Ligi Kuu Bara Kurejea Februari kwa Moto! Simba na Yanga Kuanza na Viporo

Ligi Kuu Bara Kurejea Februari kwa Moto Simba na Yanga Kuanza na Viporo

Ligi Kuu Bara Kurejea Februari kwa Moto! Simba na Yanga Kuanza na Viporo

BODI ya Ligi Nchini (TPLB) imetangaza kuwa Ligi Kuu Tanzania Bara itarejea kwa moto mwezi Februari, ikianza na mechi za viporo za vigogo Simba na Yanga. Mechi hizo zitatangulia kabla ya kuendelea na raundi ya 17 ya ligi hiyo maarufu.

Kwa mujibu wa Ofisa Mtendaji Mkuu wa TPLB, Almasi Kasongo, ligi hiyo itaanza tena mapema Februari baada ya ratiba ya michuano ya CHAN kusogezwa mbele. Kasongo alisema, “Tumesimamisha ligi kwa ajili ya Kombe la Mapinduzi na CHAN. Kombe la Mapinduzi limekamilika na CHAN imepelekwa mbele, hivyo ni lazima ligi ianze mapema mwezi wa pili.”

Ligi Kuu Bara Kurejea Februari kwa Moto! Simba na Yanga Kuanza na Viporo

Mechi za Viporo za Simba na Yanga

Ratiba inaonyesha kuwa Simba SC itakutana na Tabora United katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora. Wakati huo huo, Yanga SC itakuwa mwenyeji wa Kagera Sugar kwenye Uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam. Timu hizi mbili kubwa nchini, ambazo pia zimeshiriki michuano ya kimataifa msimu huu, zimecheza michezo 15 pekee hadi sasa, tofauti na timu nyingine ambazo zimecheza mechi 16.

Kasongo alifafanua kuwa viporo hivi vya ligi ni muhimu kwa kuhakikisha usawa wa idadi ya mechi kabla ya kuendelea na raundi ya 17. “Tuna viporo kwa klabu mbili zilizoshiriki Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho, Simba na Yanga. Ni lazima michezo yao ikamilishwe kwanza,” alisisitiza.

Mechi za Kombe la FA Kuanza Kwanza

Hata hivyo, kabla ya viporo vya ligi, klabu hizo mbili zitalazimika kumaliza mechi zao za viporo kwenye michuano ya Kombe la FA. Kasongo alieleza kuwa muda wa maandalizi bado upo, na timu zimepewa nafasi ya kukusanyika na kuanza mazoezi kabla ya kuingia uwanjani kwa mechi hizo muhimu.

“Timu zitakuwa zimeshakusanyana kuanza mazoezi, na viporo vya FA vitakamilika kabla ya ligi kuendelea,” alisema Kasongo.

Hali ya Msimamo wa Ligi

Kwa sasa, Simba SC inaongoza ligi ikiwa na pointi 40, ikiwapita wapinzani wao wa karibu kwa tofauti kubwa. Wakati huo huo, KenGold ya jijini Mbeya inashikilia mkia ikiwa na pointi sita pekee.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Mtibwa Sugar Kuwakaribisha Azam FC Manungu kwa Mechi ya Kirafiki
  2. Ligi Kuu Bara: JKT Tanzania Waitana Kambini, Kocha Apania Maboresho
  3. Watano Waagwa Azam Fc
  4. CV ya Jonathan Djogo Kapela: Winga Mpya wa Yanga SC
  5. Taifa Stars Yapangwa Kundi Laini CHAN 2024
  6. Makundi ya CHAN 2025 Yatangazwa
  7. Vituo Vya Kununua Tiketi Mechi ya Yanga vs MC Alger 18/01/2024
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo