Hiki Ndicho Kikosi Rasmi cha Brazil Copa America 2024

Hiki Ndicho Kikosi Rasmi cha Brazil Copa America 2024: Casemiro, Thiago Silva, Gabriel Jesus na Richarlison kutotajwa kwenye kikosi cha muda cha Dorival Junior cha Brazil kwa ajili ya mashindano ya Copa America 2024.

Baada ya kipigo cha kushtua kutoka kwa Croatia katika robo fainali ya Kombe la Dunia 2022, Brazil imejikuta kwenye njia panda. Maswali kuhusu uwezo wao wa kushinda Copa America 2024 yameibuka, hasa baada ya mfululizo wa matokeo yasiyoridhisha katika mechi za kufuzu Kombe la Dunia 2026. Licha ya changamoto hizi, Seleção bado inajivunia kikosi chenye vipaji vingi, hasa katika safu ya ushambuliaji. Uteuzi wa kocha mpya Dorival Junior, akichukua nafasi ya Carlo Ancelotti, unaashiria mwanzo mpya na matumaini mapya.

Kikosi Rasmi cha Brazil Copa America 2024

Kikosi cha Brazil kilichatangazwa kwa ajili ya michuano ya Copa America 2024 kimeibua mjadala mkali. Wachezaji wazoefu kama Richarlison na Casemiro wameachwa nje, huku kinda Endrick mwenye umri wa miaka 17 akipewa nafasi ya kuonyesha kipaji chake kwenye jukwaa la kimataifa.

Thiago Silva, Gabriel Jesus na Richarlison kutotajwa kwenye kikosi cha muda cha Dorival Junior cha Brazil

Fainali hizi zitakuwa fursa ya dhahabu kwa Brazil kurejesha heshima yao kama wafalme wa soka Amerika Kusini. Mwaka 2023 ulikuwa mgumu kwa Seleção, hasa baada ya kupoteza mechi tatu mfululizo za kufuzu Kombe la Dunia, ikiwemo kipigo cha nyumbani dhidi ya mahasimu wao Argentina.

Hata hivyo, ushindi dhidi ya Uingereza kwenye Uwanja wa Wembley na sare ya kusisimua dhidi ya Uhispania katika mechi za kirafiki za Machi ziliashiria mwanga wa matumaini chini ya uongozi wa Dorival Jr.

Ingawa Brazil haijafikia ubora wake wa miaka ya nyuma, na kukosekana kwa Neymar kutokana na jeraha ni pigo kubwa, bado wanasalia kuwa miongoni mwa timu zinazopewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa Copa America 2024.

Je, wataweza kutimiza matarajio haya? Muda utasema.

Hiki Ndicho Kikosi Rasmi cha Brazil Copa America 2024

Nafasi Jina La Mchezaji Klabu Anayochezea Umri
GK Bento Athletico-PR 24
GK Ederson Manchester City (ENG) 30
GK Alisson Liverpool (ENG) 31
DEF Danilo Juventus (ITA) 32
DEF Yan Couto Girona (ESP) 21
DEF Guilherme Arana Atletico-MG 27
DEF Wendell Porto (POR) 30
DEF Beraldo PSG (FRA) 20
DEF Eder Militao Real Madrid (ESP) 26
DEF Gabriel Magalhaes Arsenal (ENG) 26
DEF Marquinhos PSG (FRA) 29
MID Andreas Pereira Fulham (ENG) 28
MID Joao Gomes Wolverhampton (ENG) 23
MID Bruno Guimaraes Newcastle (ENG) 26
MID Douglas Luiz Aston Villa (ENG) 26
MID Lucas Paqueta West Ham (ENG) 26
FOR Endrick Palmeiras 17
FOR Evanilson Porto (POR) 24
FOR Rodrygo Real Madrid (ESP) 23
FOR Gabriel Martinelli Arsenal (ENG) 22
FOR Raphinha Barcelona (ESP) 27
FOR Savinho Girona (ESP) 20
FOR Vinicius Junior Real Madrid (ESP) 23

Hiki Ndicho Kikosi Rasmi cha Brazil Copa America 2024

Mapendekezo Ya Mhariri:

  1. Msimamo Wa Ligikuu Ya NBC Tanzania 2023/2024
  2. Orodha Ya Mabingwa Wa UEFA Champions League
  3. Timu Yenye Makombe Mengi ya UEFA Champions League
  4. Timu Yenye Makombe Mengi ya Ligi Kuu England (2024)
  5. Orodha Ya Washindi Wa Ligi Kuu Ya Uingereza Miaka Yote
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo