Kilichomuondoa Ramovic Yanga Hatimaye Chafichuka
Katika hali isiyotarajiwa, kocha mkuu wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya NBC, Young Africans (Yanga), Sead Ramovic, ametangaza kuachia ngazi. Taarifa hii ya kushtua imejiri wakati Yanga ikiwa katika harakati za kujiandaa na mchezo wao wa ligi dhidi ya Ken Gold, unaotarajiwa kuchezwa leo Februari 5, 2025, katika dimba la KMC Complex, jijini Dar es Salaam.
Kuondoka kwa Ramovic kumekuja kama “bomu” kwa mashabiki na wadau wa soka nchini, hasa ikizingatiwa kuwa kocha huyo alijiunga na Yanga hivi karibuni, Novemba 15, 2024, akichukua nafasi ya Miguel Gamondi.
Haya ni mabadiliko makubwa kwa Yanga, ambao walikuwa wakitarajia kocha huyo angeendelea kuinoa timu hiyo katika michuano ya ndani ambayo ni ligi kuu ya NBC na kombe la shirikisho la CRDB, hasa baada ya kutolewa katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Mchezo wa leo dhidi ya Ken Gold utakuwa wa mwisho kwa Ramovic akiwa kocha wa Yanga, na hivyo kuhitimisha safari yake fupi ya siku 81 tu ndani ya klabu hiyo. Kuondoka kwake kumeacha maswali mengi kwa mashabiki na wadau wa soka, huku wengi wakijiuliza nini hasa kimemtoa Ramovic Yanga? Endelea kusoma ili kupata undani wa taarifa hii.
Ramovic Aondoka Yanga Baada ya Dili Nono
Chanzo cha kuondoka kwa Ramovic kimethibitishwa kuwa ni ofa nono aliyopata kutoka klabu ya CR Belouizdad ya Algeria. Timu hiyo inatafuta kocha mpya baada ya kuachana na Abdelkader Amrani mnamo Januari 25, 2025. Kwa sasa, timu hiyo inaongozwa na kaimu kocha mkuu, Samir Houhou, lakini Ramovic anatarajiwa kuchukua rasmi mikoba hiyo baada ya kumaliza majukumu yake Yanga.
Ramovic, ambaye alijiunga na Yanga mnamo Novemba 15, 2024, alikaa na timu hiyo kwa siku 81 pekee, akichukua nafasi ya Muargentina Miguel Gamondi. Ndani ya muda wake mfupi, ameiongoza Yanga katika michezo 13 kwenye mashindano mbalimbali na kutoa matokeo bora, hasa katika Ligi Kuu Tanzania Bara ambapo alishinda mechi zote sita alizoiongoza.
Mshtuko kwa Wachezaji na Mashabiki
Habari za kuondoka kwa Ramovic zilisababisha mshtuko mkubwa kwa wachezaji na mashabiki wa Yanga. Katika mazoezi ya mwisho kabla ya mchezo dhidi ya KenGold, kocha huyo aliwaaga rasmi wachezaji wake, hali iliyowaacha wengi wakiwa na mshangao mkubwa.
Mmoja wa wachezaji wa Yanga alinukuliwa akisema: “Tulidhani kuna tatizo kati yake na uongozi, lakini ametueleza wazi kuwa amepata nafasi nyingine na anatuaga.” Licha ya kuondoka kwake ghafla, Ramovic aliwasisitiza wachezaji kuhakikisha wanashinda mchezo wa leo na pia kupigania kutetea ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC.
Rekodi ya Ramovic Ndani ya Yanga
Katika kipindi chake cha kuinoa Yanga, Ramovic aliiongoza timu katika mechi 13 na kufanikisha ushindi katika michezo 9, sare 2 na kupoteza michezo 2 pekee. Alifanikiwa kuiongoza Yanga kuwa kinara wa ligi kwa saa zisizozidi 24 baada ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Kagera Sugar, kabla ya Simba kuipindua kwa kuichapa Tabora United 3-0.
Matokeo ya mechi alizoongoza ni kama ifuatavyo:
Ligi Kuu Tanzania Bara
- Mechi: 6
- Ushindi: 6
- Sare: 0
- Kupoteza: 0
- Mabao ya kufunga: 22
- Mabao ya kufungwa: 2
Kombe la FA
- Mechi: 1
- Ushindi: 1
- Sare: 0
- Kupoteza: 0
- Mabao ya kufunga: 5
- Mabao ya kufungwa: 0
Ligi ya Mabingwa Afrika
- Mechi: 6
- Ushindi: 2
- Sare: 2
- Kupoteza: 2
- Mabao ya kufunga: 5
- Mabao ya kufungwa: 6
Mapendekezo ya Mhariri:
- CAF Yatangaza Tarehe ya Droo Robo Fainali ya Klabu Bingwa na Shirikisho
- Matokeo ya Yanga vs Kengold Leo 05/02/2025
- CV ya Miloud Hamdi, Kocha Mpya wa Yanga 2025
- Vinara wa Assist NBC Premier League 2024/2025
- Timu zilizofuzu 32 bora CRDB Bank Federation Cup 2024/2025
- Ratiba ya Mechi za Yanga February 2025
- Aliekua Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi Atua Al Nasr ya Libya
- Kagera Sugar Yatamba Kuondoa Unyonge KMC Complex Dhidi ya Yanga
- Morocco Aweka Mikakati ya Ushindi dhidi ya Vigogo Ndani ya Kundi C AFCON 2025
- Simba SC Yajiandaa Vikali Kuisambaratisha Tabora United
- Makundi ya Fainali za Mataifa ya Afrika AFCON 2025
Leave a Reply