Ligi Kuu Zanzibar 2024/2025 Yaanza Kuchangamka

Ligi Kuu Zanzibar 2024 2025 Yaanza Kuchangamka

Ligi Kuu Zanzibar 2024/2025 Yaanza Kuchangamka

Msimu mpya wa Ligi Kuu Zanzibar 2024/2025 umeshaanza kwa kasi, na tayari vita ya ubingwa inazidi kuchemka. Timu mbalimbali zimeanza kujipambanua kwa kutoa ushindani mkali, huku timu nyingi zikionesha uwezo wa juu katika michezo yao. Hali hii imefanya ligi kuwa yenye msisimko mkubwa, huku mashabiki wakifuatilia kwa karibu matokeo ya kila mzunguko.

Vita ya Ubingwa Yazidi Kupamba Moto

Ligi Kuu Zanzibar msimu huu inajumuisha jumla ya timu 16, ambazo zinaendelea kupigania nafasi ya kutwaa ubingwa. Hadi kufikia mzunguko wa saba, hakuna timu yoyote iliyofanikiwa kupata ushindi wa asilimia 100.

Hata hivyo, timu nne zimefanikiwa kucheza bila kufungwa, nazo ni KVZ FC, Mlandege FC, Malindi SC, na Chipukizi FC. Ingawa hazijashinda mechi zote, bado zinaonekana kuwa na nafasi nzuri katika mbio za ubingwa.

Matokeo haya yanaonesha kwamba ushindani wa msimu huu ni mkali, na timu zote zinahitaji kujipanga vyema ili kufanikisha malengo yao ya mwisho. Timu zilizoonekana kuwa na mwenendo mzuri bado zinapata changamoto kutoka kwa wapinzani wao, huku baadhi ya mechi zikimalizika kwa sare.

Msimamo wa Ligi na Timu Zinazoongoza

Katika msimamo wa ligi, hadi sasa Mwembe Makumbi City inashikilia nafasi ya kwanza ikiwa na alama 15 baada ya michezo saba. Nafasi ya pili inashikiliwa na KMKM SC yenye pointi 14, wakifuatiwa na Mafunzo FC pamoja na Malindi SC, zote zikiwa na alama 13. Ushindani wa timu hizi za juu unaonesha dalili za mbio za ubingwa kuwa ngumu zaidi kadri msimu unavyoendelea.

Ligi Kuu Zanzibar 2024/2025 Yaanza Kuchangamka

Kwa upande wa timu za mkiani, Inter Zanzibar FC inaburuza mkia kwa alama moja tu katika michezo saba, ikifuatiwa na Tekeleza FC yenye alama moja pia baada ya michezo sita. Timu nyingine zilizopo katika hatari ya kushuka daraja ni New City FC yenye pointi mbili, na Mwenge SC yenye alama nne.

Mwisho wa msimu huu, timu nne za mwisho kwenye msimamo wa ligi zitashuka daraja na kurudi Ligi Daraja la Kwanza kwa Kanda walizotoka, Unguja na Pemba. Hii inafanya vita ya kutoshuka daraja kuwa kali kama ilivyo kwa mbio za ubingwa.

Ligi hii pia imekumbwa na changamoto kadhaa za kiufundi na usimamizi. Kulingana na Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Issa Kassim, kumekuwa na makosa kadhaa ya kiufundi yaliyojitokeza katika mizunguko ya awali, hasa kutoka kwa waamuzi na baadhi ya viongozi wa timu. Hata hivyo, Bodi ya Ligi imekuwa ikifanya tathmini baada ya kila mzunguko na kuchukua hatua stahiki kwa wahusika waliokiuka kanuni za ligi.

Kassim alisisitiza kuwa Bodi itaendelea kusimamia kwa ukaribu utekelezaji wa kanuni za ligi ili kuhakikisha kuwa ligi inachezwa kwa haki na uwazi. Hatua hizi zinatarajiwa kuleta uboreshaji katika uendeshaji wa ligi, huku lengo likiwa ni kupunguza au kuondosha kabisa vitendo vinavyokiuka kanuni.

Matarajio kwa Mzunguko Ujao

Kadri ligi inavyoendelea, mashabiki na wadau wa soka Zanzibar wanaendelea kufuatilia kwa karibu matokeo na mwenendo wa timu zao pendwa. Timu zinazoongoza kama Mwembe Makumbi City, KMKM SC, na Mafunzo FC zitahitajika kuimarisha zaidi safu zao ili kuendelea na ushindani wa kutwaa ubingwa. Kwa upande mwingine, timu zilizo mkiani kama Inter Zanzibar FC na Tekeleza FC, zina kibarua kigumu cha kujinasua kutoka kwenye eneo la kushuka daraja.

Mzunguko wa nane unatarajiwa kua wenye ushindani zaidi, huku kila timu ikijaribu kujiimarisha katika nafasi zao. Kwa kuzingatia ushindani wa timu mbalimbali, ni wazi kwamba msimu wa 2024/2025 wa Ligi Kuu Zanzibar unatoa dalili za kuwa msimu wa kipekee na wenye changamoto nyingi kwa timu zote zinazoshiriki.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Erik Ten Hag Hajaridhika na Ushindi Dhidi ya Brentford, Ajiandaa Kukabiliana na Mourinho
  2. Ngorongoro Heroes Yatwaa Kombe la CECAFA U-20 Baada ya Kuicharaza Kenya
  3. Yanga Yaendelea Kugawa Dozi Kwa Maasimu Wake wa Msimbazi
  4. Matokeo ya Simba Vs Yanga Leo 19/10/2024
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo