Magoli Mawili ya Haaland Yarejesha Man City Kileleni mwa Msimamo wa Ligi

EPL: Magoli Mawili ya Haaland Yarejesha Man City Kileleni mwa Msimamo wa Ligi Kuu Ya Uingereza

  • Klabu ya Manchester City sasa imerejea namba moja katika msimamo wa ligi kuu ya EPL. Katika mchezo uliokuwa na mvutano mkali, Manchester City ilipata ushindi muhimu wa magoli 2-0 dhidi ya Tottenham Hotspur, shukrani kwa mabao mawili yalio fungwa Erling Haaland. Ushindi huu unawaweka “Manchester city kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza, wakiwa na pointi mbili zaidi ya Arsenal kabla ya mchezo wa mwisho wa msimu.

Magoli Mawili ya Haaland Yarejesha Man City Kileleni mwa Msimamo wa Ligi

Magoli Mawili ya Haaland Yarejesha Man City Kileleni mwa Msimamo wa Ligi

Manchester City imeendelea kujieka katika nafasi nzuri katika mbio za kushindania ubingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza baada ya magoli mawili ya Erling Haaland kuisaidia kupata ushindi wa 2-0 dhidi ya Tottenham Hotspur, na hivyo kuwafanya kuwa kileleni mwa msimamo wa ligi wakiwa mbele kwa pointi mbili zaidi ya wapinzania wao wa kalibu Arsenal kabla ya siku ya mwisho ya msimu.

Naafasi Klabu Mechi Tofauti Ya Magoli Pointi
1 Man City 37 60 88
2 Arsenal 37 61 86

Katika mchezo uliokuwa na presha kubwa katika Uwanja wa Tottenham Hotspur, mchezo ambao Spurs walihitaji ushindi ili kuweka hai matumaini yao ya kumaliza katika nafasi nne za juu lakini bahati haikua ambande wao. City walipata bao la kuongoza kupitia mshambuliaji wake Haaland aliyefunga kwa urahisi kupitia krosi ya Kevin De Bruyne baada ya mapumziko.

Kipa wa akiba wa City, Stefan Ortega, aliokoa michomo muhimu kutoka kwa Dejan Kulusevski na Heung-Min Son baada ya kuchukua nafasi ya Ederson, aliyeumia kichwani na kulazimika kutoka nje, lakini Haaland alifunga bao la pili kwa mkwaju wa penalti baada ya Pedro Porro kumchezea rafu mchezaji aliyeingia akiba, Jeremy Doku.

Ushindi huu, wa nane mfululizo kwa City katika Ligi Kuu, unamaanisha kuwa kikosi cha Pep Guardiola kitakuwa bingwa kwa mara ya nne mfululizo, jambo ambalo halijawahi kutokea, ikiwa watashinda West Ham katika Uwanja wa Etihad Jumapili. Arsenal watahitaji kushinda mchezo wao wa nyumbani dhidi ya Everton huku wakitumai City watateleza.

Spurs, kwa upande mwingine, sasa wametoka kwenye mbio za kuwania nafasi ya Ligi ya Mabingwa, huku kocha wao mkuu Ange Postecoglou akielezea kutoridhishwa na “misingi dhaifu” katika klabu hiyo.

Mapendekezo Ya Mhariri:

  1. Mvua Yafichua Ubovu wa Old Trafford: Video ya Kuvuja Maji Yatisha Mashabiki
  2. Yanga SC Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania 2023/24: Ushindi wa Mara ya 30 Kihistoria
  3. Mbappe Akubali Punguzo Kubwa la Mshahara Ili Kujiunga na Real Madrid
  4. Hizi Apa Takwimu za Stephane Aziz Ki na Feisal Salum 2023/2024
  5. Simba Sc Yafunga Safari Kuifata kagera Sugar (May 2024)
  6. Hiki Ndicho Kikosi Rasmi cha Brazil Copa America 2024
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo