Matokeo ya Namungo Vs Simba Leo 19/02/2025 | Matokeo ya Simba Sc Leo dhidi ya Namungo
Klabu ya Namungo leo itawakaribisha Wekundu wa Msimbazi, Simba SC, katika mchezo wa kukata shoka wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2024/2025. Mechi hiyo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi majira ya saa 12:30 jioni katika Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa, Lindi.
Kwa Simba, ushindi kwenye mchezo huu utaendelea kuiimarisha katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kwa kufikisha pointi 50, jambo ambalo litaisaidia kuendelea kuwasaka vinara wa ligi. Kwa upande wa Namungo, ushindi utaiwezesha kufikisha pointi 24, hivyo kuimarisha nafasi yake katika msimamo wa ligi.
Mashabiki wa soka kote nchini wanatarajia mchezo wa ushindani mkubwa, huku Namungo ikijivunia rekodi yake ya kutochapwa na Simba kwa miaka minne uwanjani Majaliwa. Je, Simba itaweza kuvunja mwiko huo na kurejea na alama tatu muhimu, au Namungo itaendeleza rekodi yake ya ushindani? Muda pekee ndio utaamua.
Matokeo ya Namungo Vs Simba Leo 19/02/2025
Namungo | VS | Simba Sc |
Historia ya Ushindani Kati ya Namungo na Simba
Tangu Mei 29, 2021, ambapo Simba iliibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Namungo katika Uwanja wa Majaliwa, miamba hao wa soka nchini wamekuwa wakihangaika kupata ushindi kwenye uwanja huo. Katika kipindi cha miaka minne, timu hizo zimekutana mara tatu katika uwanja huo, na kila mara mchezo umemalizika kwa sare.
- Msimu wa 2021/2022: Namungo na Simba zilitoka sare ya mabao 2-2.
- Msimu wa 2022/2023: Timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1.
- Msimu wa 2023/2024: Simba ililazimishwa sare ya mabao 2-2.
Hali hii inazifanya dakika 90 za mchezo wa leo kuwa muhimu kwa Simba, ambayo inapania kuvunja mwiko wa kutoshinda uwanjani hapo kwa siku 1363.
Kauli za Wachezaji na Makocha Kabla ya Mchezo
Beki wa Simba, David Kameta ‘Duchu’, amesema kuwa kikosi cha Simba kimejipanga kuhakikisha wanapata ushindi na kumaliza mwendo wa sare dhidi ya Namungo.
“Sisi wachezaji wa Simba tumejiandaa vizuri kwa mchezo huu. Tunafahamu kuwa tumekuwa na matokeo yasiyoridhisha katika uwanja huu, lakini huu ni mchezo mwingine na siku nyingine. Timu imebadilika, kocha ni tofauti, wachezaji pia ni wengine. Tumekusudia kushinda,” alisema Duchu.
Kwa upande wake, kocha wa Simba, Fadlu Davids, amesisitiza kuwa timu yake imepata muda mzuri wa kujiandaa kwa mchezo huu, hasa baada ya mechi yao dhidi ya Dodoma Jiji kuahirishwa.
“Mechi iliyoahirishwa dhidi ya Dodoma Jiji imetupa muda wa ziada wa maandalizi. Tunajua kwamba tunakutana na timu nzuri iliyopangiliwa vyema kwenye ulinzi, lakini tumejipanga kushambulia huku tukizingatia nidhamu ya ulinzi,” alisema Fadlu.
Kocha wa Namungo, Juma Mgunda, ameonyesha matumaini makubwa kuelekea mchezo huu, akisema kuwa kikosi chake kipo tayari kwa changamoto. “Tunamshukuru Mungu wachezaji wako kwenye hali nzuri. Mechi hii ni muhimu kwetu na maandalizi yote yamekamilika. Wale waliokuwa majeruhi sasa wapo sawa. Tunaombea wachezaji waamke salama ili kila mmoja atimize majukumu yake,” alisema Mgunda.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Kikosi cha Simba Vs Namungo Leo 19/02/2025
- Namungo Vs Simba Sc leo 19/02/2025 Saa Ngapi?
- Matokeo ya KMC vs Yanga Leo 14 Februari 2025
- Kikosi cha Yanga VS KMC Leo 14 Februari 2025
- KMC Vs Yanga Leo 14 Februari 2025 Saa Ngapi?
- Kikosi cha Simba VS Tanzania Prisons Leo 11/02/2024
- Simba VS Tanzania Prisons Leo 11/02/2024 Saa Ngapi?
- YANGA warejea nyumbani na pointi moja baada ya sare na JKT Tanzania
Leave a Reply