Matokeo ya Equatorial Guinea vs Twiga Star Leo 26/02/2024 | Matokeo ya Timu ya Taifa ya Wanawake leo Dhidi ya Equatorial Guinea Kufuzu AFCON 2025
TIMU ya Taifa ya wanawake ‘Twiga Stars’ inatarajiwa kushuka dimbani muda mfupi ujao kuvaana na wenyeji Equatorial Guinea katika mchezo wa marudiano wa kufuzu kwa Fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (WAFCON) 2026 zitakazofanyika Morocco.
Mchezo huu unachezwa kwenye Uwanja wa Estadio de Malabo, huku Stars ikiingia uwanjani na faida ya ushindi wa 3-1 walioupata katika mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Azam Complex, Chamazi. Kikosi cha Kocha Bakari Shime kinahitaji matokeo mazuri ili kusonga mbele kwenye hatua inayofuata ya mashindano haya makubwa ya bara la Afrika.
Twiga Stars inaingia dimbani ikiwa na matumaini makubwa ya kufuzu, ikitegemea washambuliaji wake wenye uzoefu kama Stumai Abdallah, Enekia Lunyamila, na Diana Msewa ambao walifunga mabao katika mchezo wa kwanza. Pia, Opah Clement anayecheza soka la kulipwa nchini Mexico na Winifrida Gerald wa JKT Queens wanatarajiwa kuwa na mchango mkubwa katika safu ya ushambuliaji.
Kwa upande wa Equatorial Guinea, wanahitaji ushindi wa mabao makubwa ili kufufua matumaini yao ya kufuzu, hivyo wanatarajiwa kucheza kwa nguvu na kushambulia kwa kasi tangu mwanzo wa mchezo. Hili linamaanisha kuwa safu ya ulinzi ya Stars inapaswa kuwa imara kuhakikisha wanazuia mashambulizi ya wapinzani wao.
Matokeo ya Equatorial Guinea vs Twiga Star Leo 26/02/2024
Equatorial Guinea | 1-1 | Twiga Star |
Iwapo Stars itafanikiwa kusonga mbele, itakutana na mshindi kati ya Uganda na Ethiopia. Katika mchezo wa kwanza wa mchuano huo, Uganda iliibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Ethiopia, hivyo timu yoyote itakayovuka hapa inatarajiwa kuwa na kibarua kigumu katika hatua inayofuata.
Wakati mashabiki wa soka wakisubiri kwa hamu matokeo ya mechi hii muhimu, matumaini ni kuwa Twiga Stars itaendelea kufanya vizuri na kujiunga na Taifa Stars, Serengeti Boys, na Ngorongoro Heroes kama moja ya timu za Tanzania zilizofanikiwa kufuzu katika mashindano makubwa ya Afrika.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Man United Wamnyemelea Xavi Kuchukua Mikoba ya Amorim
- Kocha Melis Medo Atua Singida Black Stars Kama Kocha Msaidizi
- Simba yajikuta Pabaya Baada ya Sare ya 2-2 Dhidi ya Azam
- Washindi wa Tuzo za Wachekeshaji Tanzania 2025
- Hiki Apa Kikosi cha Simba vs Azam Fc Leo 24/02/2025
- Matokeo ya Simba vs Azam Fc Leo 24/02/2025
Leave a Reply