Matokeo ya Ethiopia vs Taifa Stars Leo 16/11/2024 | Matokeo ya Tanzania Vs Ethiopia Leo Kufuzu AFCON 2025
Leo ndo ile siku ambayo Timu ya Taifa ya Mpira wa miguu Tanzania almaarufu kama TAIFA Stars itakuwa na mtihani muhimu mgumu ambapo watapambana vikali dhidi ya wenyeji wao, Ethiopia huko DR Congo katika mchezo kuwania nafasi ya kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025, Morocco. Mchezo huu, unaochezwa katika Uwanja wa Martyrs, Kinshasa, ni kama fainali kwa Taifa Stars, kwani ushindi ndio njia pekee ya kufufua matumaini yao ya kufuzu kwa mara ya nne katika historia ya michuano hii.
Taifa Stars inahitaji ushindi ili kujiweka katika nafasi nzuri kabla ya mchezo wa mwisho dhidi ya Guinea, huku Ethiopia ikijaribu kuimarisha nafasi yao licha ya kuwa katika nafasi ya mwisho kwenye msimamo wa Kundi H. Taifa Stars kwa sasa iko katika nafasi ya tatu kwenye kundi H ikiwa na pointi nne, ikitanguliwa na Guinea yenye pointi sita na DR Congo waliokwishajihakikishia kufuzu wakiwa na pointi 12. Ethiopia, inayoshikilia mkia ikiwa na pointi moja pekee, itatumia mchezo huu kama fursa ya kujenga heshima yao.
Kwa Tanzania, ushindi ni muhimu ili kuwapa nafasi nzuri ya kufuzu, hasa ikizingatiwa mchezo wa mwisho dhidi ya Guinea, ambao pia utakuwa na umuhimu mkubwa. Kocha Hemed Suleiman ‘Morocco’ amesisitiza nidhamu na mshikamano wa kikosi chake, akitegemea sana wachezaji wazoefu kama Mbwana Samatta na Simon Msuva kuongoza safu ya ushambuliaji.
Matokeo ya Ethiopia vs Taifa Stars Leo 16/11/2024
Ethiopia | 0-2 FT | Tanzania |
|
Udhaifu wa Ethiopia na Nafasi kwa Taifa Stars
Ethiopia imekuwa na changamoto kubwa katika michezo ya kufuzu, ikiwa na rekodi dhaifu ya kucheza nyumbani. Katika michezo yao mitano ya mwisho ya kufuzu, wamepoteza michezo mitatu wakifungwa mabao nane. Hii ni dalili wazi ya matatizo katika safu yao ya ulinzi, hasa kipindi cha kwanza ambapo mabao mengi yameruhusiwa.
Hali ya kutokuwa na uwanja maalum wa nyumbani pia inaathiri mikakati yao ya kiufundi na kisaikolojia. Ethiopia imekuwa ikihamahama, ikitumia viwanja tofauti kama Alassane Ouattara huko Ivory Coast na sasa Uwanja wa Martyrs nchini DR Congo.
Kwa upande wa Taifa Stars, hii ni fursa ya kutumia mwanya huu, hasa kwa kuzidisha mashambulizi ya mapema. Ushindi wa haraka, kama ilivyoshuhudiwa kwenye mchezo wa Guinea dhidi ya Ethiopia ambapo mabao matatu yalifungwa ndani ya dakika 23, unaweza kuwa na manufaa makubwa kwa Stars.
Rekodi ya Taifa Stars Ugenini
Katika michezo mitano ya hivi karibuni ya ugenini, Taifa Stars imeonesha uwezo wa kupambana licha ya changamoto za kucheza mbali na nyumbani. Ushindi dhidi ya Guinea (2-1) na Zambia (1-0) ni ushahidi kuwa kikosi hiki kinaweza kushinda hata katika mazingira magumu.
Hata hivyo, vipigo vya karibu dhidi ya DR Congo na Sudan vinatoa funzo muhimu kwa Stars kuwa nidhamu ya hali ya juu inahitajika. Kikosi kinapaswa kuzingatia matumizi bora ya nafasi na kupunguza makosa ya kiufundi.
Matarajio kwa Wachezaji wa Kipekee
Mbwana Samatta na Simon Msuva ni miongoni mwa wachezaji wanaotarajiwa kuleta mabadiliko makubwa katika mchezo huu. Samatta, akiwa mshambuliaji mwenye uzoefu wa kimataifa, atahitajika kuongoza mashambulizi, huku Msuva akiongeza kasi na ubunifu katika safu ya mbele. Kwa upande wa ulinzi, umakini wa mabeki na nidhamu ya safu ya kiungo itakuwa muhimu sana kuzuia mashambulizi ya Ethiopia. Kocha Morocco atahitaji kuhakikisha wachezaji wake wanatumia mwanya wowote unaotokea ili kupata ushindi muhimu wa ugenini.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Baada ya Kibarua Kuota Ndago Yanga, TFF nao Wampiga Pini Gamondi
- Cv ya Sead Ramovic Kocha Mpya wa Yanga
- Yanga Kubeba Mzigo wa Kulipa Faini Ya Gamond
- Bodi ya Ligi Yaanza Uchunguzi Tukio La Kukutwa Mabomba Ya Sindano Azam Complex
- Hizi Apa Rekodi Za Miguel Gamondi Akiwa Yanga
- Kali Ongala Tambulishwa Kuwa Kocha Mpya wa KMC
- Ethiopia Vs Tanzania 16/11/2024 Saa Ngapi?
- Gamondi Akalia Kuti Kavu Yanga
Leave a Reply