Matokeo ya Al Hilal VS Yanga Leo 12/01/2025 | Matokeo ya Yanga leo Dhidi ya Al Hilal Klabu Bingwa CAF
Mashabiki wa Yanga leo wanashikilia pumzi zao huku timu yao ikitarajiwa kushuka dimbani dhidi ya Al Hilal katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, hatua ya makundi. Mechi hii inachezwa katika Uwanja wa Cheikha Ould Boïdiya nchini Mauritania, ikiwa na umuhimu mkubwa kwa mabingwa wa Tanzania kufanikisha safari yao ya kufuzu hatua ya robo fainali.
Baada ya ushindi wa MC Alger dhidi ya TP Mazembe kwa bao 1-0, Yanga wanakabiliwa na jukumu la lazima la kushinda leo ili kufikisha pointi saba na kubaki nyuma ya MC Alger kwa tofauti ya pointi moja.
Hali hii inaifanya mechi dhidi ya Al Hilal kuwa ngumu na ya presha kubwa kwa kikosi cha Sead Ramovic, ambacho kinahitaji ushindi siyo tu kwa kutimiza ndoto ya hatua ya robo fainali, bali pia kwa kulinda heshima ya klabu na mashabiki wake.
Al Hilal tayari wamefuzu robo fainali na wanacheza bila shinikizo kubwa. Hata hivyo, wanalenga kumaliza hatua ya makundi wakiwa kileleni mwa Kundi A. Wapinzani wao, Yanga, wanahitaji kuonyesha uwezo mkubwa mbele ya timu iliyokamilika kiufundi na kimkakati.
Kocha wa Yanga, Sead Ramovic, anaamini katika uwezo wa timu yake. “Simuangalii mpinzani ili kuwa bora, napambana kuhakikisha najenga timu yenye ushindani. Ninachokifurahia zaidi ni namna timu yangu inavyoimarika na ipo kwenye morali nzuri,” alisema Ramovic kabla ya mchezo huu muhimu.
Kocha huyo amesisitiza maandalizi ya kimkakati kwa timu yake, akizingatia presha ya kupata pointi sita kutoka kwa mechi mbili zilizobaki, ili kufanikisha ndoto ya kufuzu robo fainali kwa mara ya pili mfululizo.
Matokeo ya Al Hilal VS Yanga Leo 12/01/2025
Al Hilal | VS | Yanga Sc |
- 🏆 #TotalEnergiesCAFCL
- ⚽️ Al Hilal🆚Young Africans SC
- 📆 12.01.2025
- 🏟 Cheikha Ould Boidiya
- 🕖 7PM🇲🇷10PM(TZ)🇹🇿
Umuhimu wa Pacome Zouzoua na Clement Mzize Katika mchezo wa Leo
Kwa mujibu wa mtandao wa fotmob.com, kiungo Pacome Zouzoua amekuwa mchezaji muhimu kwa Yanga katika hatua ya makundi. Hadi sasa, ametengeneza nafasi nane za mabao, ingawa hazijatumika ipasavyo. Ushirikiano wake na mshambuliaji Clement Mzize, ambaye amefunga mabao matano tangu mtoano, unaweza kuwa silaha muhimu kwa Yanga dhidi ya Al Hilal. Clatous Chama pia anarejea, akiipa timu nguvu zaidi katika safu ya ushambuliaji.
Kauli ya Kocha wa Al Hilal, Florent Ibenge
Kwa upande wa Al Hilal, kocha Florent Ibenge amesema kuwa wanacheza mchezo wa heshima huku wakiangalia maandalizi ya hatua ya robo fainali. “Mchezo dhidi ya Yanga utakuwa na umuhimu mkubwa kwao, lakini kwetu tunahitaji kujiandaa kwa hali yoyote. Siwezi kujivunia mapema,” alisema Ibenge. Kauli hii inaonyesha kuwa timu hiyo haina presha kubwa, jambo linaloweza kuifanya kucheza kwa uhuru zaidi.
Hali ya Kundi A
Kwa sasa, MC Alger wanaongoza kundi huku Yanga wakihitaji kushinda ili kuwaweka katika nafasi nzuri kuelekea mechi yao ya mwisho nyumbani dhidi ya MC Alger Januari 18. TP Mazembe, waliopo nafasi ya mwisho, hawana cha kupoteza katika mchezo wao wa mwisho dhidi ya Al Hilal, hali inayoweka mazingira ya ushindani mkali kwa kila timu.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Kikosi cha Simba VS Bravos do Maquis Leo 12/01/2025
- Matokeo ya Bravos do Maquis vs Simba SC Leo 12/01/2025
- Bravos do Maquis vs Simba SC Leo 12/01/2025 Saa Ngapi?
- Kikosi cha Yanga VS Al Hilal Leo 12/01/2025
- Ratiba ya Mechi za Leo 12/01/2025
- Al Hilal VS Yanga Leo 12/01/2025 Saa Ngapi?
- Timu Zilizofuzu Robo Fainali Klabu Bingwa Afrika 2024/2025
- Rachid Taoussi Apania Kushusha Nyota Zaidi Dirisha Dogo
- AS Vita Yamnyakua Dennis Modzaka Kutoka Coastal Union
- Walioitwa Kwenye Usaili Uhamiaji 2025
Leave a Reply