Matokeo Kengold Vs Yanga Sc Leo 25/09/2024 | Matokeo ya Yanga Leo Vs Kengold | Matokeo ya Kengold Dhidi ya Yanga Ligi Kuu
Leo, tarehe 25 Septemba 2024, mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania, Yanga SC, watakalibishwa na Kengold SC katika Uwanja wa Sokoine, jijini Mbeya, majira ya saa 10 jioni. Mchezo huu unatarajiwa kuwa wa kihistoria, kwani ni mara ya kwanza timu hizi zinakutana kwenye mechi rasmi ya ligi kuu ya Tanzania bara. Kengold, ambao wamepanda daraja hivi karibuni, watakutana na changamoto kubwa dhidi ya Yanga, ambao wapo kwenye hali nzuri baada ya kushinda michezo yao mingi ya hivi karibuni.
Matokeo Kengold Vs Yanga Sc Leo 25/09/2024
KenGold Sc | VS | Yanga Sc |
- 🏆 #NBCPremierLeague
- ⚽️ Ken Gold🆚Young Africans SC
- 📆 25.09.2024
- 🏟 Sokoine
- 🕖 4:00PM(EAT)
Kikosi cha Yanga Kinachoanza
- 39 Diarra
- 21 Yao
- 23 Boka
- 5 Job
- 4 Bagga
- 8 Augho
- 2 Maxi
- 38 Abuya
- 24 M2128
- 10 A212 Ki
- 17 Ghama
Wachezaji wa Ziada: Aweso, Kibabage, Aziz A, Mkude Mudathir, Shekhan, Pacome, Musonda, Dube, Baleke
Uchambuzi Kuelekea Matokeo Kengold Vs Yanga Sc Leo 25/09/2024
Kengold SC imeuanza msimu wa 2024/2025 kwa mkosi wa kupokea vichapo tangu waanze kucheza mechi za Ligi Kuu. Timu hiyo imekua katika kiwango kisichorizisha na kupoteza michezo minne mfululizo dhidi ya Singida Black Stars, Fountain Gate, KMC, na Kagera Sugar. Matokeo haya yamewafanya wasalie mkiani bila alama yoyote katika msimamo wa ligi kuu ya Tanzania 2024/2025, huku changamoto za kiufundi zikiwa wazi hadi kocha wao mkuu, Fikiri Elias, kujiuzulu.
Licha ya changamoto hizo, kocha mpya wa Kengold, Jumanne Challe, ameweka wazi kwamba wanajipanga vyema kwa mchezo wa leo. “Mpira ni dakika 90, chochote kinaweza kutokea. Tunajua nguvu ya Yanga, lakini tutahakikisha tunajipanga kwa ushindi,” alisema Challe akielezea matarajio yake ya kuvunja rekodi mbaya na kujiweka pazuri.
Kwa upande wa Yanga SC, wao wameuanza msimu wa 2024/2025 kwa kiwango cha hali ya juu.
Baada ya kushinda mechi zao za Ligi ya Mabingwa Afrika kwa ushindi wa jumla wa magoli 17-0 dhidi ya Vital’O na CBE SA ya Ethiopia, Yanga imeonyesha kuwa ni tishio kwa timu yoyote watakayokutana nayo. Katika mechi za hivi karibuni, Yanga imefunga jumla ya mabao 24 na kuruhusu bao moja pekee, hali inayoonesha uimara wao katika safu ya ulinzi na ushambuliaji.
Kocha mkuu wa Yanga, Miguel Gamond, alisisitiza kuwa malengo yao katika mchezo huu ni kupata pointi tatu, bila kujali idadi ya mabao. “Kiu yangu ni kuona Yanga inapata pointi tatu, hata tukipata bao moja ni sawa. Lakini kama tutapata nafasi ya kufunga zaidi, tutaongeza mabao. Nimewaandaa vyema wachezaji wangu kwa mchezo huu,” alisema Gamond, akionesha kujiamini na maandalizi bora.
Yanga itamkosa Farid Mussa kutokana na majeraha, lakini kocha huyo alieleza kuwa kikosi chake kina wachezaji wengi wenye uwezo wa kujaza nafasi hiyo. Aidha, aliongeza kuwa ratiba yao imekuwa ngumu lakini uzoefu na upana wa kikosi vinampa uhakika wa kupata matokeo mazuri. “Ratiba ni ngumu, lakini wachezaji wangu wana uzoefu. Tumecheza mechi ya Ligi ya Mabingwa juzi na leo tutacheza tena, sina hofu yoyote,” aliongeza.
Mapednekezo ya Mhariri:
- Fadlu David na Simba SC Wamejipanga Vyema Kukabiliana na Azam FC Kesho
- Kengold Vs Yanga Leo 25/09/2024 Saa Ngapi
- Kikosi cha Yanga Vs Kengold Leo 25 September 2024
- JKT Tanzania VS Coastal Union Leo 25/09/2024 Saa Ngapi?
- Kengold Wakijichanganya Tunawapiga Nyingi, Gamondi Atoa Onyo
- Azam FC Kwenye Mtihani Mzito Zanzibar Dhidi ya Simba
- Takwimu za Chama Yanga zaanza kutisha Klabu Bingwa
Leave a Reply