Matokeo ya Mashujaa VS Yanga Sc Leo 23/02/2025 | Matokeo ya Yanga leo dhidi ya Mashujaa Fc
Timu ya Wananchi Yanga SC leo itakuwa ugenini kuwakabili Mashujaa FC katika Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma. Mechi hii inatarajiwa kuanza saa 10:15 jioni na ni moja ya michezo inayovuta hisia nyingi kutokana na umuhimu wake katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Ushindani mkali unatarajiwa kati ya timu hizi mbili, huku kila moja ikihitaji pointi tatu kwa malengo tofauti.
Kwa upande wa Yanga, ushindi katika mchezo huu utaihakikishia kuendelea kuongoza msimamo wa ligi kwa kufikisha pointi 55. Matokeo mazuri yataiweka timu hiyo katika mazingira mazuri kuelekea mechi inayofuata dhidi ya Pamba na hatimaye Kariakoo Dabi dhidi ya Simba SC tarehe 8 Machi. Pia, ushindi wa Yanga leo utaiongezea presha Simba SC ambayo iko nyuma kwa pointi mbili, huku ikitarajiwa kucheza mechi ngumu dhidi ya Azam FC siku ya Jumatatu.
Iwapo Yanga itapoteza au kutoka sare, itajiweka katika mazingira magumu kwa kuongeza presha kuelekea dabi ya Kariakoo. Hii itatoa nafasi kwa Simba kujipanga vyema kwa mchezo wake wa Jumatatu, kwani bado ina mechi moja mkononi.
Kwa Mashujaa FC, ushindi katika mechi hii ni muhimu kwa sababu utawafanya kufikisha pointi 26 na kupanda hadi nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi. Hata hivyo, endapo watapoteza pointi, bado hawatakuwa salama kwani wanakaribia eneo la kushuka daraja kwa tofauti ya pointi tano tu kutoka kwa timu inayoshika nafasi ya mwisho kwenye mstari wa kushuka daraja.
Mashujaa inalazimika kupambana kwa nguvu ili kupata matokeo chanya, jambo ambalo linatarajiwa kuongeza ushindani katika mechi hii dhidi ya mabingwa watetezi wa ligi.
Matokeo ya Mashujaa VS Yanga Sc Leo 23/02/2025
Mashujaa Fc | 0-1 | Yanga Sc |
Taarifa za Mchezo
🏆 #NBCPremierLeague
⚽️ Mashujaa FC🆚Young Africans SC
📆 23.02.2025
🏟 Lake Tanganyika
🕖 10:15 Jioni
Historia ya Mechi za Huko Nyuma
Katika rekodi za Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga SC imekutana na Mashujaa FC mara tatu na kushinda mechi zote. Matokeo yalikuwa kama ifuatavyo:
- Yanga 2-1 Mashujaa
- Yanga 1-0 Mashujaa
- Yanga 3-2 Mashujaa
Kwa rekodi hizi, Mashujaa wana kibarua kigumu cha kutafuta ushindi wa kwanza dhidi ya Wananchi.
Wachezaji wa Kuzingatiwa
Katika mchezo huu, Yanga itapaswa kumakinika na mshambuliaji hatari wa Mashujaa FC, David Ulomi, ambaye amefunga mabao manne msimu huu. Ulomi amekuwa tishio kwa wapinzani kutokana na uwezo wake wa kufunga mabao kwa mashuti ya mbali.
Kwa upande wa Yanga, safu yake ya ushambuliaji inayoongozwa na Clement Mzize (mfungaji bora wa ligi kwa mabao 10) na Prince Dube (mabao 9) inatarajiwa kuipa Mashujaa kibarua kigumu. Yanga imekuwa bora zaidi katika mechi za ugenini msimu huu, ikiwa imekusanya pointi 25 kutokana na ushindi mara nane na sare moja katika mechi tisa.
Kwa Mashujaa, rekodi yao nyumbani msimu huu haijawa thabiti, wakishinda michezo minne, kutoka sare nne na kupoteza miwili kati ya mechi 10 walizocheza katika Uwanja wa Lake Tanganyika.
Tamba za Makocha Kabla ya mchezo
Kocha wa Yanga, Hamdi Miloud, amesema kuwa lengo lao ni kushinda mchezo huu na kurudi na pointi tatu muhimu.
“Tunajua mechi itakuwa ngumu, tunawaheshimu wapinzani wetu lakini hatupo hapa kupumzika, tunahitaji pointi tatu,” alisema Miloud.
Kwa upande wake, kocha wa Mashujaa, Mohamed Abdallah ‘Baresi’, alisema kuwa wanajua wanakutana na timu yenye wachezaji wenye uwezo wa kuamua matokeo, lakini wamejipanga vyema kwa ajili ya mchezo huu.
“Tupo kwenye nafasi inayotulazimisha kupata matokeo mazuri. Tunahitaji pointi hizi ili kujiepusha na presha ya kushuka daraja,” alisema Baresi.
Ratiba Nyingine za Ligi Kuu Leo
Mbali na mchezo wa Mashujaa vs Yanga, kutakuwa na mechi nyingine mbili:
- Singida Black Stars vs Pamba Jiji FC – Saa 8:00 mchana, Uwanja wa CCM Liti, Singida.
- Namungo FC vs Coastal Union – Saa 1:00 usiku, Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa, Lindi.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Kikosi cha Yanga vs Mashujaa Leo 23/02/2025
- Washindi wa Tuzo za Wachekeshaji Tanzania 2025
- Droo Robo Fainali Klabu Bingwa Afrika CAF 2025
- Droo Robo Fainali Kombe la Shirikisho 2025
- Droo ya Robo Fainali CAF Kombe la Shirikisho & Klabu Bingwa (Februari 20 2025)
- Wapinzani wa Simba Robo Fainali Kombe la Shirikisho CAF
- Matokeo ya Namungo Vs Simba Leo 19/02/2025
- Kikosi cha Simba Vs Namungo Leo 19/02/2025
Leave a Reply