timu yake inaweza kupata matokeo chanya ikiwa watafanikiwa kutumia udhaifu wa Simba. Lazaro ameongeza kuwa wamejipanga vizuri na wanajua udhaifu wa Simba, huku akisema kuwa timu yake itajitahidi kutumia mbinu zote kuhakikisha wanapata ushindi kwenye mchezo huu mgumu.

Hii ni mechi muhimu kwa Coastal Union, kwani wako kwenye nafasi isiyoridhisha kwenye msimamo wa ligi, na wanahitaji pointi tatu ili kujiondoa kwenye hatari ya kushuka daraja.

Takwimu na Rekodi za Simba Vs Coastal Union Michezo Iliopita

Takwimu na Rekodi za Simba Vs Coastal Union Michezo Iliopita

Kwa ujumla, Simba SC wanaingia kwenye mechi hii wakiwa na motisha ya kuendeleza rekodi yao ya kutoshindwa dhidi ya Coastal Union tangu msimu wa 2019/2020. Katika mechi 12 walizokutana, Simba wameshinda michezo 10 na kutoka sare mara mbili, hivyo kuwapa faida ya kisaikolojia kuelekea mchezo huu wa leo.

Coastal Union, ambao hadi sasa wameshinda mechi moja tu kati ya sita walizocheza msimu huu, wanakabiliwa na changamoto kubwa, lakini wana matumaini ya kufufua hali yao. Matarajio ya mashabiki ni kuona mchezo wenye ushindani mkubwa, ambapo timu zote mbili zinapigania alama muhimu kwa ajili ya msimamo wa ligi.

Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo