Matokeo ya CS Constantine vs Simba Leo 08/12/2024 | Matokeo ya Simba Leo Dhidi ya CS Constantine
Leo, saa 1:00 usiku kwa saa za Tanzania, kikosi cha Simba SC kitashuka dimbani kwenye Uwanja wa Mohamed Hamlaoui, mji wa Constantine, Algeria, kwa ajili ya mchezo muhimu dhidi ya CS Constantine katika raundi ya pili ya Kombe la Shirikisho Afrika, hatua ya makundi. Huu ni mtihani mkubwa kwa Simba, ambapo Kocha Mkuu, Fadlu Davids, ameahidi kuwa timu yake itacheza kwa mikakati madhubuti ili kuhakikisha wanapata matokeo mazuri. Mchezo huu utakuwa na ushindani mkubwa kutokana na changamoto zinazokikabili kila upande, huku CS Constantine ikikosa wachezaji wake watatu muhimu.
Simba SC inajiandaa kwa mchezo huu huku ikiwa na kumbukumbu nzuri ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Bravo do Maquis ya Angola katika raundi ya kwanza. Kocha Fadlu Davids amesema maandalizi ya mchezo huu yamekamilika kwa kiwango cha juu, na kwamba timu yake itacheza kwa mikakati ya kipevu ili kukabiliana na wapinzani wao wa Algeria. Akizungumzia mchezo huo, Fadlu amesema:
“Mandalizi yamekamilika, na tumejipanga kuhakikisha tunapata matokeo mazuri. CS Constantine ni timu nzuri, lakini tunajua tunachohitaji kufanya. Lengo letu ni kupata bao mapema ili kuweka presha kwa wapinzani wetu. Tumejizatiti na maandalizi ya kiufundi, hivyo mchezo utakuwa wa kimkakati na wa kasi.”
Kocha Fadlu pia amesisitiza umuhimu wa kasi katika kushambulia na kurejesha haraka wakiwa wanapokonywa mpira, akiongeza kuwa, “Hatutakiwi kufunguka sana. Tunahitaji maamuzi ya haraka na nidhamu ya kurudi nyuma ili kuepuka mashambulizi ya CS Constantine.”
Kwa upande wa CS Constantine, kocha Kheireddine Madoui anatazama mechi hii kama mtihani mkubwa kwa timu yake, hasa kwa kukosa wachezaji wake muhimu watatu, akiwemo kiungo mshambuliaji Abdennour Iheb Belhocini, kiungo mkabaji Salifou Tapsoba, na mshambuliaji Mounder Temine. Madoui alieleza kuwa timu yake inakutana na changamoto kubwa kwa kutokuwapo kwa wachezaji hawa, lakini ana matumaini kuwa wachezaji waliobaki watajitahidi kujaza nafasi hizo kwa ufanisi.
Madoui alisema: “Tutapambana kwa nguvu, hata kama hatutakuwa na wachezaji hawa muhimu. Tuna morali ya kushinda na tunajua mchezo huu ni muhimu kwa safari yetu ya Kombe la Shirikisho.” Licha ya changamoto hizi, kocha Madoui anaamini timu yake itajitahidi kukabiliana na Simba kwa mbinu za kimkakati.
Matokeo ya CS Constantine vs Simba Leo 08/12/2024
CS Constantine | 2-1 FT | Simba Sc |
|
- 🏆 #CAFCC
- ⚽️ MC Alger🆚Young Africans SC
- 📆 08.12.2024
- 🏟 Mohamed Hamlaoui
- 🕖 07:00pm🇹🇿
Mapendekezo ya Mhariri:
- Kikosi cha Simba Vs CS Constantine Leo 08/12/2024
- Ratiba ya Mechi za Leo 08 December 2024
- Dodoma Jiji Yatolewa Kombe la Shirikisho na Leo Tena kwa Penalti
- CS Constantine vs Simba Leo 08/12/2024 Saa Ngapi?
- Msimamo wa Kundi la Yanga Klabu Bingwa Afrika CAF 2024/2025
- Yanga Yapasuka Tena Klabu Bingwa, Yachapwa 2-0 na MC Alger
Leave a Reply