Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili Jeshi la Uhamiaji 2025
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Uhamiaji ametangaza rasmi orodha ya majina ya waombaji walioitwa kushiriki usaili wa ajira kwa mwaka 2025. Tangazo hili linawahusu wale walioomba nafasi za ajira kupitia Mfumo wa e-Ajira wa Idara ya Uhamiaji na waliopokea taarifa kupitia barua pepe au ujumbe mfupi wa simu.
Waombaji wote wanatakiwa kufika katika vituo vya usaili vilivyotengwa ifikapo saa 1:00 asubuhi tarehe 15 Januari 2025.
Waombaji walioomba nafasi za kazi Tanzania Bara wanapaswa kufika katika Ukumbi wa Maktaba (Library) Ndaki ya Elimu (CoED) Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM). Waombaji wa Zanzibar wanatakiwa kufika katika Ukumbi wa Dkt. Ali Mohamed Shein Hall uliopo Tunguu Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Ili kushiriki katika usaili huu, waombaji wote wanatarajiwa kuwa na vitu vifuatavyo: Namba ya ombi la Ajira (Application ID) kama ilivyochapishwa kwenye barua pepe au ujumbe wa simu, kitambulisho chenye picha (kama vile Kitambulisho cha Taifa, Kitambulisho cha Mkazi, Kadi ya Mpiga Kura, Pasipoti au kitambulisho kingine chochote kinachotambulika), na kalamu ya wino wa bluu kwa ajili ya kuandika.
Waombaji wenye fani za TEHAMA na ufundi magari wanapaswa kujiandaa kwa usaili wa vitendo (Practical Examination) ambao utawajaribu katika ujuzi na uwezo wao katika fani husika.
Ni muhimu kutambua kwamba waombaji wote wanatakiwa kujigharamia chakula, usafiri na malazi wakati wote wa zoezi la usaili.
Waombaji wote wanakumbushwa kufika kwa wakati na kuzingatia maadili ya usaili. Vaa nguo nadhifu na zenye heshima, na hakikisha unafika na vitendea kazi vyote muhimu. Uaminifu na uadilifu ni sifa muhimu kwa afisa yeyote wa Uhamiaji, hivyo waombaji wanapaswa kuzingatia hili wakati wote wa usaili.
Tarehe na Vituo vya Usaili Uhamiaji 2025
Waombaji wanatakiwa kufika katika vituo vya usaili kama ilivyoainishwa hapa chini:
Tanzania Bara:
- Eneo: Ukumbi wa Maktaba (Library), Ndaki ya Elimu (CoED), Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
- Tarehe: 15 Januari 2025.
- Saa: Saa 1:00 asubuhi.
Zanzibar:
- Eneo: Ukumbi wa Dkt. Ali Mohamed Shein Hall, Tunguu, Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja.
- Tarehe: 15 Januari 2025.
- Saa: Saa 1:00 asubuhi.
Orodha ya Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili Uhamiaji 2025
Orodha ya majina ya waombaji walioitwa kwenye usaili inapatikana katika tovuti ya Idara ya Uhamiaji (www.immigration.go.tz). Waombaji wanashauriwa kutembelea tovuti hii ili kuhakikisha kama wameitwa kwenye usaili.
Tangazo Kuitwa Usaili, Januari 2025Kumbuka, usaili huu ni hatua muhimu katika mchakato wa kujiunga na Jeshi la Uhamiaji. Waombaji wote wanapaswa kujiandaa vya kutosha ili waweze kuonyesha uwezo wao na kutimiza ndoto zao za kuitumikia Tanzania. Bahati nzuri kwa wote!
Mapendekezo ya Mhariri:
- Ajira Portal | Ajira Mpya za Walimu December 2024
- Mfumo wa Maombi ya Ajira Uhamiaji Recruitment Portal (Immigration Recruitment Portal)
- Nafasi za Kazi Benki Kuu ya Tanzania BOT December 2024
- Mfano wa Barua ya Maombi ya Kazi Jeshi la Uhamiaji
- Majina Ya Walioitwa Kazini Utumishi Na Ajira Portal 30 November 2024
Leave a Reply