Hapa Tumekuletea Orodha ya Majina ya Waliochaguliwa Chuo Kikuu Cha UDOM Awamu ya Pili 2024/2025 (UDOM Second Selection 2024/2025) pamoja na Majina Ya Wanafunzi wa Diploma Waliochaguliwa UDOM Awamu ya Pili
Majina ya Waliochaguliwa Chuo Kikuu Cha UDOM Awamu ya Pili 2024/2025
Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kimekamilisha mchakato wa udahili wa wanafunzi katika awamu ya pili kwa mwaka wa masomo wa 2024/2025. Orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na programu mbalimbali za masomo zinazotolewa na chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) imetangazwa rasmi, na imeambatanishwa kwa ajili ya umma kuona majina ya waliofanikiwa.
Wanafunzi waliochaguliwa wanapaswa kuthibitisha udahili wao kupitia mfumo rasmi wa udahili wa UDOM (https://application.udom.ac.tz) kuanzia tarehe 5 Oktoba 2024. Barua za udahili zitapatikana pia kupitia akaunti zao za mtandao wa udahili. UDOM inapenda kuwapongeza wote waliochaguliwa na kuwakaribisha kwa moyo mkunjufu kwenye chuo hicho kikubwa na chenye heshima nchini Tanzania.
Jinsi ya Kuangalia Majina ya Waliochaguliwa UDOM 2024/2025
Majina ya waliochaguliwa UDOM yametangazwa rasmi, na kuna njia kadhaa za kuthibitisha kama mwanafunzi amechaguliwa:
1. Kupitia Ujumbe wa Simu
Wanafunzi waliofanikiwa watapokea ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) kwenye namba za simu walizotumia wakati wa kutuma maombi. Ujumbe huu utakuwa na taarifa kuhusu kozi ambayo mwanafunzi amechaguliwa.
2. Kupitia Mfumo wa Udahili wa UDOM (UDOM OAS)
Wanafunzi wanaweza kuingia kwenye mfumo wa udahili wa UDOM kupitia tovuti rasmi: https://application.udom.ac.tz.
Hatua za kufuata ni:
- Ingia kwenye akaunti yako kwa kutumia jina la mtumiaji na nenosiri ulilotumia wakati wa kuomba.
- Baada ya kuingia, utaona taarifa ya kama umechaguliwa na kozi uliyodahiliwa.
- Thibitisha udahili kwa kuingiza namba maalum ya siri (Special Code) ambayo utatumiwa kwa SMS.
Pia Wanafunzi waliotuma maombi wanaweza kuangalia Majina ya Waliochaguliwa Chuo Kikuu Cha UDOM Awamu ya Pili 2024/2025 katika dokumenti za pdf zilizopo hapa chini. Dokumenti hizi zinamajina ya waliochaguliwa kujiunga na kozi za shahada ya kwanza UDOM kwenye kozi moja na Majina ya waliochaguliwa kujiunga Diploma. Kama hautafanikiwa kuona jina lako katika pdf hizi tunashauri utumia njia ya kuangalia kama umechaguliwa kupitia mfumo wa UDOM OAS kama tulivyo eleza hapo juu.
Angalia Hapa
- Â Announcement For Applicants With Multiple Admissions For The 2024/2025 Academic Year- Second Round Of Admission
- Announcement For Students Admitted Into Different Study Programmes At The University Of Dodoma With Single Admission For The 2024/2025 Academic Year–Second Round Admission
- Announcement For Students Admitted Into Diploma Programmes At The University Of Dodoma In The Second Round Of Admission For The 2024/2025 Academic Year
Uthibitisho wa Udahili kwa Waliochaguliwa Zaidi ya Chuo Kimoja
Wanafunzi waliochaguliwa zaidi ya chuo kimoja wanapaswa kuthibitisha udahili wao kwa kuchagua chuo kimojawapo kuanzia tarehe 5 hadi 21 Oktoba 2024. Uthibitisho unapaswa kufanyika kwa kutumia namba maalum ya siri waliyopewa kupitia SMS au barua pepe walizotumia wakati wa kutuma maombi.
Ikiwa mwanafunzi hajapokea namba ya uthibitisho, anashauriwa kuingia kwenye mifumo ya vyuo husika na kuomba ujumbe mfupi wenye namba hiyo maalum. Kwa msaada zaidi, wanaweza kutembelea tovuti ya TCU (www.tcu.go.tz) ili kuona orodha ya waliodahiliwa zaidi ya chuo kimoja Au Angalia Hapa katika chapisho letu > Majina ya Waliochaguliwa Chuo Zaidi ya Kimoja 2024/2025
UDAHILI WA AWAMU YA TATU UDOM 2024/2025
Kwa wale ambao hawakudahiliwa kwenye awamu ya kwanza na ya pili, Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imeongeza muda wa udahili. Awamu ya tatu itafanyika kuanzia tarehe 5 hadi 9 Oktoba 2024, na inatoa nafasi kwa wale ambao hawakuweza kupata udahili kwenye awamu za awali kuomba tena.
Kuhusu Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM)
Chuo Kikuu cha Dodoma kilianzishwa mwaka 2007, kikiwa na lengo la kuwa chuo kikubwa zaidi nchini Tanzania. UDOM kimejengwa takribani kilomita 7 mashariki mwa jiji la Dodoma, kikimiliki eneo la ukubwa wa hekta 6,000. Mpango wa chuo ni kuwa na uwezo wa kudahili wanafunzi 40,000 mara miundombinu yake itakapokamilika.
UDOM ni fahari ya Tanzania kwani ujenzi wake umegharamiwa kikamilifu na fedha za ndani, lengo likiwa ni kutoa mchango mkubwa kwa maendeleo ya taifa na dunia kwa ujumla. Chuo hiki kipo katika kitovu cha nchi, jambo linalowezesha kuwa na mazingira bora ya masomo na kuunganisha wanafunzi kutoka pande zote za Tanzania.
Kwa sasa, UDOM ina vyuo vikuu sita (6), shule tatu (3), na taasisi mbili (2), zenye uwezo wa kudahili idadi tofauti ya wanafunzi kwa wakati mmoja. Vyuo hivi vina maeneo yao ya kipekee ndani ya kampasi kuu, huku kila chuo kikiwa na huduma zote muhimu kwa wanafunzi na walimu.
Leave a Reply