KMC Vs Yanga Leo 14 Februari 2025 Saa Ngapi?

Taarifa Muhimu za Mechi ya KMC Vs Yanga Leo 14 Februari 2025

KMC Vs Yanga Leo 14 Februari 2025 Saa Ngapi?

KMC FC leo itawakaribisha mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya NBC, Yanga SC, katika dimba la KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam. Huu ni mchezo wa kukata na shoka, ukitarajiwa kuanza saa 10:15 jioni. Mashabiki wa soka wanatarajia kuona mechi yenye ushindani mkubwa kati ya timu hizi mbili, huku kila moja ikisaka pointi tatu muhimu.

Taarifa Muhimu za Mechi ya KMC Vs Yanga Leo 14 Februari 2025

  • Muda wa Mchezo: Saa 10:15 Jioni
  • Uwanja: KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam
  • Mashindano: Ligi Kuu ya NBC Tanzania
  • Historia ya Mikutano: Yanga imeshinda mara 10 kati ya mechi 13 zilizopita
  • Kocha wa Yanga: Miloud Hamdi
  • Kocha wa KMC: Kally Ongala
  • Rekodi ya Mabao: Yanga imefunga mabao 21 dhidi ya KMC, huku KMC ikifunga mabao 5 pekee

KMC Vs Yanga Leo 14 Februari 2025 Saa Ngapi?

Historia na Rekodi ya KMC Dhidi ya Yanga

KMC na Yanga zimekutana mara 13 kwenye Ligi Kuu tangu KMC ilipoanza kushiriki ligi hiyo mwaka 2018. Katika michezo hiyo, Yanga imeibuka kidedea mara 10, huku KMC ikishinda mara moja pekee, na mechi mbili zikiisha kwa sare. Yanga imefunga mabao 21 dhidi ya KMC, huku ikiruhusu mabao matano pekee.

Kwa upande wa KMC, historia haiko upande wao, lakini watajitahidi kubadilisha mwenendo huo kwa kuendeleza uimara wao waliouonyesha katika mechi ya hivi karibuni dhidi ya Singida Black Stars. KMC ilifanikiwa kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo, jambo linaloweza kuwapa morali kuelekea mchezo huu mgumu dhidi ya Yanga.

Msimamo wa Timu na Maandalizi ya Mechi

Yanga inakuja kwenye mchezo huu ikiwa na azma ya kurejea katika rekodi za ushindi baada ya kuambulia sare dhidi ya JKT Tanzania katika mechi yao iliyopita. Kikosi hicho kinachoongozwa na kocha mpya, Miloud Hamdi, kinajivunia safu kali ya ushambuliaji ambayo imeshafunga mabao 42 katika mechi 18 za ligi msimu huu.

Kwa upande wa KMC, timu hiyo inaendelea kujijenga chini ya kocha Kally Ongala. Tangu aanze kuiongoza timu hiyo, ameshinda mechi mbili, kutoka sare mbili na kupoteza tatu kati ya mechi saba alizoiongoza.

Ingawa rekodi yao si ya kuvutia, KMC imeonyesha maendeleo kwa kupunguza idadi ya mabao inayofungwa na Yanga. Katika mzunguko wa kwanza wa msimu huu, walipoteza kwa bao 1-0 pekee, ikilinganishwa na vipigo vikubwa vya 5-0 na 3-0 walivyopata msimu uliopita.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Kikosi cha Simba VS Tanzania Prisons Leo 11/02/2024
  2. Simba VS Tanzania Prisons Leo 11/02/2024 Saa Ngapi?
  3. YANGA warejea nyumbani na pointi moja baada ya sare na JKT Tanzania
  4. Matokeo ya JKT Tanzania Vs Yanga Leo 10/02/2025
  5. Kikosi cha Yanga vs JKT Tanzania Leo 10/02/2025
  6. Ratiba ya Mechi za Leo 10 Februari 2025
  7. Viingilio Mechi ya JKT Tanzania Vs Yanga Leo 10/02/2025
  8. JKT Tanzania Vs Yanga Leo 10/02/2025 Saa Ngapi?
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo