Majina Ya WALIOITWA Kwenye Usaili Jeshi La Zimamoto Na Uokoaji 2025

uSAILI JESHI LA ZIMAMOTO

Majina Ya WALIOITWA Kwenye Usaili Jeshi La Zimamoto Na Uokoaji 2025

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Tanzania limeanza rasmi kuwatumia barua pepe waombaji wa nafasi za ajira waliofanikiwa kuingia kwenye orodha ya walioitwa kwenye usaili. Hii ni kwa mujibu wa tangazo rasmi kutoka kwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, ambaye amethibitisha kuwa mchakato wa usaili utaanza rasmi mwezi Aprili 2025 kwa waombaji wa kada mbalimbali.

Majina Ya WALIOITWA Kwenye Usaili Jeshi La Zimamoto Na Uokoaji 2025

Majina Ya WALIOITWA Kwenye Usaili Jeshi La Zimamoto Na Uokoaji 2025 PDF

Bofya viungo vilivyopo Hapa Chini kupakua majina ya walioitwa kwenye usaili Zimamoto

Pakua Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili 

Pakua Orodha ya Walioitwa kwenye usaili Kidato Cha Nne

Pakua Orodha ya Walioitwa kwenye usaili Zimamoto Kwa Taaluma Mabambali

Ratiba ya Usaili na Maeneo ya Kufanyia

Kwa mujibu wa taarifa rasmi, usaili utafanyika katika maeneo yafuatayo kulingana na ngazi ya maombi:

Usaili utafanyika kuanzia tarehe 05 Aprili, 2025 hadi tarehe 17 Aprili, 2025 kuanzia saa 1:00 Asubuhi kwa kila kundi.

  • Waombaji waliomba ajira kwa elimu ya kidato cha nne usaili wao utafanyika kuanzia tarehe 05 hadi 09 Aprili, 2025 saa 1:00 Asubuhi kwenye mikoa walioichagua wakati wa kutuma maombi.
  • Waombaji wenye elimu ya Shahada na taaluma mbalimbali usaili wao utafanyika katika Ukumbi wa Andengenye – Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Dodoma kuanzia tarehe 14 Aprili hadi 17 Aprili, 2025 saa 1:00 Asubuhi kwa kila kundi.

Nyaraka Muhimu za Kuwasilisha

Waombaji wote walioitwa kwenye usaili wanatakiwa kuja na nyaraka halisi walizotumia wakati wa kutuma maombi ya kazi, ambazo ni:

  1. Vyeti vya kitaaluma
  2. Vyeti vya taaluma
  3. Cheti cha kuzaliwa
  4. Kitambulisho cha Taifa (NIDA) au Namba ya NIDA (NIN)
  5. Barua ya utambulisho
  6. Barua ya maombi ya kazi iliyoandikwa kwa mkono

Maelekezo Muhimu kwa Waombaji

Ili kuhakikisha usaili unafanyika kwa ufanisi, waombaji wote wanapaswa kuzingatia yafuatayo:

  • Kuhakikisha wanajitokeza kwa wakati kulingana na ratiba iliyotangazwa.
  • Kuvaa mavazi yanayofaa na ambayo hayatazuia kushiriki majaribio ya ukimbiaji.
  • Kuendelea kufuatilia taarifa zaidi kupitia akaunti zao na kurasa rasmi za mitandao ya kijamii za Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.

Pia Vijana walioitwa kwenye usaili wametakiwa Kuzingatia yafuatayo:

  1. Kila mmoja anatakiwa kufika kwenye usaili siku na tarehe aliyopangiwa na si vinginevyo.
  2. Kuwa nadhifu na kuvaa mavazi ya staha.
  3. Kufika na vyeti vyote halisi vilivyotumika kwenye maombi ya ajira kama vile cheti cha Kidato cha nne, Kidato cha sita, Cheti cha taaluma, cheti cha kuzaliwa, pamoja na Kitambulisho cha Taifa au Namba ya kitambulisho cha Taifa (NIDA)
  4. Kwa walioomba nafasi ya Udereva pamoja na maelekezo hayo wanatakiwa kuja na leseni halisi ya udereva Daraja E.
  5. Gharama za usafiri, chakula na malazi ni juu ya msailiwa kwa muda wote atakaokuwa kwenye usaili.
  6. Vijana watakaofanya usaili Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wazingatie tarehe zao za usaili. Aidha, atakayekuja tarehe ambayo haijapangwa hatapokelewa.

Jinsi ya Kupata Majina ya Walioitwa

Majina ya waombaji waliofanikiwa kuingia kwenye orodha ya walioitwa kwenye usaili tayari yametangazwa. Waombaji wanashauriwa kuingia kwenye akaunti zao walizotumia wakati wa kutuma maombi ili kuona kama wameitwa kwenye usaili.

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linawahimiza waombaji wote kufuata maelekezo yaliyotolewa kwa umakini ili kuhakikisha wanajiandaa vyema kwa usaili huu muhimu. Kwa taarifa zaidi na masasisho ya mara kwa mara, waombaji wanashauriwa kufuatilia mitandao rasmi ya kijamii ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji. Aidha, pdf yenye orodha rasmi ya majina pamoja na taarifa za ziada zitawekwa katika chapisho hili pindi itakapotangazwa rasmi. Tunawatakia kila la heri waombaji wote katika mchakato wa usaili wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji 2025.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Mfano wa Barua ya Maombi ya Kazi Jeshi la Polisi 2025
  2. Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili TRA 2025 pdf
  3. Nafasi za Kujiunga na Jeshi la Polisi 2025
  4. Mwisho wa Kutuma Maombi Ajira Mpya Jeshi la Polisi Tanzania 2025
  5. Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili TRA Kutangazwa Machi 22, 2025
  6. Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili MDAs NA LGAs 2025
  7. Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili MDAs NA LGAs 2025
  8. Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili NEC 2025 Mkoa wa Dar es Salaam
  9. Mfano wa Barua Ya Maombi ya Kazi Jeshi la Zimamoto 2025
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo