Matokeo ya NECTA Kidato Cha Sita 2024 Haya Hapa
Breaking news. Baraza la mtihani tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya kidato cha sita 2024. Matokeo hayo yametangazwa leo july 13 2024 na mtendaji necta anatangaza matokeo ya kidato cha sita na ualimu 2024
Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya kidato cha sita mwaka 2024. Matokeo haya yamewekwa wazi leo Jumamosi, Julai 13, 2024, katika hafla iliyofanyika ofisi za Baraza hilo Zanzibar. Taarifa hizi zinasubiriwa kwa hamu na wanafunzi na wazazi kote nchini, na ni hatua muhimu kwa watahiniwa katika safari yao ya elimu.
Ufaulu wa Mtihani NECTA Kidato Cha Sita 2024
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), Dk Said Mohamed, alieleza kuwa ufaulu wa jumla kwa mwaka huu umeongezeka kwa asilimia 0.26 ukilinganisha na mwaka uliopita. Hii ni habari njema kwa wanafunzi na wazazi kwani inaonyesha juhudi za walimu, wanafunzi, na serikali katika kuinua viwango vya elimu.
Dk Said Mohamed alibainisha kuwa ufaulu kwa masomo yote upo zaidi ya asilimia 90. Hii ina maana kuwa wanafunzi waliofanya mtihani wa kidato cha sita mwaka huu wamepata alama nzuri katika masomo mbalimbali, jambo linaloashiria maandalizi mazuri na kazi nzuri ya walimu katika shule mbalimbali nchini.
Idadi ya Watahiniwa na Vituo vya Mitihani
Mwaka huu, jumla ya watahiniwa 113,504 walifanya mtihani wa kidato cha sita. Mtihani huu ulifanyika katika shule 931 na vituo vya watahiniwa wa kujitegemea 258. Hii inaonyesha ongezeko la idadi ya watahiniwa ikilinganishwa na miaka iliyopita, jambo linaloashiria uboreshaji katika sekta ya elimu nchini.
Angalia Hapa Utangazaji Wa NECTA Kidato Cha Sita 2024 Hapa
Angalia Hapa Matokeo ya NECTA Kidato Cha Sita 2024
Jinsi ya Kuangalia Matokeo ya NECTA Kidato cha Sita 2024
1. Tembelea Tovuti ya NECTA
Tembelea tovuti rasmi ya NECTA: www.necta.go.tz.
2. Nenda kwenye Menyu ya Tovuti na Bonyeza “Matokeo”
Katika ukurasa wa kwanza wa tovuti ya NECTA, nenda kwenye menyu kuu na bonyeza kipengele cha “Matokeo.”
3. Chagua “Matokeo ya ACSEE”
Kutoka kwenye orodha ya matokeo, chagua “Matokeo ya ACSEE” ambayo ni matokeo ya mtihani wa Kidato cha Sita.
4. Bonyeza “Matokeo ya ACSEE 2024”
Ukurasa wa Matokeo ya ACSEE utafunguka, bonyeza “Matokeo ya ACSEE 2024” kuona matokeo ya mwaka 2024.
5. Tafuta Shule Yako
Ukurasa wa “Utafutaji wa Matokeo ya Mtihani wa ACSEE 2024” utafunguka. Tafuta jina la shule yako kutoka kwenye orodha iliyopo.
6. Bonyeza Kiungo cha Shule Yako
Bonyeza kiungo cha shule yako ili kuona matokeo yake. Ili kupata matokeo yako binafsi, fungua kiungo cha shule yako kisha tafuta jina lako baada ya ukurasa wa matokeo ya shule kufunguka.
Hatua za Kuangalia Matokeo ya Kidato cha Sita 2024 Kupitia USSD
- Piga *152*00#
- Chagua namba 8. ELIMU
- Chagua namba 2. NECTA
- Chagua aina ya huduma 1. MATOKEO
Chagua aina ya Mtihani 2. ACSEE - Ingiza Namba ya Mtihani na Mwaka Mfano: S0334-0556-2019
- Chagua aina ya Malipo (Gharama kwa SMS ni Tshs 100/=)
- Baada ya kukamilisha malipo, utapokea ujumbe mfupi wenye matokeo.
Mapenekzo ya Mhariri:
Leave a Reply