Matokeo CBE SA vs Yanga Leo 14 September 2024

Matokeo CBE SA vs Yanga Leo 14 September 2024 | Matokeo CBE vs Young Africans | Matokeo Yanga Vs CBE Live

Mabingwa watetezi wa Ligikuu ya NBC Tanzania, Young Africans SC almaarufu kama Yanga SC, watashuka dimbani leo dhidi ya CBE SA ya Ethiopia katika mechi ya mkondo wa kwanza ya raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mchezo huu utapigwa kwenye Uwanja wa Abebe Bikila, Addis Ababa, majira ya saa 9:00 alasiri kwa saa za Afrika Mashariki (15:00 EAT). Hii ni hatua muhimu kwa Yanga ambao wanatamani kuandika historia ya kufika hatua ya makundi kwa mara ya pili mfululizo.

Yanga SC inakutana na CBE SA, mabingwa wa Ligi Kuu ya Ethiopia. CBE SA imefanya vizuri msimu uliopita na kufanikiwa kutwaa taji hilo licha ya kuwa ni msimu wao wa kwanza kucheza Ligi Kuu baada ya kupanda daraja mwaka 2021. Wenyeji hawa wamekuwa wakionyesha nia ya kuandika historia mpya kwa kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mara ya kwanza.

Kwa upande mwingine, Yanga SC walitinga hatua hii baada ya ushindi wa kishindo wa jumla ya mabao 10-0 dhidi ya Vital’O ya Burundi. Wananchi wanatarajia kurejea kwenye hatua ya makundi na kuendelea na rekodi yao nzuri waliyoiweka msimu uliopita walipofika hadi robo fainali ya michuano hiyo.

Hata hivyo, maandalizi ya Yanga kwa ajili ya mchezo huu yamekumbwa na changamoto, kwani wachezaji 14 wa kikosi cha kwanza walikuwa kwenye majukumu ya timu zao za taifa kwenye mechi za kufuzu AFCON. Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi, alikiri kuwa timu yake haijapata muda wa kutosha kufanya mazoezi ya pamoja, jambo linaloweza kuathiri uimara wa kikosi chao. Licha ya hilo, Gamondi ana imani kuwa timu yake itaweza kuwashinda wapinzani na kusonga mbele kwenye michuano hii.

Matokeo CBE SA vs Yanga Leo 14 September 2024

CBE SA 0-1 YANGA SC

Prince Dube Anaifungia Yanga goli la Kwanza Dakika 45

  • 🏆 #CAFCL
  • ⚽️ CBE SA🆚Young Africans SC
  • 📆 14.09.2024
  • 🏟 Abebe Bikila
  • 🕖 3:00PM
Matokeo CBE SA vs Yanga Leo 14 September 2024
Matokeo Yanga Vs CBE

Kikosi na Mbinu za Yanga

Yanga itaingia uwanjani bila baadhi ya wachezaji wake muhimu. Beki Nickson Kibabage hatawepo kutokana na msiba wa baba yake, na Farid Mussa anasumbuliwa na jeraha baada ya kufanyiwa upasuaji wa hivi karibuni. Hata hivyo, kuna habari njema kwa Wananchi kwani mlinzi Kouassi Yao amerudi mazoezini baada ya kupona jeraha lake, japokuwa bado hajafikia kiwango chake cha juu kabisa.

Gamondi ameweka wazi kuwa kikosi chake kimefanya maandalizi maalum kwa kupitia video za CBE SA ili kuelewa staili yao ya uchezaji. Hii ni hatua muhimu kutokana na kutokujua kwa undani kuhusu wapinzani wao, kwani ni mara ya kwanza kwa timu hizi kukutana. Kocha huyo anaamini kuwa mbinu hizo zitawasaidia kupata matokeo chanya katika uwanja wa ugenini.

Angalia Hapa Kikosi cha Yanga Vs CBE SA Leo 14/09/2024

Rekodi na Changamoto

Yanga SC haijawahi kupata ushindi katika mechi zao za ugenini nchini Ethiopia. Mara ya mwisho walipocheza huko ilikuwa mwaka 2018 dhidi ya Welayta Dicha na walifungwa bao 1-0, lakini walifuzu kwa ushindi wa jumla wa 2-1.

Hii inawapa Wananchi changamoto kubwa dhidi ya CBE, timu ambayo inacheza soka la kushambulia na kumiliki mpira, staili ambayo ni ngumu kuikabili kwa wachezaji ambao bado wanajenga ushirikiano baada ya majukumu ya kimataifa.

CBE SA ni timu inayomilikiwa na Benki ya Biashara ya Ethiopia (Commercial Bank of Ethiopia), na imejijenga vizuri kupitia uwekezaji mkubwa. Hii imeifanya kuwa moja ya timu bora zaidi nchini humo, licha ya kuwa na historia fupi kwenye michuano ya kimataifa.

Kikosi cha CBE kina wachezaji watatu wa kigeni, wakiwemo Caleb Amankwah na Umar Bashiru kutoka Ghana, pamoja na Simon Oketch kutoka Uganda. Kwa upande wa Yanga, watategemea uzoefu wao mkubwa kwenye mashindano haya, huku wakiwa na lengo la kuweka rekodi ya kufuzu hatua ya makundi kwa mara ya pili mfululizo.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Ratiba ya Mechi za Leo 14 September 2024
  2. Yanga Vs CBE SA: Saa Ngapi Mechi Inaanza?
  3. Jeuri ya Simba Kombe la Shirikisho CAF ipo Hapa
  4. Ubora wa Dube na Pacome Wamfanya Kocha CBE Kuingiwa na Hofu
  5. Goli Pekee la Ngushi Laipa Mashaujaa Ushindi Dhidi ya Coastal Union
  6. Nani Atashinda Ballon d’Or 2024? Rodri, Vinicius Jr, Au Jude Bellingham?
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo