Mapinduzi Cup 2025 Kuchezwa na Timu za Taifa Badala ya Vilabu
Hii ni habari mpya kwa mashabiki wa soka nchini Tanzania, Kenya, na Uganda, kwani Kombe la Mapinduzi 2025 halitakuwa na mashindano ya vilabu kama ilivyokuwa kwa miaka ya nyuma. Kwa mara ya kwanza, michuano hiyo itajumuisha timu za taifa pekee, na lengo kuu ni kutoa fursa ya kuziandaa timu hizo kwa ajili ya michuano mikubwa ya kimataifa, ikiwa ni pamoja na mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) na Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) mwaka 2025.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Kombe la Mapinduzi, Suleiman Jabir, alisema kuwa mabadiliko haya ni muhimu, hasa kwa kuzingatia kuwa Tanzania, Kenya, na Uganda ni miongoni mwa wenyeji wa mashindano hayo ya kimataifa. “Mashindano ya mwaka huu yatajumuisha timu za taifa badala ya vilabu ili kutoa mazoezi kwa timu za taifa,” alisema Jabir.
Ratiba ya Mapinduzi Cup 2025 na Maandalizi
Michuano ya Mapinduzi Cup 2025 itaanza rasmi Januari 3, huku fainali zikitarajiwa kufanyika Januari 13. Droo ya kupanga makundi itafanyika kwenye uwanja wa Gombani Pemba, ambao utatumika kama uwanja wa mashindano baada ya uwanja wa Amaan kuwa kwenye maboresho.
Kwa mujibu wa Jabir, mashindano hayo yatahusisha timu za taifa kutoka Zanzibar, Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi, na Burkina Faso. Timu hizi zitagawanywa katika makundi mawili, ambapo timu mbili bora kutoka kila kundi zitafuzu hatua ya nusu fainali, na baadaye, washindi watakutana katika fainali.
Zawadi na Sapraizi
Bingwa wa mashindano haya ataondoka na zawadi ya shilingi milioni 100. Pamoja na mashindano ya mpira wa miguu, kamati ya maandalizi imepanga kutoa sapraizi na zawadi mbalimbali kwa mashabiki na wachezaji. Jabir alibainisha kuwa kutakuwa na tuzo za wachezaji mmoja mmoja katika vipengele mbalimbali, na mipango ya kuongeza vionjo vya kipekee kwenye mashindano haya imekamilika.
Timu Zitakazoshiriki Mapinduzi Cup 2025
Timu za taifa zilizothibitishwa kushiriki michuano ya Mapinduzi Cup 2025 ni:
- Zanzibar Heroes
- Kenya
- Uganda
- Kilimanjaro Stars (Tanzania)
- Burundi
- Burkina Faso
Mapendekezo ya Mhariri:
- Kocha Ramovic Aeleza Sababu za Yanga Kushindwa Mbele ya Waarabu
- Yanga Karibu Kumsajili Kelvin Nashon kutoka Singida
- Habib Kyombo Ajiunga na Pamba Jiji Kwa Mkopo
- Shabani Pandu na Mudrik Abdi Gonda Mbiuoni Kujiunga Fountain Gate
- Msimamo Kundi la Simba Kombe la Shirikisho CAF 2024/2025
- Dodoma Jiji Yatolewa Kombe la Shirikisho na Leo Tena kwa Penalti
Leave a Reply