Kikosi cha Yanga vs Stand United Leo 15/04/2025

Kikosi cha Yanga vs Stand United Leo 15 04 2025

Kikosi cha Yanga vs Stand United Leo 15/04/2025 | Kikosi cha Yanga Leo Dhidi ya Stand United

Kikosi cha Wananchi, Yanga SC, leo Aprili 15, 2025, kitashuka dimbani kwenye Uwanja wa KMC Complex jijini Dar es Salaam katika harakati za kuwania tiketi ya kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho la CRDB (CRDB Federation Cup), maarufu pia kama Kombe la FA. Huu ni mchezo wa kusisimua unaowakutanisha mabingwa watetezi wa taji hilo dhidi ya Stand United, timu yenye historia ya kuumiza vigogo, ikiwemo kumbukumbu ya kuvuruga rekodi ya kutopoteza ya Yanga miaka ya nyuma.

Kwa Yanga, huu ni mchezo wa muhimu mno katika juhudi zao za kutetea ubingwa wa Kombe la CRDB pamoja na kuendelea kuonesha uimara wao katika soka la Tanzania Bara.

Wananchi wanaingia uwanjani wakiwa na motisha kubwa ya ushindi, hasa baada ya kuiona Simba SC – watani wao wa jadi – wakitinga nusu fainali siku chache zilizopita. Yanga, inayodhaminiwa na SportPesa, inalenga kufuata nyayo hizo kwa ushindi dhidi ya Stand United.

Mchezo huu utachezwa saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa KMC Complex – uwanja ambao hivi karibuni uliwaona Yanga wakitoka sare tasa dhidi ya JKT Tanzania, na baadaye kupata ushindi dhidi ya Coastal Union.

Kikosi cha Yanga vs Stand United Leo 15/04/2025

Kikosi cha Yanga vs Stand United Leo 15/04/2025

Kikosi rasmi cha Yanga kitakacho anza leo dhidi ya Stand United kinatarajiwa kutangazwa majira ya saa 9 alasiri. Hapa tutakuletea orodha kamili ya wachezaji wote watakaounda kikosi hicho mara tu kitakapotangazwa na kocha mkuu wa Yanga Miloud Hamdi.

Historia ya Mkutano wa Timu Hizi

Yanga na Stand United wanakutana kwa mara ya kwanza msimu huu wa 2024/2025, kwa kuwa Stand United ilishuka daraja na haishiriki Ligi Kuu. Mchezo wao wa mwisho kukutana katika kiwango cha juu ulikuwa mwaka 2018, ambapo Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 4-3 kwenye Uwanja wa Mkapa – mchezo ulioacha historia ya Alex Kitenge wa Stand United kufunga hat-trick mbele ya Wananchi.

Takwimu, Fomu na Nyota wa Kuangalia Kwa Yanga Sc

Yanga SC wanaendelea kutawala Ligi Kuu Tanzania Bara wakiwa na alama 67 baada ya mechi 25, wakitupia mabao 64, jambo linalowafanya kuwa na safu kali ya ushambuliaji.

Kwa sasa, safu yao ya ulinzi imeruhusu mabao 10 tu, ikiwa ni ukuta wa pili bora baada ya Simba walioruhusu mabao 8. Kwenye mechi 22, Yanga wameibuka na ushindi, sare moja na vichapo viwili dhidi ya Azam FC na Tabora United – lakini wamelipa kisasi kwa ushindi dhidi ya timu hizo kwenye mechi za marudiano.

Mchezaji wa kuangaliwa leo ni Prince Dube, mshambuliaji tegemezi wa Yanga mwenye mabao 12 msimu huu. Dube ndiye aliyefunga dhidi ya Azam FC kwenye Dar Derby na alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mechi hiyo.

Stand United: Azma ya Kufufua Ndoto za Ligi Kuu

Stand United, inayoshiriki Championship, ipo kwenye mbio za kurejea Ligi Kuu. Baada ya mechi 26, wamekusanya alama 55, wakiwa nafasi ya tatu. Safu yao ya ushambuliaji imetupia mabao 42, huku wakiwahi kuibuka na ushindi dhidi ya Songea United (2-1) kwenye mchezo uliopita – matokeo yanayowapa ari kuelekea mchezo huu mkubwa.

Kwa wastani, Stand United hufunga bao moja kila baada ya dakika 55, na hufungwa bao moja kila baada ya dakika 106, jambo linalowafanya kuwa timu ya ushindani mkubwa msimu huu kwenye Championship.

Wachezaji Wanaokosekana Kwa Yanga

Yanga watakosekana huduma ya kiungo mkabaji Khalid Aucho, aliyeumia kwenye mchezo dhidi ya Coastal Union. Aidha, nyota wao mwingine wa safu ya ushambuliaji, Stephane Aziz Ki Pacome, bado ni kitendawili baada ya kupata maumivu katika mechi dhidi ya Azam FC.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Viingilio Mechi ya Yanga SC VS Stand United Leo 15/04/2025
  2. Yanga VS Stand United Leo 15/04/2025 Saa Ngapi?
  3. Jean Jacques Atangazwa Kusimamia Mechi ya Simba SC na Stellenbosch FC
  4. Simba Kucheza na Singida BS Nusu Fainali Kombe la Shirikisho CRDB Federation
  5. Mafanikio ya Msuva Ligi Kuu Iraq Yazidi Kushangaza
  6. Ifahamu Timu ya Stellenbosch Wapinzani Wa Simba Nusu Fainali Kombe la Shirikisho CAF
  7. Simba na Stellenbosch Kukipiga Zenji Nusu Fainali Kombe la Shirikisho CAF
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo