Mambo Bado Yamoto Ligi Kuu Tanzania

Mambo Bado Yamoto Ligi Kuu Tanzania

Mambo Bado Yamoto Ligi Kuu Tanzania

AADA ya Yanga kupata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Tabora United hivi karibuni, mashindano ya Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2024/2025 yameingia katika hatua ya moto. Mechi saba zilizobaki kwa vigogo Simba na Yanga zimebeba hatima ya ubingwa wa msimu huu.

Kwa sasa, Yanga imefikisha jumla ya pointi 61 baada ya kucheza mechi 23. Simba ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 57 kutokana na michezo 22. Hii inaonesha tofauti ya pointi nne huku Simba ikiwa na mchezo mmoja mkononi.

Hata hivyo, tofauti hii inaweza kuongezeka endapo Yanga itaendelea na ushindi katika michezo yake mitatu ya mwezi huu wa Aprili, wakati Simba ikiwa haichezi mechi yoyote ya ligi hadi Mei 2, 2025.

Mambo Bado Yamoto Ligi Kuu Tanzania

Ratiba ya Yanga Mwezi Aprili: Mtihani wa Pointi

Yanga ina jumla ya michezo mitatu ya Ligi Kuu ndani ya Aprili. Tayari imeshinda dhidi ya Tabora United.

Mechi zinazofuata ni dhidi ya Coastal Union, Azam FC, na Fountain Gate.

  • Aprili 7, 2025: Yanga vs Coastal Union – Mchezo utafanyika katika Uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam. Katika raundi ya kwanza, Yanga ilishinda bao 1-0.
  • Aprili 10, 2025: Azam FC vs Yanga – Safari hii Yanga itakuwa mgeni. Mchezo wa awali, Yanga ilifungwa bao 1-0.
  • Aprili 20, 2025: Fountain Gate vs Yanga – Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Manyara. Mechi ya kwanza Yanga ilishinda mabao 5-0.

Kama Yanga itashinda michezo yote mitatu iliyobaki mwezi huu, itafikisha pointi 70. Hii itaongeza tofauti ya pointi hadi 13 dhidi ya Simba, jambo ambalo linaweza kuathiri kwa kiasi kikubwa morali na presha kwa upande wa wapinzani wao wa jadi.

Simba haitacheza mechi yoyote ya Ligi Kuu ndani ya Aprili isipokuwa kama itatolewa kwenye mashindano ya kimataifa dhidi ya Al Masry. Ratiba ya Simba ya Ligi Kuu itarejea Mei 2, 2025, ambapo itakipiga na Mashujaa FC. Hali hii inaipa Yanga fursa ya kuongeza pengo la pointi bila Simba kucheza.

Hata hivyo, presha itarudi kwa Simba mwezi Mei kwani itakuwa na mechi nyingi mfululizo karibu kila baada ya siku tatu. Mchezo wa wao kwa wao dhidi ya Yanga pia bado haujachezwa, na unatarajiwa kuwa na mchango mkubwa katika kuamua bingwa wa msimu huu.

Mei: Mwezi wa Uamuzi kwa Yanga na Simba

Ratiba ya Yanga mwezi Mei:

  • Yanga vs Namungo FC – Raundi ya kwanza ilimalizika kwa Yanga kushinda 2-0.
  • Tanzania Prisons vs Yanga (Mei 21) – Yanga ilishinda 4-0 kwenye mchezo wa awali.
  • Yanga vs Dodoma Jiji (Mei 25) – Mechi ya awali, Yanga ilishinda 4-0.
  • Mchezo dhidi ya Simba (kiporo) – Tarehe haijathibitishwa.

Ratiba ya Simba mwezi Mei:

  • Mei 2: Simba vs Mashujaa – Raundi ya kwanza, Simba ilishinda 1-0.
  • Mei 5: Simba vs JKT Tanzania – Simba ilishinda 1-0 katika mechi ya kwanza.
  • Mei 8: Simba vs Pamba – Mchezo wa kwanza ulimalizika kwa ushindi wa bao 1-0.
  • Mei 11: Simba vs KMC – Tarehe hii iko katikati ya mechi nyingi.
  • Mei 14: Simba vs Singida Black Stars – Mchezo mgumu kwa Simba.
  • Mei 17: Simba vs KenGold (Ugenini) – Mechi dhidi ya timu inayochukuliwa kuwa na kiwango cha chini.
  • Mei 21/25: Simba vs Kagera Sugar – Simba ilishinda 5-2 katika raundi ya kwanza.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Yanga Yaingia Mawindondi Kuisaka Saini ya Mohamed Omar Ali
  2. Fei Toto Aelezea Umuhimu wa Mechi Sita Zilizosalia Kwa Azam
  3. De Bruyne Atangaza Kuondoka Man city Mwishoni Mwa Msimu
  4. Ratiba Ya Robo Fainali Crdb Bank Federation Cup 2024/2025
  5. Simba Yaianza Robo Fainali Shirikisho CAF Kwa Kichapo Cha 2-0
  6. Matokeo ya Tabora united vs Yanga Leo 02/04/2025
  7. Kikosi cha Yanga VS Tabora united Leo 02/04/2025
  8. Viingilio Mechi ya Tabora united Vs Yanga SC Leo 02/04/2025
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo