Majina ya Waliochaguliwa Kidato cha Kwanza 2025

Vigezo vya Kuchaguliwa Kidato cha Kwanza

Majina ya Waliochaguliwa Kidato cha Kwanza 2025

Dar es Salaam. Serikali imetangaza rasmi majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka wa masomo wa 2025. Jumla ya wanafunzi 974,332, sawa na asilimia 100 ya watahiniwa waliokidhi vigezo vya kufaulu mtihani wa kumaliza elimu ya msingi wa mwaka 2024, wamepangiwa shule mbalimbali za sekondari nchini.

Kati ya wanafunzi hao, wasichana ni 525,225 na wavulana 449,107, na wote wamepangiwa shule kwa awamu moja. Hii ni hatua muhimu inayosisitiza dhamira ya serikali kuhakikisha kila mtoto aliyefaulu anapata nafasi ya kuendelea na masomo yake ya sekondari.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mheshimiwa Mohammed Mchengerwa, alitoa tangazo hilo katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Alieleza kuwa mchakato wa uteuzi ulifuata mwongozo wa Wizara ya Elimu, Sayansi, na Teknolojia na kwamba wanafunzi wote waliofaulu kwa alama kati ya 121 na 300 wamechaguliwa kujiunga na shule za sekondari za serikali.

“Maandalizi yote yamekamilika kuhakikisha wanafunzi wote waliofaulu mtihani wa PSLE 2024 wananza masomo yao ifikapo Januari 13, 2025,” alisema Mheshimiwa Mchengerwa.

Majina ya Waliochaguliwa Kidato cha Kwanza 2025

Mchakato wa Uteuzi wa Wanafunzi wa Kujiunga Form One 2025

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Bw. Mohammed Mchengerwa, alitoa taarifa hii wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam. Alieleza kuwa uteuzi wa wanafunzi umezingatia miongozo iliyotolewa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

“Uteuzi huu umefanyika kwa kuzingatia ufaulu wa wanafunzi katika mtihani wa Darasa la Saba. Wanafunzi wote waliopata alama kati ya 121 hadi 300 wamepangiwa shule za sekondari za Serikali,” alisema Bw. Mchengerwa.

Aidha, alibainisha kuwa shule hizo zimegawanywa katika makundi mawili makuu:

  1. Shule za Bweni: Zimejumuisha shule maalum, shule za bweni za kiufundi, na shule za bweni za kitaifa.
  2. Shule za Kutwa: Ambazo zimepangiwa wanafunzi walio karibu na maeneo wanayoishi.

Waliochaguliwa Kidato cha Kwanza 2025 Shule Maalum na Vipaji Maalum

Kwa upande wa shule maalum, jumla ya wanafunzi 809 (329 wasichana na 480 wavulana) wamechaguliwa kujiunga na shule zinazohudumia wanafunzi wenye ufaulu wa hali ya juu. Baadhi ya shule hizi ni pamoja na:

  1. Msalato
  2. Mzumbe
  3. Kilakala
  4. Kibaha
  5. Ilboru
  6. Tabora Girls
  7. Tabora Boys

Waliochaguliwa Kidato cha Kwanza 2025 Shule za Bweni za Kiufundi

Shule za kiufundi zimepangiwa wanafunzi 1,174 (197 wasichana na 977 wavulana). Shule hizi zinatoa mafunzo maalum ya kiufundi na zinajumuisha:

  1. Tanga Tech
  2. Moshi Tech
  3. Musoma Tech
  4. Bwiru Boys
  5. Ifunda Tech
  6. Iyunga Tech
  7. Mtwara Tech
  8. Mwadui Tech
  9. Chato Tech

Waliochaguliwa Kidato cha Kwanza 2025 Shule za Bweni za Kitaifa

Kwa upande wa shule za kitaifa, jumla ya wanafunzi 6,810 (5,199 wasichana na 1,611 wavulana) wamechaguliwa kujiunga. Hii ni pamoja na wasichana 3,320 waliopangiwa shule za sayansi za mkoa.

Shule za Kutwa

Idadi kubwa ya wanafunzi, yaani 965,539 (519,500 wasichana na 446,039 wavulana), wamechaguliwa kujiunga kidato cha kwanza katika shule za kutwa za Serikali karibu na maeneo yao ya makazi. Hii imezingatia urahisi wa kusafiri na kuhakikisha wanafunzi wote wanapata nafasi ya kuanza masomo bila changamoto kubwa.

Maandalizi ya Mwaka wa Masomo 2025

Bw. Mchengerwa alisisitiza kuwa maandalizi yote muhimu yamekamilika ili kuhakikisha wanafunzi wote 974,332 wanapata nafasi ya kuanza masomo yao tarehe 13 Januari 2025. Aliongeza kuwa Serikali imeweka mikakati kabambe ya kuhakikisha utekelezaji wa mtaala mpya wa elimu kwa ngazi ya awali, msingi, na sekondari unafanikiwa.

“Juhudi za kuhakikisha mafanikio ya mtaala mpya zinaendelea. Tunahakikisha kuwa kila mwanafunzi anapata elimu bora inayozingatia viwango vya kitaifa na kimataifa,” alieleza Bw. Mchengerwa.

Jinsi ya Kupata Majina ya Waliochaguliwa Kidato cha Kwanza 2025

Majina ya Waliochaguliwa Kidato cha Kwanza 2025 yamewekwa kwenye tovuti rasmi za Serikali, na pia yatapatikana katika ofisi za elimu za wilaya na mikoa kote nchini. Wazazi na walezi wanashauriwa kuwasiliana na ofisi za elimu au kutumia njia za mtandao kama ifuatavyo:

Tembelea tovuti rasmi ya TAMISEMI (www.tamisemi.go.tz). au bofya viungo vilivyopo hapa chini kuangalia moja kwa moja

ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA
GEITA IRINGA KAGERA
KATAVI KIGOMA KILIMANJARO
LINDI MANYARA MARA
MBEYA MOROGORO MTWARA
MWANZA NJOMBE PWANI
RUKWA RUVUMA SHINYANGA
SIMIYU SINGIDA SONGWE
TABORA TANGA

Mapendekezo ya Mhariri;

  1. Shule Walizopangiwa Darasa la Saba 2025
  2. Majina ya Wanafunzi na Shule Walizopangiwa Kidato cha Kwanza 2025
  3. Matokeo ya Darasa la Nne 2024/2025 (NECTA Standard Four Results)
  4. Jinsi ya Kuangalia Matokeo ya Kidato Cha Pili 2024
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo