Matokeo Simba Vs El-Qanah Egypt Leo (22 July 2024) Mechi Ya Kirafiki

Matokeo Simba Vs El-Qanah Egypt Leo (22 July 2024) Mechi Ya Kirafiki

Wekundu wa Msimbazi, Simba Sports Club leo watacheza dhidi ya El-Qanah kutoka Misri katika mchezo wao wa kwanza wa Kirafiki uko  Ismailia, Misri ambapo wapo katika kambi maalumu ya maandalizi ya kujiweka sawa na msimu wa 2024/2025.

Mechi hii ya Simba Vs Vs El-Qanah Egypt itatimua vumbi majira ya saa11:30 jioni katika Uwanja wa Old Suez Canal. Lengo kuu la mechi hii ni kuwapa nafasi wachezaji wapya wa Simba kuonyesha uwezo wao, pamoja na kocha mpya, Fadlu Davids, kuonyesha mbinu zake.

Mechi hii ya kirafiki ina malengo kadhaa muhimu kwa Simba SC kuelekea msimu wa 2024/2025. Miongoni mwa malengo muhimu ya mchezo huu wa kirafiki dhidi ya El-Qanah Egypt ni pamoja na;

1. Kuwapa Nafasi Wachezaji Wapya: Simba imesajili wachezaji wapya katika dirisha hili la usajili. Mechi hii itawapa fursa ya kuonyesha vipaji vyao na kujenga muunganiko mzuri na wachezaji wa zamani.

2. Mtihani wa Mbinu za Kocha Mpya: Fadlu Davids, kocha mpya wa Simba, atakuwa na nafasi ya kujaribu mbinu zake za mchezo kabla ya mechi muhimu dhidi ya Yanga SC katika ngao ya jamii. Hii itasaidia kutambua maeneo yanayohitaji kuboreshwa.

Mechi hii inatarajiwa kuwa ya kusisimua na yenye ushindani mkubwa. Kwa mashabiki wa Simba SC na wapenzi wa soka kwa ujumla, huu ni mtanange usiofaa kukosa. Endelea kufuatilia habari na taarifa zaidi kuhusu mchezo huu kupitia mitandao ya kijamii na vyombo vya habari.

Matokeo Simba Vs El-Qanah Egypt Leo (22 July 2024) Mechi Ya Kirafiki

Simba Sc 3-0 FT El-Qanah Egypt
  • >> Dakika ya 14 Ahoua ⚽
  • >> Dakika ya 16 Ahoua⚽
  • >> Dakika ya 120, Okejepha ⚽

Kipindi cha kwanza; Matokeo Simba Vs El-Qanah Egypt Leo

Kikosi kinachoanza Leo dhidi ya El-Qanah: Ally Salim (1) Shomari Kapombe (12) Mohamed Hussein (15) Karaboue Chamou (2) Che malone (20) Mzamiru Yassin (19) Yusuph Kagoma (21) Edwin Balua (16) Joshua Mutale (7) Jean Charles Ahoua (10) Freddy Michael (18).

Hapa chini tumekuletea orodha ya wachezaji wanaotarajiwa kuunda kikosi cha Simba SC dhidi ya El-Qanah Egypt

MAGOLIKIPA

  • Ayoub Lakred 🇲🇦
  • Ally Salim 🇹🇿
  • Hussein Abeli 🇹🇿

MABEKI

  • Che Fondoh Malone 🇨🇲
  • Abdulrazack Hamza 🇹🇿
  • Hussein Kazi 🇹🇿
  • Chamou Karaboue 🇨🇮
  • Shomari Kapombe 🇹🇿
  • Valentin Nouma 🇧🇫
  • Mohammed Hussein 🇹🇿
  • Israel Mwenda 🇹🇿

VIUNGO WAKABAJI

  • Augustine Okejepha 🇳🇬
  • Yusuph Kagoma 🇹🇿
  • Fabrice Ngoma 🇨🇩
  • Mzamiru Yassin 🇹🇿
  • Debora Mavambo 🇬🇦

VIUNGO WASHAMBULIAJI

  • Jean Charles Ahoua 🇨🇮
  • Kibu Denis Prosper 🇹🇿
  • Omary Omary 🇹🇿
  • Joshua Mutale 🇿🇲
  • Edwin Balua 🇹🇿
  • Ladack Chasambi 🇹🇿
  • Salehe Karabaka 🇹🇿

WASHAMBULIAJI

  • Freddy Michael Kouablan 🇨🇮
  • Valentino Mashaka 🇹🇿
  • Steven Dese Mukwala 🇺🇬

Matokeo Simba Vs El-Qanah Egypt Leo (22 July 2024) Mechi Ya Kirafiki

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. APR Yatangulia Fainali Cecafa Dar Port Kagame Cup 2024
  2. Matokeo ya Yanga vs FC Augsburg Leo 20 Julai 2024: Yaliyojiri Uwanjani
  3. Kikosi Cha Yanga Vs FC Augsburg Mpumalanga Cup 20/July/2024
  4. Matokeo Azam FC vs US Yacoub El Mansour Leo (20/07/2024) | Mechi ya Kirafiki
  5. Awesu na Onana Watua Misri Kujiunga na Kambi ya Mazoezi ya Simba
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo