Kikosi cha Yanga VS Tabora united Leo 02/04/2025 | Kikosi cha Yanga leo dhidi ya Tabora United
Tabora United leo itawakaribisha mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya NBC katika dimba la Ali Hassan Mwinyi, Tabora, katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2024/2025. Hii ni mechi inayosubiriwa kwa hamu kubwa kutokana na matokeo ya duru la kwanza ambapo Tabora United iliishangaza Yanga kwa ushindi wa mabao 3-1, matokeo ambayo yalipelekea kuondoka kwa aliyekuwa kocha wa Yanga, Miguel Gamondi.
Baada ya kufanikisha ushindi katika mchezo wa hatua ya 16 bora ya Kombe la Shirikisho (FA) dhidi ya Songea United, Yanga inarejea kwenye kampeni ya kutetea ubingwa wake wa Ligi Kuu Bara.
Timu hiyo inayonolewa na kocha mpya Miloud Hamdi, inashuka dimbani ikiwa na rekodi bora ya kushinda mechi nne na kutoka sare moja kati ya tano zilizopita. Katika mechi hizo tano, Yanga imefunga mabao 16, ikiwa na wastani wa mabao matatu kwa kila mchezo.
Kwa upande wa Tabora United, wanakutana na Yanga wakiwa na kocha mpya, Genesis Mang’ombe kutoka Zimbabwe, ambaye amechukua nafasi ya Anicet Kiazayidi Makiadi. Timu hiyo, ambayo kwa sasa inashika nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi kwa pointi 37, inaingia kwenye mchezo huu baada ya kushindwa kufurukuta dhidi ya Kagera Sugar katika Kombe la FA, ambapo waliondoshwa kwa mikwaju ya penalti.
Kikosi cha Yanga VS Tabora united Leo 02/04/2025
Kikosi rasmi cha Yanga kitakachoshuka dimbani leo kinatarajiwa kutangazwa majira ya saa 09:00 Jioni. Tutakuletea orodha kamili ya wachezaji mara tu kocha Miloud Hamdi atakapokitangaza. Tegemea mchezo wenye ushindani na muto wa kipee, ambapo Yanga itaendelea kuendeleza rekodi yake ya ushindi, huku Tabora United wakipamana kuandika rekodi nyengine ya kuwafunga mabingwa wa ligi kuu.
Mikakati ya Timu Zote Mbili
Kwa Yanga, mchezo huu ni muhimu kwa sababu wanahitaji pointi tatu ili kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi kwa kufikisha pointi 61. Kocha Hamdi anatarajiwa kuendeleza mfumo wake wa kushambulia kwa kasi, jambo ambalo linaweza kuwa changamoto kwa safu ya ulinzi ya Tabora United ambayo imekuwa na udhaifu kwa kuruhusu mabao 28 katika mechi 23.
Kwa upande wa Tabora United, kocha Mang’ombe amesisitiza kuwa wanapaswa kurekebisha safu yao ya ulinzi na kiungo ili kupunguza makosa yanayowagharimu. Katika mechi zao zilizopita, wamekuwa na changamoto ya kulinda mabao yao kwani mara nyingi wamekuwa wakitangulia kufunga lakini wakishindwa kudhibiti uongozi wao.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Viingilio Mechi ya Tabora united Vs Yanga SC Leo 02/04/2025
- Tabora United VS Yanga Leo 02/04/2025 Saa Ngapi?
- Real Madrid Yaweka Dau la Pauni Milioni 90 Kumnasa Bruno Fernandez
- Kagera Sugar Yagonga Mwamba Usajili wa George Mpole
- Ratiba ya Nusu Fainali Kombe la FA 2024/2025 England
- Timu Zilizofuzu Nusu Fainali Kombe la FA Uingereza 2024/2025
Leave a Reply