Man City na Liverpool Wapigania Saini ya Mchezaji wa Crystal Palace

Man City na Liverpool Wapigania Saini ya Mchezaji wa Crystal Palace

Man City na Liverpool Wapigania Saini ya Mchezaji wa Crystal Palace

Klabu kongwe za soka nchini Uingereza, Manchester City na Liverpool, zimeingia katika vita kali ya kumsajili kiungo mshambuliaji machachari wa Crystal Palace, Eberechi Eze, pamoja na kiungo mkabaji chipukizi, Adam Wharton.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa mtoa taarifa wa masuala ya usajili, Ekrem Konur, vilabu vyote viwili vimeonesha nia ya dhati ya kuwania saini za wachezaji hawa, huku Tottenham Hotspur nayo ikihusishwa na mbio hizo.

Man City na Liverpool Wapigania Saini ya Mchezaji wa Crystal Palace

Eze, mwenye umri wa miaka 26, amekuwa kivutio kikubwa kwa vilabu vikubwa kutokana na uwezo wake wa kipekee wa kulisakata kabumbua, ikiwa pamoja na uwezo wake wa kupiga pasi za uhakika na kufunga mabao. Licha ya Crystal Palace kuanza msimu huu kwa kusuasua, Eze ameendelea kung’ara na kuwavutia wengi.

Hata hivyo, dau la kumnasa Eze sio dogo. Crystal Palace inataka kitita cha pauni milioni 89 ili kumwachia mchezaji huyo, jambo ambalo linaweza kuwa kikwazo kwa baadhi ya vilabu.

Wakati huohuo, Liverpool na Man City pia zimekutana katika mtanange mwengine wa kumnasa kiungo mkabaji kinda mwenye umri wa miaka 20, Adam Wharton. Wharton, ambaye ni matunda ya akademi ya Blackburn Rovers, amekuwa mmoja wa wachezaji bora wa Crystal Palace msimu huu, licha ya timu hiyo kutofanya vizuri.

Ushindani wa kumsajili Wharton unatarajiwa kuwa mkali, huku Palace ikitajwa kutaka kitita cha euro milioni 65. Hata hivyo, Liverpool na Man City zinaonekana kuwa tayari kutoa ofa ya karibu euro milioni 45.

Inaelezwa kuwa Liverpool na Man City tayari zimeanza mazungumzo na Crystal Palace, lakini bado hakuna makubaliano yaliyofikiwa. Itakuwa ni jambo la kuvutia kuona ni klabu gani itaibuka mshindi katika mbio hizi za kuwania saini za wachezaji hawa wenye vipaji.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Guardiola Atoa Mapya Kuhusu Mustakabali Wake Man City
  2. Yanga Yataja Siri ya Ushindi Kwenye Dabi dhidi ya Simba
  3. Fountain Gate Yaahidi Ushindi Dhidi ya KMC Oktoba 20
  4. Che Malone Awataka Wachezaji wenzake Kua Makini Kwenye Mechi ya Watani Jumamosi
  5. Washindi wa Tuzo za Ligi Kuu Ya NBC 2024/2025 Mwezi Septemba
  6. Viingilio Mechi ya Simba VS Yanga 19/10/2024
  7. Fadlu Aanza Mikwara Kuelekea Dabi ya Kariakoo
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo