Kocha wa Simba Fadlu David Aelezea Kuhusu Sare Dhidi ya Coastal Union

Kocha wa Simba Fadlu David Aelezea Kuhusu Sare Dhidi ya Coastal Union

Kocha wa Simba Fadlu David Aelezea Kuhusu Sare Dhidi ya Coastal Union

Dar es Salaam, Tanzania – Kocha Mkuu wa Simba SC, Fadlu Davids, ameelezea kutoridhishwa kwake na matokeo ya sare ya 2-2 dhidi ya Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa Uwanja wa KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam.

Simba walionekana kuwa mbioni kupata ushindi rahisi baada ya kupata mabao mawili ya mapema kupitia kwa Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ na Leonel Ateba katika kipindi cha kwanza. Hata hivyo, Coastal Union walionyesha ujasiri na kupambana vikali kipindi cha pili, wakisawazisha mabao yote mawili kupitia kwa Hassan Abdallah na Ernest Malonga.

Kocha wa Simba Fadlu David Aelezea Kuhusu Sare Dhidi ya Coastal Union

Fadlu alikiri kuwa wachezaji wake walionekana kuridhika na matokeo baada ya kupata mabao mawili ya kuongoza, na kushindwa kuongeza juhudi katika kipindi cha pili.

“Mechi ilitakiwa kumalizika kipindi cha kwanza kwa kufunga goli la tatu,” alisema Fadlu. “Lakini kwa kilichotokea nina kazi ya kubadili mitazamo ya wachezaji. Tutarudi uwanja wa mazoezi kujiandaa kuelekea mchezo ujao dhidi ya Yanga.”

Kocha huyo wa Simba aliongeza kuwa anakabiliwa na changamoto kubwa kuelekea mchezo huo wa Oktoba 19 dhidi ya watani wao wa jadi Yanga SC, kwani wachezaji wengi watajiunga na vikosi vya timu za taifa.

“Hakuna la kufanya, tutaendelea na mazoezi na hawa waliopo kuelekea kwenye mchezo huo muhimu,” alisema Fadlu.

Kwa upande wake, Kaimu Kocha Mkuu wa Coastal Union, Joseph Lazaro, alisema Simba waliingia kwenye mtego wao wa kucheza kwa kujihami kipindi cha pili, na ndiyo maana walifanikiwa kusawazisha mabao.

“Kikubwa ni kwamba tuliwaheshimu hasa kipindi cha kwanza,” alisema Lazaro. “Sasa wakaingia kwenye mtego kudhani tutakuja hivyo hivyo kipindi cha pili. Matokeo yake tulibadilika na kushambulia, mabao yote ni ya kushtukiza.”

Sare hiyo inaifanya Simba kupanda hadi nafasi ya pili katika msimamo wa ligi, wakiwa na pointi 13 sawa na Fountain Gate, huku Coastal Union wakibaki nafasi ya 13 wakiwa na pointi tano.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Huu Apa Utaratibu wa Droo ya Makundi CAF, Klabu Bingwa na Kombe la Shirikisho 2024/25
  2. Orodha ya Mabingwa Ligi kuu Tanzania Bara
  3. JKT Queens Waichapa Yanga Fainali ya Ngao ya Jamii Wanawake 2024
  4. Kikosi Cha Coastal Union FC 2024/2025
  5. Gamondi Ataja Siri ya Ushindi wa 4-0 Dhidi ya Pamba Jiji
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo