Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili Kada ya Ualimu 2025 Mikoa Mbalimbali

Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili Kada ya Ualimu 2025 Mikoa Mbalimbali

Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili Kada ya Ualimu 2025 Mikoa Mbalimbali

Kama wewe ni miongoni mwa maelfu ya waombaji wa nafasi za kazi za ualimu zilizotangazwa na Wizara, Idara zinazojitegemea, Wakala za Serikali, Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa (MDAs & LGAs) kupitia Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma mwezi Agosti 2024, basi habari njema ni kwamba majina ya walioitwa kwenye usaili yametangazwa rasmi.

Baada ya muda mrefu wa kusubiri kwa hamu, hatimaye orodha ya majina ya walimu waliofuzu hatua ya awali imetolewa, ikiwapa fursa ya kuendelea katika mchakato wa kuwania nafasi hizo muhimu katika sekta ya elimu nchini. Tangazo hili linaashiria hatua muhimu kwa waombaji hawa kuelekea kutimiza ndoto zao za kuwa walimu. Hivyo, ni wakati wa kujipanga vyema kwa ajili ya usaili, ambao utakuwa ni kipimo cha uwezo, ujuzi, na umahiri wao katika fani hii adhimu.

Katika makala haya, tutakufahamisha kwa undani kuhusu orodha ya majina ya walioitwa kwenye usaili, maeneo na taasisi ambazo usaili utafanyika, pamoja na maelekezo muhimu kwa waombaji wote.

Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili Kada ya Ualimu 2025 Mikoa Mbalimbali

Orodha ya Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili Kwa Mikoa Mbalimbali

1. Mkoa wa Kilimanjaro

  • Usaili wa kuandika: Chuo cha Ushirika Moshi (MoCU)
  • Usaili wa mahojiano: Chuo cha Ushirika Moshi (MoCU)

2. Mkoa wa Lindi

  • Usaili wa kuandika: Shule ya Sekondari WAMA Sharaf-Mitwero
  • Usaili wa mahojiano: Shule ya Sekondari WAMA

3. Mkoa wa Manyara

  • Usaili wa kuandika: Chuo cha Uhasibu Arusha – Kampasi ya Babati
  • Usaili wa mahojiano: Chuo cha Uhasibu Arusha – Kampasi ya Babati

4. Mkoa wa Mara

  • Usaili wa kuandika: Chuo cha Maendeleo ya Jamii Buhare – Musoma
  • Usaili wa mahojiano: Chuo cha Maendeleo ya Jamii Buhare – Musoma

5. Mkoa wa Mbeya

  • Usaili wa kuandika: Catholic University of Mbeya (CUoM)
  • Usaili wa mahojiano: Chuo cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST)

6. Mkoa wa Morogoro

  • Usaili wa kuandika: Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Moringe Sokoine Campus – Jengo la Maabara Jumuishi
  • Usaili wa mahojiano: Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA)

Bofya hapa Kupakua Walioitwa Kwenye Usaili Kada Za Ualimu Mikoa Ya Kilimanjaro,Lindi,Manyara,Mara,Mbeya Na Morogoro 11-01-2025

7. Mkoa wa Geita

  • Usaili wa kuandika: Shule ya Sekondari ya Wasichana Nyankumbu & Shule ya Sekondari Mwatulole
  • Usaili wa mahojiano: Shule ya Sekondari ya Wasichana Nyankumbu

8. Mkoa wa Iringa

  • Usaili wa kuandika: Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa (MUCE), Kleruu Teachers’ College & Ruaha Catholic University (RUCU)
  • Usaili wa mahojiano: Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa

9. Mkoa wa Kagera

  • Usaili wa kuandika: Chuo cha VETA Mkoa wa Kagera – Burugo, Shule ya Sekondari ya Rugambwa, Shule ya Sekondari ya Ihungo & Shule ya Sekondari Bukoba

10. Mkoa wa Katavi

  • Usaili wa kuandika: Shule ya Sekondari ya Wasichana Mpanda
  • Usaili wa mahojiano: Shule ya Sekondari ya Wasichana Mpanda

11. Mkoa wa Kigoma

  • Usaili wa kuandika: Shule ya Sekondari Buronge
  • Usaili wa mahojiano: Shule ya Sekondari Kigoma

Bofya Hapa Kupakua Walioitwa Kwenye Usaili Kada Za Ualimu Mikoa Ya Geita,Iringa,Kagera,Katavi Na Kigoma 11-01-2025

12. Mkoa wa Arusha

  • Usaili wa kuandika: Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA)
  • Usaili wa mahojiano: Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA)

13. Mkoa wa Dar es Salaam

  • Usaili wa kuandika: Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo cha Usafirishaji (NIT), Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere & Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu DSM (DUCE)
  • Usaili wa mahojiano: Jengo la Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni

14. Mkoa wa Dodoma

  • Usaili wa kuandika: Chuo cha Dodoma (UDOM)
  • Usaili wa mahojiano: Ofisi za Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma (PSRS), eneo la Dr. Asha Rose Migiro

Bofya Hapa Kupakua

Walioitwa Kwenye Usaili Mikoa Ya Arusha,Dar Es Salaam Na Dodoma 11-01-2025

 Walioitwa Kwenye Usaili Kada Za Ualimu Mikoa Ya Simiyu, Singida, Songwe, Tabora, Tanga Na Zanzibar 11-01-2025

 Walioitwa Kwenye Usaili Mtwara,Mwanza,Njombe,Pwani,Rukwa,Ruvuma Shinyanga 11-01-2025

Maelekezo Muhimu kwa Waombaji

Kila msailiwa anatakiwa kufika katika kituo kilichopangwa kwa muda uliotajwa.

Waombaji wanashauriwa kufika na nyaraka muhimu kama barua ya mwaliko wa usaili, vitambulisho vyao, na cheti cha taaluma.

Ni muhimu kwa waombaji kuzingatia muda na kufuata maelekezo yaliyotolewa na mamlaka husika ili kuepuka changamoto zisizotarajiwa.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Mfano wa Barua ya Kuomba Kazi TRA (Tanzania Revenue Authority)
  2. Nafasi za Kazi Ualimu MDAs NA LGAs February 2025
  3. Mfumo wa Kutuma Maombi ya Ajira TRA (TRA recruitment Portal Login)
  4. Nafasi za Kazi TRA Februari 2025: Ajira Zaidi ya 1000 kwa Fani Mbalimbali
  5. Majina waliochaguliwa kujiunga na Mafunzo Jeshi la Uhamiaji 2025
  6. Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili Ualimu 2025 (Mikoa Mbalimbali)
  7. Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili Jeshi la Uhamiaji 2025
  8. Ajira Portal | Ajira Mpya za Walimu December 2024
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo