Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili Jeshi la Polisi Tanzania April 2025

Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili Jeshi la Polisi Tanzania April 2025

Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili Jeshi la Polisi Tanzania April 2025

Jeshi la Polisi Tanzania limetangaza rasmi orodha ya majina ya walioitwa kwenye usaili wa ajira kwa mwezi Aprili 2025. Tangazo hili linawahusu waombaji wote waliowasilisha maombi yao kupitia Tanzania Police Force Recruitment Portal, ambapo zoezi la usaili limepangwa kufanyika kuanzia tarehe 28 Aprili hadi 11 Mei 2025 katika maeneo mbalimbali nchini.

Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili Jeshi la Polisi Tanzania April 2025

Maelezo Muhimu Kuhusu Usaili Jeshi la Polisi Tanzania April 2025

Usaili wa ajira ya Jeshi la Polisi utahusisha waombaji kutoka makundi mbalimbali kulingana na kiwango cha elimu walichokipata.

Kwa wale waliokuwa na elimu ya Shahada, Stashahada na Astashahada, usaili utafanyika jijini Dar es Salaam katika Uwanja wa Gwaride ulio ndani ya Kambi ya Polisi, barabara ya Kilwa, nyuma ya Kituo cha Polisi cha Kilwa Road.

Kwa waombaji wenye elimu ya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita, usaili utahudhuriwa katika maeneo ya makamanda wa polisi wa mikoa waliyochagua wakati wa kuwasilisha maombi yao. Hii ni hatua muhimu inayowawezesha waombaji kufanya usaili katika mikoa yao ili kuondoa usumbufu wa kusafiri mbali.

Kwa upande wa waombaji kutoka Zanzibar, usaili utatofautiana kulingana na kiwango cha elimu. Waombaji wenye Shahada, Stashahada, Astashahada, Kidato cha Sita na Kidato cha Nne watafanya usaili katika maeneo maalum yaliyopo Unguja na Pemba.

Katika mkoa wa Unguja, usaili utafanyika Makao Makuu ya Polisi Zanzibar (Ziwani), wakati mikoa ya Pemba itakuwa na usaili katika Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba (Chakechake).

Vitu Muhimu vya Kubeba kwa Usaili

Kila msailiwa atatakiwa kufika katika eneo la usaili akiwa na vyeti halisi vya elimu (Academic certificates), cheti cha kuzaliwa, kitambulisho cha Taifa cha NIDA au namba ya NIDA. Aidha, waombaji wanapaswa kuwa na nguo na viatu vya michezo, kwani usaili utahusisha majaribio ya kimichezo.

Ratiba ya Usaili Jeshi la Polisi Tanzania April 2025 na Maeneo

Usaili utaanza rasmi tarehe 28 Aprili 2025 saa 07:00 asubuhi na utaendelea hadi tarehe 11 Mei 2025.

Ni muhimu kwa waombaji kufika kwa wakati katika maeneo yaliyotangazwa. Msailiwa yeyote atakayefika baada ya tarehe 28 Aprili 2025 hataweza kuhudhuria usaili, na hivyo atakuwa ameondolewa katika mchakato.

PDF ya Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili Jeshi la Polisi Tanzania April 2025

BOFYA HAPA KUPAKUA RODHA YA WALIOITWA KWENYE USAILI

Mapenekezo ya Mhariri:

  1. Majina Ya WALIOITWA Kwenye Usaili Jeshi La Zimamoto Na Uokoaji 2025
  2. Usaili Jeshi la Zimamoto 2025 Kuanza Aprili 5 – 17, 2025
  3. Mfano wa Barua ya Maombi ya Kazi Jeshi la Polisi 2025
  4. Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili TRA 2025 pdf
  5. Nafasi za Kujiunga na Jeshi la Polisi 2025
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo