Ligi 20 Bora Afrika 2025 | Ligi Zenye Ubora Barani Afrika 2024/2025
Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) limetangaza orodha mpya ya viwango vya ligi bora barani Afrika kwa mwaka 2025. Kwa mujibu wa viwango hivyo, ligi za kanda ya Kaskazini mwa Afrika zinaendelea kuongoza, huku mataifa mengine yakifuatia kwa karibu.
Katika orodha mpya iliyotolewa, Ligi Kuu ya Misri imepewa heshima ya kuwa namba moja, ikifuatwa na Ligi Kuu ya Morocco katika nafasi ya pili, huku Ligi ya Algeria ikishikilia nafasi ya tatu. Haya yanathibitisha ubora wa ligi za Afrika Kaskazini katika michuano ya ndani.
Katika orodha hiyo mpya, Ligi kuu ya Tanzania bara imeshika nafasi ya sita, ikiwa ni nchi pekee kutoka Afrika Mashariki kwenye orodha ya kumi bora. Angola inashikilia nafasi ya saba, ikifuatiwa na Ligi ya DR Congo katika nafasi ya nane. Ligi za Sudan na Ivory Coast zinakamilisha kumi bora, zikiwa katika nafasi za tisa na kumi mtawalia.
Orodha ya Ligi 20 Bora Afrika 2025
- Egypt
- Morocco
- Algeria
- South Africa
- Tunisia
- Tanzania
- Angola
- DR Congo
- Sudan
- Ivory Coast
- Libya
- Mali
- Nigeria
- Ghana
- Guinea
- Botswana
- Senegal
- Mauritania
- Congo
- Cameroon
Mapendekezo ya Mhariri:
- Yanga Wamejipanga Kupambana Kesho: Ramovic
- Kocha MC Alger Atamba Kupata Pointi 3 Dhidi ya Yanga Licha ya Joto Kali
- Ligi Kuu Bara Kurejea Februari kwa Moto! Simba na Yanga Kuanza na Viporo
- Mtibwa Sugar Kuwakaribisha Azam FC Manungu kwa Mechi ya Kirafiki
- Ligi Kuu Bara: JKT Tanzania Waitana Kambini, Kocha Apania Maboresho
- Watano Waagwa Azam Fc
- CV ya Jonathan Djogo Kapela: Winga Mpya wa Yanga SC
- Taifa Stars Yapangwa Kundi Laini CHAN 2024
Leave a Reply