Majina ya Waliochaguliwa kujiunga Chuo Kikuu Cha UDSM 2024/2025

Majina ya Waliochaguliwa kujiunga Chuo Kikuu Cha UDSM 2024 2025

Majina ya Waliochaguliwa kujiunga Chuo Kikuu Cha UDSM 2024/2025 | Waliochaguliwa Chuo Kikuu cha Dar es salaam

Kupata nafasi ya kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ni hatua kubwa katika safari ya elimu ya kila mwanafunzi nchini Tanzania. Nafasi hii ni fursa ya kipekee ya kujifunza kutoka kwa wataalamu wenye uzoefu wa hali ya juu, kufanya utafiti wa kina, na kuchangia katika maendeleo ya jamii. Katika mwaka wa masomo wa 2024/2025, maelfu ya wanafunzi waliohitimu elimu ya A-level na shashahada wameomba kujiunga na kozi mbalimbali za shahada ya kwanza (Degree) ambazo zinatolewa na chuo kikuu cha UDSM, na sasa, wakati umefika wa kuangalia kama ndoto zao za kujiunga na chuo hiki bora zimetimia.

Angalia Hapa Majina ya Waliochaguliwa Chuo Cha UDSM Awamu ya Pili 2024/2025

Historia Fupi ya Chuo cha UDSM: Kutoka Chuo Kidogo Hadi Taasisi Kubwa

Kabla ya kuzama katika mchakato wa kuangalia majina ya waliochaguliwa kujiunga chuo kikuu cha UDSM 2024/2025, hebu tuangalie kwa ufupi historia ya UDSM. Chuo kikuu cha Dar es salaam (University of Dar es salaam) almaarufu kama UDSM kilianzishwa tarehe 25 Oktoba 1961 kama Chuo cha Kikuu cha Dar es Salaam (UCD), ambacho kilikuwa tawi la Chuo Kikuu cha London. Kilianza na Kitivo kimoja tu, Kitivo cha Sheria, ambacho kilikuwa na wanafunzi 14, mmoja wao akiwa mwanafunzi wa kike aitwaye Julie Manning.

Mwaka 1963, chuo hiki kilikua kuwa sehemu ya Chuo Kikuu cha Afrika Mashariki pamoja na Chuo Kikuu cha Makerere (Uganda) na Chuo Kikuu cha Nairobi (Kenya). Tarehe 1 Julai 1970, UDSM kilipata hadhi kamili ya chuo kikuu kwa mujibu wa Sheria Na. 12 ya mwaka huo.

Tangu wakati huo, UDSM imekua kwa kasi katika nyanja mbalimbali ikiwemo idadi ya wanafunzi, vitivo, uwezo wa utafiti, na programu za kitaaluma. Chuo hiki kinajumuisha vyuo vya tawi, shule, na taasisi mbalimbali zinazotoa programu za shahada, stashahada, astashahada, na mafunzo ya cheti. UDSM pia inatoa programu za masomo ya jioni ambazo zinawalenga hasa watu wanaofanya kazi, ingawa mtu yeyote mwenye sifa zinazohitajika anaweza kujiunga.

Leo, UDSM kina vyuo vikuu vingine, shule, na taasisi mbalimbali zinazotoa mamia ya programu za masomo katika nyanja mbalimbali ngazi tofauti tofauti za elimu, ikiwa ni pamoja na sayansi, uhandisi, biashara, sanaa, na sheria. Chuo hiki kinajivunia kuwa na wahadhiri wenye sifa za juu, vifaa vya kisasa, na mazingira mazuri ya kujifunzia.

Majina ya Waliochaguliwa kujiunga Chuo Kikuu Cha UDSM 2024/2025

Kwa wale walioomba kujiunga na chuo cha UDSM mwaka 2024/2025, kuna njia mbili kuu za kuangalia kama wamechaguliwa:

1. Kupitia Ujumbe Mfupi wa Simu (SMS)

  • UDSM itatuma SMS kwa wanafunzi waliochaguliwa kwenye namba za simu walizotumia wakati wa kutuma maombi ya kujiunga na chuo.
  • Ujumbe huu utakuwa na maelezo muhimu, ikiwa ni pamoja na kozi ambayo mwanafunzi amechaguliwa
  • Hakikisha namba yako ya simu inafanya kazi na ipo sehemu yenye mtandao wa kutosha kupokea ujumbe.

Kama hujapokea SMS kufikia tarehe ya mwisho ya kuthibitisha udahili, tumia njia ya pili (online) kuangalia kama umechaguliwa.

2. Kutumia Mfumo wa Maombi ya Mtandaoni (Online Admission System)

  1. Tembelea tovuti rasmi ya UDSM OAS (https://admission.udsm.ac.tz/).
  2. Tafuta sehemu ya “Admissions” au “Kuangalia Majina ya Waliochaguliwa”.
  3. Ingia kwenye akaunti yako kwa kutumia jina la mtumiaji na nenosiri ulilounda wakati wa kuomba.
  4. Mara baada ya kuingia, utaona ujumbe unaoonyesha kama umechaguliwa au la.Kama umechaguliwa, utaona maelezo ya kozi uliyopangiwa.
  5. Ili kuthibitisha udahili wako, utahitajika kuingiza msimbo maalum (SPECIAL CODE) utakaotumwa kwako kwa njia ya SMS.

Majina ya Waliochaguliwa kujiunga Chuo Kikuu Cha UDSM 2024/2025

Waliochaguliwa kujiunga Chuo Kikuu Cha UDSM

Mambo ya Kuzingatia kwa Waliochaguliwa kujiunga Chuo Kikuu Cha UDSM 2024/2025

Hongera sana kama umechaguliwa kujiunga na UDSM! Lakini safari yako haishii hapo. Hapa kuna hatua muhimu unazopaswa kuchukua:

  • Thibitisha Udahili Wako: Hakikisha unathibitisha udahili wako kabla ya tarehe ya mwisho iliyoainishwa na UDSM. Kutothibitisha kunaweza kusababisha nafasi yako kupewa mwanafunzi mwingine.
  • Soma kwa Makini Fomu za Kujiunga: UDSM itatoa fomu za kujiunga ambazo utahitajika kuzijaza na kuzirejesha. Soma fomu hizi kwa makini na uhakikishe unatoa taarifa sahihi.
  • Lipa Ada na Gharama Nyingine: UDSM itatoa maelezo kuhusu ada ya masomo na gharama nyingine zinazohitajika. Hakikisha unalipa ada kwa wakati ili kuepuka matatizo yoyote.
  • Jiandae kwa Maisha ya Chuo Kikuu: Maisha ya chuo kikuu ni tofauti na maisha ya shule ya sekondari. Jiandae kwa changamoto mpya na fursa nyingi za kujifunza na kukua.

Mapendekezo ya Mhariri;

  1. Majina Ya Waliochaguliwa Kujiunga Na Chuo Kikuu Cha SUA 2024/2025
  2. Majina ya Waliochaguliwa kujiunga na vyuo Vikuu 2024/2025
  3. Majina ya waliochaguliwa Chuo Kikuu Cha UDOM 2024/2025
  4. Kozi Za VETA na Gharama zake 2024/2025
  5. Ada Za Chuo Cha NIT 2024/2025
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo