Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili Jeshi La Polisi July 2024, Usaili Ajira Mpya Jeshi La Polisi Tanzania 2024 , Ajira Tanzania , Jeshi La Polisi Tanzania Interview , Walioitwa Kwenye Usaili Jeshi La Polisi » Jeshi La Polisi
Jeshi la Polisi Tanzania kupitia Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania, Camilius Wambura, limetangaza majina ya walioitwa kwenye usaili jeshi la polisi 2024 kwa nafasi za ajira zilizotangazwa kupitia mfumo wa Ajira TANZANIA POLICE FORCE RECRUITMENT PORTAL.
Usaili huu unatarajiwa kuanza kuanzia tarehe 29 Julai 2024 hadi tarehe 11 Agosti 2024. Usaili kwa vijana waliochaguliwa utafanyika katika maeneo mbalimbali nchini kulingana na ngazi ya elimu na eneo la waombaji.
Taarifa Muhimu Kwa Waliochaguliwa kwenye usaili jeshi la polisi 2024
Vijana wote waliochaguliwa kwenye usaili Jeshi la Polisi Tanzania wanapaswa kufahamu taarifa muhimu kuhusu usaili, ikiwa ni pamoja na maeneo ya kufanyia usaili, vitu vya kubeba na mahitaji maalum kwa ajili ya usaili. Ni muhimu kuzingatia taarifa hizi ili kuhakikisha mchakato wa usaili unafanyika kwa ufanisi na bila usumbufu wowote.
TAARIFA MPYA: Majina ya Waliochaguliwa Kujiunga na Jeshi la Polisi 2024
1. Tanzania Bara
Wenye Elimu ya Juu (Shahada, Stashahada, na Astashahada): Waombaji walio na elimu hizi watafanyiwa usaili jijini Dar es Salaam katika Chuo cha Taaluma ya Polisi (DPA) kilichopo Barabara ya Kilwa, Kurasini.
Waombaji wanatakiwa kufika na nyaraka zote muhimu kama vile vyeti vya taaluma, cheti cha kuzaliwa, na kitambulisho cha Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) au namba ya utambulisho wa Taifa (NIDA).
Wenye Elimu ya Sekondari (Kidato cha Nne na Sita): Usaili utafanyika katika mikoa waliyochagua wakati wa kutuma maombi yao. Ni muhimu kuhakikisha kuwa wamebeba vyeti halisi vya taaluma, cheti cha kuzaliwa, na kitambulisho cha NIDA.
2. Zanzibar
Wenye Elimu ya Juu (Shahada, Stashahada, na Astashahada), Kidato cha Sita na Nne: Usaili kwa waombaji wa Zanzibar utafanyika katika maeneo mawili tofauti kulingana na eneo walilopo:
- Unguja: Usaili utafanyika Makao Makuu ya Polisi Zanzibar. Waombaji wote wanatakiwa kuwa na vyeti halisi vya taaluma, cheti cha kuzaliwa, na kitambulisho cha NIDA.
- Pemba: Usaili utafanyika Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba, Chakechake. Waombaji wanapaswa kuhakikisha wana nyaraka zote muhimu za usaili.
Mahitaji ya Usaili Jeshi La Polisi 2024
Waombaji wote wanatakiwa kufika kwenye usaili wakiwa na nyaraka zifuatazo:
- Vyeti halisi vya taaluma (academic certificates).
- Cheti cha kuzaliwa.
- Kitambulisho cha Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) au namba ya utambulisho wa Taifa (NIDA).
- Nguo na viatu vya michezo kwa ajili ya mazoezi.
Kumbuka: Kijana yeyote atakayefika kwenye usaili baada ya tarehe 29 Julai 2024 hatapokelewa.
Majina ya walioitwa kwenye usaili jeshi la polisi 2024
Orodha ya majina ya waliochaguliwa kufanya usaili jeshi la Polisi imeambatishwa katika pdf hapa chini. Ni muhimu kwa kila mwombaji kuhakikisha kuwa jina lake linapatikana kwenye orodha ili kujitayarisha ipasavyo kwa ajili ya usaili.
TANGAZO-LA-KUITWA-KWENYE-USAILI-WWW.HABARIFORUM.COMJeshi la Polisi linawahimiza waombaji wote kuhakikisha wanazingatia tarehe na mahitaji ya usaili ili kuepuka usumbufu wowote.
Usaili huu ni hatua muhimu katika kuhakikisha kwamba Jeshi la Polisi linapata vijana wenye sifa stahiki za kujiunga na kulinda usalama wa raia na mali zao. Kwa taarifa zaidi na orodha kamili ya majina ya walioitwa kwenye usaili, tembelea tovuti rasmi ya Jeshi la Polisi au wasiliana na ofisi za polisi za karibu.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Ajira Mpya za Walimu Tanzania 2024: Nafasi 11,015 Zatangazwa, Maombi Hadi Agosti 2
- Nafasi Mpya za Kazi Almashauri ya Wilaya ya Kibiti (Mwisho wa Maombi 28 Julai, 2024)
- Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Yatangaza Nafasi za Kazi (Mwisho 25/07/2024)
- Tangazo La Nafasi Za Kazi Halmashauri Ya Wilaya Ya Mbogwe (Mwisho Wa Maombi 26 Julai 2024)
Leave a Reply