Kikosi cha Yanga vs Tanzania Prison leo 22/12/2024 | Kikosi cha Yanga leo dhidi ya Tz Prison
Leo tarehe 22 Desemba 2024, klabu ya Yanga SC itawakaribisha Tanzania Prisons katika dimba la KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam. Mechi hii ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2024/2025 ni muhimu kwa Yanga, kwani inatoa fursa kwa mabingwa watetezi hao kuendelea kujijenga katika nafasi bora ya kutetea taji lao kwa mara ya nne. Mchezo huu unatarajiwa kuanza majira ya saa 10:00 jioni na unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa, ukizingatia umuhimu wa pointi kwa timu zote mbili.
Yanga SC ambayo sasa inashikilia nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ikiwa na jumla ya pointi 30, ina viporo viwili vya michezo dhidi ya Dodoma Jiji na Fountain Gate. Ushindi wa leo utaipa nafasi nzuri ya kufikia pointi 33, sawa na Azam FC, lakini kwa tofauti ya mabao wanaweza kupanda hadi nafasi ya pili.
Kwa upande wa Tanzania Prisons, hali si shwari. Wako katika nafasi ya pili kutoka chini wakiwa na pointi 11 tu baada ya kushinda mechi mbili, sare tano, na kupoteza saba. Ushindi wa leo ni muhimu sana kwao ili kujiondoa kwenye nafasi ya hatari ya kushuka daraja.
Yanga inajivunia kurejea kwenye kiwango bora baada ya ushindi wao wa 3-2 dhidi ya Mashujaa FC katika mchezo uliopita. Katika mechi hiyo, Prince Dube aling’ara kwa kupiga hat-trick, na kuweka rekodi kama mchezaji wa kwanza kufanikisha hilo msimu huu.
Hata hivyo, bado kuna changamoto za majeruhi katika kikosi. Kipa wa kwanza Djigui Diarra na wachezaji muhimu kama Maxi Nzengeli na Clatous Chama hawatacheza leo kutokana na majeraha. Kibwana Shomari, aliyecheza mechi yake ya kwanza msimu huu dhidi ya Mashujaa, alionyesha kiwango kizuri na anatarajiwa kuendelea na ubora wake leo.
Kikosi cha Yanga vs Tanzania Prison leo 22/12/2024
Kikosi cha Yanga kilichoanza dhidi ya Tanzania Prisons:
- 16: Msheri
- 15: Kibwana
- 30: Kibabage
- 5: Job
- 4: Bacca
- 8: Aucho
- 12: Faridi
- 27: Mudathir
- 10: Dube
- 9: Aziz Ki
- 24: Mzize
Wachezaji wa Akiba: Khomieny, Yao, Mwanyeto, Boka, Nkane, SureBoy, Kipande, Sheikhan, Abuya & Pacome Zouzoua
Hali ya Kikosi cha Tanzania Prisons
Kwa Tanzania Prisons, hali ni tofauti. Timu inakabiliwa na changamoto za majeruhi, huku pia benchi la ufundi likiwa limefanyiwa mabadiliko makubwa. Kaimu Kocha Mkuu, Shaban Mtupa, aliyeteuliwa hivi karibuni, ana jukumu kubwa la kurejesha ari na kujiamini kwa wachezaji wake. Licha ya rekodi mbaya dhidi ya Yanga, Mtupa anaamini kuwa lolote linaweza kutokea katika mchezo wa leo.
Kauli za Makocha
Kocha wa Yanga, Sead Ramovic, alisema: “Tunaenda kucheza mechi ngumu dhidi ya timu inayojilinda vizuri. Tutahakikisha tunapata ushindi kwani tunahitaji pointi tatu muhimu. Hatujali rekodi za nyuma, kila mechi ni mpya na tunawaheshimu wapinzani wetu.”
Kwa upande wake, Kaimu Kocha wa Prisons, Shaban Mtupa, alisema: “Tumejipanga kuhakikisha tunatoa ushindani mkubwa. Tumefanyia kazi maeneo yenye upungufu na tunajua Yanga ni timu bora, lakini tuna matumaini ya kufanya vizuri.”
Mapendekezo ya Mhariri:
Leave a Reply