Matokeo ya Coastal Union Vs Mashujaa Leo 13/09/2024

Matokeo ya Coastal Union Vs Mashujaa Leo 13/09/2024

Leo, tarehe 13 Septemba 2024, mashabiki wa soka watashuhudia pambano kati ya Coastal Union na Mashujaa FC katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara. Mchezo huu utatimua vumbi katika dimba la KMC Complex, jijini Dar es Salaam, baada ya Uwanja wa Mkwakwani kufungiwa kwa muda ili kupisha zoezi la ukarabati.

Coastal Union, maarufu kama Wagosi wa Kaya, wanaingia kwenye mchezo huu wakiwa na matumaini makubwa baada ya kutoka sare ya 1-1 dhidi ya KMC katika mechi yao ya kwanza ya msimu. Kikosi hicho kinachonolewa na kocha Joseph Lazaro kinatarajia kutumia vyema faida ya uwanja wa nyumbani ili kuibuka na ushindi wao wa kwanza msimu huu.

Kwa upande mwingine, Mashujaa FC wameanza msimu kwa nguvu, wakishinda mechi moja na kutoka sare kwenye nyingine kati ya mechi mbili walizocheza. Mashujaa wana pointi nne na wanatarajia kuongeza pointi tatu muhimu katika mechi hii. Kocha wao, Mohamed Abdallah ‘Bares’, anatarajia mchezo mgumu lakini ana imani kuwa timu yake itapata matokeo mazuri.

Matokeo ya Coastal Union Vs Mashujaa Leo 13/09/2024

Coastal Union  0-1 Mashujaa

Matokeo ya Coastal Union Vs Mashujaa Leo 13/09/2024

Kauli za Makocha Kabla ya Mchezo

Kocha wa Coastal Union, Joseph Lazaro, ameonyesha kujiamini licha ya changamoto anazotarajia kutoka kwa Mashujaa FC. Lazaro alisema timu yao imejipanga vyema na hawatarudia makosa waliyofanya katika michezo ya nyuma.

Akisisitiza umuhimu wa mchezo huu, alieleza kuwa ushindi ni muhimu ili kujiweka kwenye nafasi nzuri msimu huu na kuhakikisha wanapata nafasi ya kumaliza ndani ya nne bora.

“Tunajua ubora wa Mashujaa ambao wamekuwa wakitupa changamoto kila tunapokutana nao. Hatuwezi kurudia makosa tuliyofanya awali, tumejipanga kuhakikisha tunapata ushindi ili kuweka matumaini ya kumaliza msimu kwenye nafasi za juu,” alisema Lazaro.

Kwa upande wa kocha wa Mashujaa, Mohamed Abdallah ‘Bares’, alisema licha ya changamoto ya kucheza ugenini, anatarajia timu yake itaibuka na ushindi. Alikiri kuwa Coastal Union watakuwa na ari kubwa kutokana na matokeo yao ya nyuma, lakini naye amejiandaa kuhakikisha hawapotezi pointi katika mechi hii muhimu.

“Najua Coastal Union wanatoka kwenye matokeo mabaya, hivyo watakuja kwa nguvu zaidi. Hata hivyo, mimi pia sitaki kupoteza pointi tena baada ya kutoka sare na Tanzania Prisons. Dakika 90 zitaamua ubora wetu,” alisema Abdallah.

Matarajio ya Mchezo

Mchezo huu unatarajiwa kuwa mkali na wa ushindani kutokana na hali ya timu zote mbili. Coastal Union wanahitaji ushindi ili kupata pointi tatu za kwanza msimu huu, huku Mashujaa wakipania kuendeleza mwenendo mzuri wa kupata matokeo. Hali ya uwanja wa KMC Complex inaweza pia kuwa na athari, hasa kwa Coastal ambao wamekuwa wakizoea kucheza katika uwanja wa Mkwakwani.

Mashabiki wa soka wanatarajia kuona mchezo wa kasi, hasa ukizingatia kwamba timu zote mbili zinahitaji ushindi kwa sababu tofauti. Kocha Lazaro wa Coastal Union anahitaji kuboresha safu yake ya ulinzi ambayo imeonyesha udhaifu katika mechi za hivi karibuni, huku kocha Abdallah wa Mashujaa akijikita zaidi katika kuhakikisha kikosi chake kinadhibiti mpira katikati ya uwanja na kushambulia kwa kasi.

Muda na Mahali pa Mchezo

Mchezo huu wa Ligi Kuu Bara kati ya Coastal Union na Mashujaa utapigwa leo saa 10:00 jioni katika Uwanja wa KMC Complex. Mashabiki wanakaribishwa kushuhudia mchezo huu mubashara kwenye viwanja au kupitia vituo vya televisheni vya michezo vinavyorusha matangazo ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kwa matokeo ya papo hapo ya mchezo huu, endelea kufuatilia habari hizi ambazo zitakujulisha matokeo kamili, takwimu za mchezo, na jinsi kila timu ilivyopambana.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Kundi la Tanzania Kufuzu AFCON U20 Kanda ya CECAFA
  2. Ratiba Ngao ya Jamii Wanawake 2024
  3. Msimamo NBC Premier league 2024/2025 | Ligi Kuu Bara
  4. Kocha wa Arsenal Arteta asaini mkataba mpya hadi 2027
  5. Michuano ya Ngao ya Jamii Kwa Wanawake Kuanza Septemba 24
  6. Yanga Yaunda Kikosi Kazi cha Misheni ya Makombe
  7. Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili Utumishi 2024
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo