Kikosi cha Yanga vs Songea United Leo 29/03/2025

Yanga vs Songea United Leo 29 03 2025

Kikosi cha Yanga vs Songea United Leo 29/03/2025 | Kikosi cha Yanga Leo Dhidi ya Songea United | Kikosi cha Yanga Kinachoanza leo dhidi ya Songe United Kombe la Shirikisho la CRDB

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya NBC, Yanga SC, leo watakuwa dimbani kuvaana na Songea United katika mchezo wa kuisaka tiketi ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho la CRDB. Mchezo huu wa hatua ya 16 bora utafanyika katika Uwanja wa KMC Complex kuanzia saa 10:00 jioni.

Yanga SC wanaingia kwenye mchezo huu wakiwa na rekodi bora katika michuano ya Kombe la FA, ambapo wamefanikiwa kulitwaa taji hili kwa misimu mitatu mfululizo. Timu hiyo haijapoteza mchezo wowote wa michuano hii tangu mwaka 2021, walipochapwa na Simba SC katika fainali ya FA iliyofanyika kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma. Hadi sasa, Yanga SC wamecheza michezo 20 ya FA bila kufungwa, rekodi ambayo inawafanya kuwa timu tishio katika mashindano haya.

Katika Ligi Kuu ya NBC, Yanga SC wanaendelea kuonyesha ubabe wao kwa kushika nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa ligi. Baada ya kucheza michezo 22, wamepata ushindi mara 19, sare moja na kupoteza michezo miwili pekee. Wamefanikiwa kufunga mabao 58 na kuruhusu mabao 9, wakikusanya jumla ya pointi 58.

Songea United wanakabiliwa na kibarua kigumu mbele ya mabingwa watetezi wa FA. Timu hii inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza (NBC Championship) inashika nafasi ya nane kwenye msimamo wa ligi hiyo, ikiwa na pointi 40 baada ya michezo 24. Wamefanikiwa kushinda michezo 11, sare 7 na kupoteza michezo 6, huku wakifunga mabao 32 na kuruhusu mabao 26.

Japokuwa Songea United hawana rekodi bora kama Yanga SC, mchezo wa leo ni fursa yao kuandika historia mpya kwa kutinga robo fainali ya FA kwa mara ya kwanza. Itakuwa kazi ngumu kwao kutokana na ubora wa Yanga SC, lakini ndani ya soka, lolote linaweza kutokea.

Kikosi cha Yanga vs Songea United Leo 29/03/2025

Kikosi cha Yanga vs Songea United Leo 29/03/2025

Kikosi rasmi cha Yanga kitakachoshuka dimbani leo kinatarajiwa kutangazwa majira ya saa 09:00 Jioni. Tutakuletea orodha kamili ya wachezaji mara tu kocha Miloud Hamdi atakapokitangaza. Tegemea mchezo wenye ushindani na muto wa kipee, ambapo Yanga itaendelea kuendeleza rekodi yake ya ushindi, huku Songea United wakipamana kuandika rekodi ya kuwafunga mabingwa wa ligi kuu.

Kikosi cha Yanga vs Songea United Leo 29/03/2025

Yanga SC na Ndoto ya Kutetea Taji

Kwa upande wa Yanga SC, wanataka kuendeleza rekodi yao ya kutopoteza mchezo wa FA kwa miaka mitatu na pia kutetea ubingwa wao. Kikosi chao kimekuwa imara kwa miaka ya hivi karibuni, kikiongozwa na safu kali ya ushambuliaji inayoweza kufumania nyavu kwa urahisi.

Mchezo huu unatarajiwa kuwa wa kusisimua, huku Songea United wakitafuta njia ya kushangaza mabingwa watetezi. Je, Yanga SC wataendeleza rekodi yao ya ushindi, au Songea United watavunja mwiko kwa kuiondosha timu hiyo kwenye mashindano? Jibu litapatikana jioni hii kwenye Uwanja wa KMC Complex.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Hispania, Morocco na Ureno Wataka Kuandaa Kombe la Dunia la Wanawake 2035
  2. Aishi Manula Bado Mambo Magumu Msimbazi
  3. Kane Atazamia Kufikia Rekodi ya Shilton na Kuweka Historia Mpya Uingereza
  4. Yaliyojiri Mkutano wa Waziri Kabudi na TFF, TPLB, Yanga na Simba
  5. CAF Yaondoa Marufuku Uwanja wa Benjamin Mkapa
  6. Sowah Aweka Bayana Nia Yake Yakubeba Kiatu Cha Dhahabu
  7. Majeraha ya Goti Yamkosesha Alphonso Davies Mechi za Mwisho za Msimu
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo