Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili NECTA Oktoba 2024

Usaili NECTA

Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili NECTA Oktoba 2024 | Tangazo La Kuitwa Kwenye Usaili Wa Ajira Kwa Njia Ya Uhamisho Baraza la Mitihani Tanzania NECTA

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) amewatangazia watumishi wa umma walioomba nafasi za kuhamia NECTA kwa njia ya usaili kuwa usaili utafanyika tarehe 17 na 18 Oktoba 2024. Awali, NECTA ilitangaza nafasi za ajira kwa watumishi wa umma wanaotaka kuhamia NECTA. Nafasi hizo ni pamoja na Afisa Mitihani II – Mratibu wa Somo la Chemistry, Afisa Mitihani II – Mratibu wa Somo la Physics, na Afisa Mitihani II – Mratibu wa Somo la Kiswahili.

Usaili wa maandishi na vitendo utafanyika tarehe 17 Oktoba 2024 katika kituo cha NECTA Mbezi Wani, Mbezi Makonde, Dar es Salaam. Usaili wa mahojiano ya ana kwa ana utafanyika tarehe 18 Oktoba 2024 katika ofisi za NECTA Mikocheni, Dar es Salaam.

Waombaji waliokidhi vigezo wameorodheshwa katika dokumenti ya Pdf iliopo mwishoni mwa chapisho hili chini, na wanatakiwa kufika katika eneo la usaili saa 1:00 asubuhi wakiwa na kitambulisho cha kazi na vyeti halisi vya elimu na taaluma.

Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na TCU, NACTE, au NECTA.

Majina ya watakaofaulu usaili wa maandishi na vitendo yatawekwa kwenye tovuti ya NECTA (www.necta.go.tz) tarehe 17 Oktoba 2024 kuanzia saa 12 jioni. Waombaji ambao majina yao hayatakuwa kwenye orodha hii hawakukidhi vigezo.

Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili NECTA Oktoba 2024

Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili NECTA Oktoba 2024

Majina ya waombaji walioitwa kwa usaili yanapatikana kwenye tovuti rasmi ya NECTA.

Kila mwombaji anashauriwa kutembelea tovuti ya baraza hilo, www.necta.go.tz, ili kujiridhisha na kuhakikisha jina lake lipo kwenye orodha. Majina ya watakaofaulu usaili wa kuandika pia yatachapishwa kwenye tovuti hiyo ifikapo jioni ya tarehe 17 Oktoba 2024.

Angalia Majina ya walioitwa kwenye usaili baraza la mitihani Tanzania Hapa Chini

ORODHA YA MAJINA YA WASAILIWA

Mambo ya Kuzingatia

  • Msailiwa anapaswa kujigharamia chakula, malazi, na usafiri.
  • Kwa waombaji waliosoma nje ya nchi, wanashauriwa kuhakikisha vyeti vyao vimehakikiwa na taasisi husika kama TCU, NACTE, au NECTA.
  • Usaili wa Kuandika utahusisha nafasi kama Afisa Mitihani II, wakuu wa masomo kama Chemistry, Physics, na Kiswahili pamoja na nafasi za ajira kama Dereva II, Internal Auditor, na Office Management Secretary.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Sifa za Kujiunga na JKT 2024, Mafunzo ya Kujitolea
  2. Nafasi za Kujiunga na JKT 2024/2025
  3. Vigezo & Sifa za Kujiunga na Mafunzo ya Kujitolea JKT 2024
  4. Majina ya Walioitwa kwenye Usaili Ajira Portal 2024
  5. Mfano wa Barua ya Maombi ya Nafasi ya Kujiunga JKT 2024
  6. Majina ya Waliochaguliwa Kujiunga na Jeshi la Polisi 2024
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo