Kikosi cha Yanga vs Tp Mazembe Leo 04/01/2024

Yanga vs Tp mazembe Leo Saa Ngapi

Kikosi cha Yanga vs Tp Mazembe Leo 04/01/2024 | Kikosi cha Yanga leo Dhidi ya TP Mazembe Klabu Bingwa

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania, Yanga SC, leo wanarejea dimbani katika kibarua kingine cha kimataifa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Katika mchezo wa marudiano, Yanga SC watawakalibisha TP Mazembe kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DR Congo) kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, saa 10:00 jioni.

Mchezo huu unatarajiwa kuwa wa kihistoria, ukizingatia matokeo ya sare ya 1-1 kwenye mchezo wa awali, ambapo Yanga walifanikiwa kusawazisha dakika za mwisho mjini Lubumbashi.

Kwa Yanga, mchezo huu si tu wa kawaida bali ni daraja lao la kuvuka kuelekea hatua ya robo fainali ya michuano ya kimataifa. Hadi sasa, Yanga wameshika nafasi ya mwisho katika msimamo wa Kundi A wakiwa na pointi moja pekee baada ya michezo mitatu.

Kinara wa kundi hilo ni Al Hilal ya Sudan yenye alama tisa. Hali hii inawapa Wanayanga jukumu kubwa la kuhakikisha wanapata ushindi wa pointi tatu ili kujiweka kwenye nafasi bora.

Akizungumza kuhusu maandalizi ya mchezo huu, Ofisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe, alieleza kuwa wachezaji wamejiandaa kwa kiwango cha juu na wamekubaliana kucheza kama mchezo wa leo ndio wa mwisho kwao msimu huu.

Aliwasihi mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuujaza Uwanja wa Benjamin Mkapa na kutoa hamasa kwa timu yao, akielezea umuhimu wa kufanya uwanja huo kuwa ‘tanuri la moto’ kwa wapinzani.

“Tuna jukumu kubwa leo. Ukweli mchungu ni kwamba hatujafanya vizuri kwenye hatua hii ya makundi, lakini bado tuna nafasi ya kubadilisha hali hii kwa kushinda mchezo huu,” alisema Kamwe. Aliongeza kuwa kushika nafasi ya mwisho si kitu kinachostahili klabu kubwa kama Yanga, ambayo msimu uliopita ilifika hatua ya robo fainali.

Kikosi cha Yanga vs Tp Mazembe Leo 04/01/2024

Kikosi cha Yanga vs Tp Mazembe Leo 04/01/2024

Kikosi rasmi cha Yanga Sc kitakacho anza leo dhidi ya TP Mazembe kinatarajiwa kutangazwa majira ya saa tisa jioni. Hapa tutakuletea orodha kamili ya wachezaji wote watakaounda kikosi hicho mara tu kitakapotangazwa na kocha mkuu wa Yanga Sead Ramovic.

kikosi cha Yanga leo

Hali ya Kikosi cha Yanga

Kocha Mkuu wa Yanga, Sead Ramovic, ameendelea kuandaa kikosi kwa umakini mkubwa huku akiwajumuisha wachezaji waliokuwa majeruhi. Habari njema ni kwamba golikipa Djigui Diarra, Maxi Nzengeli, na Clatous Chama tayari wameanza mazoezi na timu. Hata hivyo, Yao Kouassi bado hajapona kabisa na hatakuwa sehemu ya kikosi cha leo.

Yanga pia wanajivunia kurejea kwa wachezaji muhimu waliokuwa majeruhi, hali inayoongeza matumaini ya ushindi kwa mashabiki wao. Kwa upande wa wapinzani, kikosi cha TP Mazembe kiliwasili nchini jana jioni tayari kwa mchezo huu muhimu.

Rekodi za Hivi Karibuni

Katika hatua hii ya makundi, Yanga walianza kwa kupoteza michezo miwili ya awali kwa mabao 2-0 dhidi ya Al Hilal na MC Alger ya Algeria. Sare ya 1-1 dhidi ya TP Mazembe iliyoipata mjini Lubumbashi imebaki kuwa alama yao pekee hadi sasa. Mchezo wa leo unatarajiwa kuwa fursa yao ya kuonesha dhamira ya kusonga mbele.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Yanga Kuwakosa Maxi, Chama na Yao Mechi Dhidi ya TP Mazembe Leo
  2. Yanga vs Tp Mazembe Leo 04/01/2024 Saa Ngapi?
  3. Kikosi cha Kilimanjaro Stars VS Zanzibar Heroes leo 03/01/2024
  4. Viingilio Mechi ya Yanga VS TP Mazembe 04/01/2025
  5. Matokeo ya Zanzibar Heroes VS Kilimanjaro Stars leo 03/01/2024
  6. Ratiba ya Kombe la Mapinduzi 2025
  7. Kikosi Cha Kilimanjaro Stars Kitakacho Shiriki Mapinduzi Cup 2025
  8. Penati ya Dakika za Majeruhi Yaipa Simba Pointi Tatu Dhidi ya JKT
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo