Majina ya Waliochaguliwa Kidato cha Tano 2025/2026 (Form Five Selection)

Majina ya Waliochaguliwa Kidato cha Tano

Majina ya Waliochaguliwa Kidato cha Tano 2025/2026 (Form Five Selection) | Majina ya wanafunzi waliochaguliwa na TAMISEMI kujiunga Kidato cha Tano 2025/2026 | TAMISEMI Form Five Selection

Majina ya Waliochaguliwa Kidato cha Tano 2025/2026 (Form Five Selection)

Kutangazwa kwa Majina ya Waliochaguliwa Kidato cha Tano kwa mwaka wa masomo 2025/2026 almaharufu kama TAMISEMI Form Five Selection ni taarifa ya msingi inayosubiriwa kwa hamu na wanafunzi waliomaliza elimu ya sekondari, pamoja na wazazi na walezi wao kote nchini Tanzania. Taarifa hii inaashiria mwanzo wa hatua mpya katika safari ya kitaaluma ya wanafunzi, ikiashiria mpito kutoka elimu ya sekondari ya chini kuelekea sekondari ya juu na hatimaye, maandalizi kwa elimu ya juu na soko la ajira.

Kupitia mchakato huu, serikali kupitia Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), huendesha upangaji wa wanafunzi waliofaulu Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne (CSEE), kwa kuzingatia ufaulu wao, uchaguzi wa tahasusi, na nafasi zilizopo katika shule mbalimbali nchini. Hatua hii hufuata misingi ya uwazi, usawa, na haki kwa kila mwanafunzi aliyekidhi vigezo vya kitaaluma.

Katika makala hii, wasomaji watapata mwongozo wa kina kuhusu vigezo vinavyotumika katika upangaji wa wanafunzi, hatua rasmi za kuangalia majina ya waliochaguliwa, pamoja na taratibu zinazofuata baada ya uteuzi. Lengo ni kuwawezesha wanafunzi na wazazi kupata taarifa sahihi, kwa wakati, na kwa kutumia njia zilizo rasmi.

Mchakato wa Kuchaguliwa Kidato cha Tano 2025/2026

Mchakato wa kuchagua wanafunzi wataojiunga na shule za serikali za kidato cha tano unafanywa kwa umakini na uwazi mkubwa, huku Ofisi ya Rais – TAMISEMI ikitoa orodha rasmi ya majina ya wanafunzi waliofaulu na shule walizopangiwa. Uchaguzi huu huzingatia vigezo kadhaa, ikiwa ni pamoja na matokeo ya kitaaluma ya mwanafunzi, machaguo ya masomo, na upatikanaji wa nafasi katika shule husika.

Kwa mwaka wa masomo 2025/2026, wanafunzi wanapaswa kutembelea tovuti rasmi ya TAMISEMI ili kutafuta matokeo yao kwa urahisi. Kupitia makala hii, tutatoa mwongozo wa hatua kwa hatua ili kuhakikisha kila mwanafunzi anapata majina yake na shule alizopangiwa.

Vigezo Vinavyotumika Katika Upangaji wa Wanafunzi 2025/2026

TAMISEMI hutekeleza mchakato wa upangaji kwa kuzingatia vigezo vilivyo rasmi na vinavyolenga kuhakikisha usawa katika upatikanaji wa fursa za elimu ya sekondari ya juu. Miongoni mwa vigezo vinavyotumika ni pamoja na:

  1. Ufaulu wa Masomo: Mwanafunzi anatakiwa kuwa na angalau alama za A, B au C katika masomo yasiyo ya dini, ikiwa ni kiashiria cha uwezo wake kitaaluma.
  2. Tahasusi Aliyochagua: Uchaguzi wa masomo maalum (tahasusi) ni kipengele muhimu, kwani huathiri shule atakayopangiwa mwanafunzi.
  3. Upatikanaji wa Nafasi: Idadi ya nafasi katika kila shule huathiri mchakato wa upangaji, hasa katika shule zenye ushindani mkubwa.
  4. Umri wa Mwanafunzi: Mwanafunzi anatakiwa kuwa na umri wa chini ya miaka 25 ili kupangiwa nafasi ya kidato cha tano katika shule za serikali.

Ni Lini Majina ya Waliochaguliwa Kidato cha Tano 2025/2026 Yatatangazwa?

Taarifa rasmi kuhusu lini majina ya waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano kwa mwaka wa masomo 2025/2026 yatatangazwa hutolewa na Ofisi ya Rais – TAMISEMI. Kwa kuzingatia utaratibu wa miaka ya nyuma, orodha ya kwanza ya waliochaguliwa (First Selection) hutangazwa kati ya mwezi Mei na Juni, mara baada ya matokeo ya mtihani wa taifa wa kidato cha nne (CSEE) kutangazwa rasmi na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) mapema mwezi Januari.

Kwa mujibu wa ratiba ya mwaka huu:

  • Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) 2024 yalitangazwa mwezi Januari 2025.
  • Uteuzi wa Awamu ya Kwanza (First Selection) unatarajiwa kutolewa mapema mwezi Juni 2025.
  • Uteuzi wa Awamu ya Pili (Second Selection), ikiwa utahitajika, unatarajiwa kufanyika mwezi Septemba 2025.

Ni muhimu kwa wanafunzi na wazazi kufuatilia tovuti rasmi ya TAMISEMI kupitia selform.tamisemi.go.tz kwa ajili ya taarifa sahihi na za wakati kuhusu kutangazwa kwa majina hayo. Aidha, vyombo vya habari vya serikali na mitandao ya kijamii ya TAMISEMI hutumika pia kama vyanzo rasmi vya kutangaza taarifa hizi.

Jinsi ya Kuangalia Majina ya Waliochaguliwa Kidato cha Tano 2025/2026 (Form Five Selection)

Ili kupata orodha rasmi ya majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano, ni muhimu kufuata taratibu zilizoainishwa na TAMISEMI kupitia mfumo wa mtandaoni. Hapa chini ni hatua muhimu za kufuata:

1. Tembelea Tovuti Rasmi ya TAMISEMI

Fungua kivinjari chako (browser) kisha nenda kwenye tovuti rasmi ya TAMISEMI kupitia anuani: https://selform.tamisemi.go.tz. Hii ndiyo njia salama na ya kuaminika kupata majina ya wanafunzi waliochaguliwa.

Majina ya Waliochaguliwa Kidato cha Tano 2025/2026 (Form Five Selection)

2. Chagua Kipengele cha “Form Five Selection”

Baada ya kufika kwenye tovuti, bonyeza kiungo kinachosema “Selection Results” au “Form Five Selection 2025” ili kufungua ukurasa wa matokeo.

3. Chagua Mkoa, wilaya na Shule ya Sekondari Ulipofanya Mtihani

Chagua jina la mkoa na wilaya ulipo fanya mtihani wa kidato cha nne, kisha tafuta shule yako katika orodha inayotolewa.

Form Five Selection

4. Pakua na Angalia Orodha ya Majina ya Waliochaguliwa

Baada ya kuchagua shule, orodha ya wanafunzi waliochaguliwa itajitokeza, ikiwa ni pamoja na shule walizopangiwa. Majina yanaonyeshwa kulingana na ufaulu na machaguo ya masomo.

5. Chukua Hatua Muhimu Baada ya Kupata Taarifa

Mara baada ya kuona jina lako na shule, hakikisha unachukua hatua muhimu kama vile kujiandaa kwa mahitaji ya shule na kuripoti kwa wakati.

Awamu za Majina ya Waliochaguliwa Kidato cha Tano 2025/2026

Baada ya kutangazwa kwa majina, wanafunzi waliochaguliwa huorodheshwa katika awamu mbili za uchaguzi:

  • Uchaguzi wa Kwanza; Hii ni orodha ya wanafunzi waliofanikiwa kupata nafasi katika shule za kidato cha tano. Wanafunzi hawa watalazimika kuchukua hatua kama vile kupakua barua ya kujiunga na shule zao na kujiandaa kwa ratiba ya kuripoti.
  • Uchaguzi wa Pili; Ikiwa mwanafunzi hakupata nafasi katika awamu ya kwanza, anaweza kufuatilia uteuzi wa awamu ya pili. TAMISEMI hutangaza orodha hii baada ya awamu ya kwanza, na inahusisha wanafunzi waliokidhi vigezo lakini hawakupata nafasi kwa sababu ya ushindani wa nafasi.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Majina ya Wanafunzi na Shule Walizopangiwa Kidato cha Tano 2025/2026
  2. Jinsi ya Kuangalia Majina ya Waliochaguliwa Kidato cha Tano 2025/2026
  3. Ni Lini TAMISEMI Itatangaza Majina ya Waliochaguliwa Kidato cha Tano 2025/2026?
  4. Orodha ya Shule Nzuri za Advanced za Serikali Tanzania
  5. Sifa za Kuchaguliwa Kidato cha Tano 2025
  6. Sifa za Kujiunga na Jeshi La Polisi Tanzania 2025
  7. NECTA Matokeo ya Kidato Cha Pili 2024 (Form Two Results)
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo