Makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika 2024/2025 (Caf Confederation Cup Groups)

Makundi ya Kombe la shirikisho CAF

Makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika 2024/2025 (Caf Confederation Cup Groups) | Makundi ya Confederation Cup | Kundi la Simba Kombe la Shirikisho CAF 2024/2025

Shirikisho la mpira wa miguu Barani Afrika (CAF), limetangaza rasmi makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF Confederation Cup) kwa msimu wa 2024/2025, baada ya droo iliyofanyika jijini Cairo, Misri. Droo hii iliyosubiriwa kwa hamu kubwa imepangilia timu 16 katika makundi manne, ambapo kila kundi lina timu nne zitakazochuana vikali kuwania nafasi ya kuingia hatua ya robo fainali.

Msimu huu unatarajiwa kuwa wenye ushindani mkubwa, huku timu kubwa na zenye uzoefu kama Zamalek SC ya Misri, Simba Sc ya Tanzania, ASEC Mimosas ya Ivory Coast, Stellenbosch kutoka Afrika Kusini na nyingine nyine zikiwa zimepangwa katika makundi tofauti. Mashabiki wa soka barani Afrika wanatarajia kushuhudia mechi kali zenye ushindani wa hali ya juu na kandanda safi la kuvutia, huku kila timu ikipambana kuonyesha ubora wake na kutafuta tiketi ya kuendelea katika michuano hii mikubwa.

Baada ya droo hii, wachambuzi wa soka wameanza kutoa maoni yao kuhusu makundi, huku wengi wakitabiri kuwa Kundi C litakuwa “kundi la kifo” kutokana na uwepo wa timu zenye nguvu kama USM ALger na Asec Mimosa. Hata hivyo, michuano hii imekuwa na misukosuko mingi hapo awali, na hakuna anayeweza kutabiri kwa uhakika ni timu gani itaibuka kidedea.

Makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika 2024/2025

Kundi A (Kundi la Simba Kombe la Shirikisho CAF 2024/2025)

  • Simba SC (Tanzania)
  • CS Sfaxien (Tunisia)
  • CS Constantine (Algeria)
  • FC Bravos do Maquis (Angola)

Kundi B

  • RS Berkane (Morocco)
  • Stade Malien (Mali)
  • Stellenbosch FC (South Africa)
  • CD Lunda-Sul (Angola)

Kundi C

  • USM Alger (Algeria)
  • ASEC Mimosas (Ivory Coast)
  • ASC Jaraaf (Senegal)
  • Orapa United (Botswana)

Kundi D

  • Zamalek SC (Egypt)
  • Al Masry SC (Egypt)
  • Enyimba FC (Nigeria)
  • A. Black Bulls (Mozambique)

Makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika 2024/2025 (Caf Confederation Cup Groups)

Mapendekezo ya Mhariri:

Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo