Majina Ya Walioitwa Kwenye Usaili Mteknolojia Msaidizi Daraja La II 29/08/2024

Majina Ya Walioitwa Kwenye Usaili Mteknolojia Msaidizi Daraja La II 29/08/2024

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya MDAs & LGAs anapenda kuwataarifu  Waombaji Kazi wote walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa tarehe 10-09-2024 hatimaye  kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili huo.Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili  wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:

  1. Usaili utafanyika kuanzia tarehe kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili muda na sehemu ambapo usaili utafanyika umeainishwa kwa kila Kada.
  2. Kila msailiwa anatakiwa kufika kwenye eneo la usaili akiwa amevaa Barakoa (Mask)  3. Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;
  3. Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga  kura,Kitambulisho cha kazi,Kitambulisho cha Uraia, Hati ya kusafiria au barua ya utambulisho kutoka  Serikali ya Mtaa/Kijiji unachotoka.
  4. Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa,kidato cha IV, VI, Astashahada, Stashahada,Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji.
  5. Wasailiwa watakaowasilisha Testimonials, Provisional Results, Statement of results, hatiza matokeo za kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA  HAWATARUHUSIWAKUENDELEA NAUSAILI.
  6. Kila msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi.
  7. Kila Msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili.
  8. Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na  Mamlaka husika (kama TCU, NACTE au NECTA)
  9. Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi  vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya  tangazo husika.
  10. Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma wanapaswa kuja na vyeti vyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni za kufanyia kazi.
  11. Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wahakikishe wanaingia kwenye akaunti zao na kunakili namba ya mtihani kwa kuwa namba hizo hazitatolewa iku ya usaili
  12. Wasailiwa wote mnajulishwa kuwa hali ya hewa ya Jiji la Dodoma ni baridi hivyo mnashauriwa kuvaa nguo zinazohimili hali ya hewa ya ubaridi

Majina Ya Walioitwa Kwenye Usaili Mteknolojia Msaidizi Daraja La II

Majina Ya Walioitwa Kwenye Usaili Mteknolojia Msaidizi Daraja La II

Majina ya walioitwa kwenye usaili yamewekwa kwenye orodha inayopatikana kwenye tovuti rasmi ya Sekretarieti ya Ajira. Waombaji kazi wanapaswa kuhakikisha wananakili namba zao za mtihani kabla ya siku ya usaili, kwani namba hizo hazitatolewa tena siku ya usaili.

Kwa wale ambao hawakuitwa kwenye usaili, wanashauriwa kutokata tamaa bali waendelee kuomba nafasi zitakapotangazwa tena, huku wakizingatia mahitaji ya kila tangazo la kazi.

Sekretarieti ya Ajira inaendelea kusisitiza umuhimu wa kufuata maelekezo yote kwa umakini ili kuweza kufanikisha usaili na hatimaye kupata nafasi za ajira zinazotarajiwa.

Bofya Hapa Kupakua PDF yenye Taarifa Kamili ya Walioitwa Kwenye Usaili Mteknolojia Msaidizi Daraja La II

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili Kada za Afya MDAs & LGAs 28-08-2024
  2. Walioitwa Kwenye Usaili Tume ya Uchaguzi (NEC) 2024
  3. Mfano wa Barua ya Kuomba Kazi Ajira Portal
  4. Majina ya walioitwa kwenye Usaili Tume ya Utumishi wa Mahakama JSC
  5. Mfano wa Barua ya Kuomba Kazi ya Udereva
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo