Kilimanjaro Stars Kukamilisha Ratiba Mapinduzi Cup Dhidi ya Burkina Faso

Kilimanjaro Stars Kukamilisha Ratiba Mapinduzi Cup Dhidi ya Burkina Faso

Kilimanjaro Stars Kukamilisha Ratiba Mapinduzi Cup Dhidi ya Burkina Faso

Katika mfululizo wa michuano ya Kombe la Mapinduzi, timu ya soka ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars, inatarajiwa kushuka dimbani leo kukamilisha ratiba dhidi ya Burkina Faso. Mtanange huo unatarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Gombani, ulioko Kisiwani Pemba.

Ingawa Kilimanjaro Stars tayari imeshaaga mashindano hayo baada ya kupoteza mechi mbili mfululizo, mchezo huu unakuwa wa kukamilisha ratiba na kujaribu kumaliza mashindano kwa heshima.

Safari ya Kilimanjaro Stars katika Kombe la Mapinduzi mwaka huu imekuwa ya kusikitisha. Baada ya kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya wenyeji, Zanzibar Heroes, kwa bao 1-0, matumaini ya timu hiyo yalizimwa kabisa kufuatia kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Kenya. Matokeo haya yameifanya Kilimanjaro Stars kuondolewa rasmi kwenye mashindano, huku ikiwa haina alama yoyote na haijafunga bao lolote hadi sasa.

Licha ya kuondolewa, Kilimanjaro Stars itashuka dimbani kuwakabili Burkina Faso katika mchezo wa kukamilisha ratiba. Mchezo huu unatoa fursa kwa kocha mkuu, Hamad Ally, kujaribu mbinu mpya na kuwapa wachezaji nafasi ya kuonyesha uwezo wao.

Pia, ni nafasi ya kujitahidi kumaliza mashindano kwa heshima na kuondoka na somo muhimu kwa maandalizi ya michuano mingine. Mchezo unatarajiwa kupigwa majira ya saa 1:00 usiku.

Kilimanjaro Stars Kukamilisha Ratiba Mapinduzi Cup Dhidi ya Burkina Faso

Hali ya Mashindano

Kufikia sasa, Kenya na Burkina Faso zinaongoza msimamo wa mashindano zikiwa na pointi nne kila moja, zikifuatiwa na Zanzibar Heroes yenye pointi tatu. Mechi nyingine iliyopangwa kuchezwa leo ni kati ya Zanzibar Heroes dhidi ya Burkina Faso.

Matokeo ya mechi hizi yataamua timu zitakazocheza fainali, ambayo imepangwa kufanyika Januari 13. Fainali itahusisha timu itakayomaliza katika nafasi ya kwanza dhidi ya timu itakayokuwa katika nafasi ya pili kwenye msimamo.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Shassir Nahimana (31) Atambulishwa Rasmi na Pamba Jiji
  2. Msimamo Wa Kundi Mapinduzi Cup 2025
  3. Kikosi cha Kilimanjaro Stars vs Kenya Leo 07/01/2025
  4. Msimamo wa Kundi la Yanga Klabu Bingwa Afrika CAF 2024/2025
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo