Kikosi cha Yanga Vs Simba Leo 08/03/2025 | Kikosi cha Yanga Leo Dhidi ya Simba 08 Machi 2025 | Vikosi Yanga Vs Simba Leo Ligi kuu | Kikosi cha Simba Leo Dhidi ya Yanga | Kikosi cha simba vs Yanga 08/03/2025
Kikosi cha mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya NBC, Yanga SC, leo kitashuka dimbani kuwakabili mahasimu wao wa muda mrefu, Simba SC, maarufu kama Wekundu wa Msimbazi. Mchezo huu wa kukata na shoka utapigwa katika dimba la Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, majira ya saa 1:15 usiku. Mashabiki na wapenzi wa soka wanatarajia burudani ya aina yake, huku matokeo ya mechi hii yakitarajiwa kuwa na athari kubwa katika kinyang’anyiro cha ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Dabi hii ya Kariakoo ni ya 114 kwa timu hizi kukutana tangu mwaka 1965. Yanga inaongoza msimamo wa Ligi kwa pointi 58, huku Simba ikiwa na pointi 54. Ushindi kwa Yanga utawaweka hatua moja mbele katika kutetea ubingwa wao kwa msimu wa nne mfululizo.
Kwa upande wa Simba, ushindi utapunguza pengo la pointi na kuwafanya kuwa na matumaini ya kurejea kileleni endapo watashinda mechi zao zijazo, ikiwemo dhidi ya Dodoma Jiji. Kwa aina ya vikosi na ushindani uliopo, Uwanja wa Mkapa utakuwa na mvutano wa hali ya juu, huku dakika 90 za mchezo huu zikitarajiwa kuamua hatima ya nani ataendelea kutawala soka la Tanzania kwa msimu huu.
Kikosi cha Yanga Vs Simba Leo 08/03/2025
Kikosi rasmi cha Yanga kitakachoshuka dimbani leo kinatarajiwa kutangazwa majira ya saa 12:15 Jioni. Tutakuletea orodha kamili ya wachezaji mara tu kocha Miloud Hamdi atakapokitangaza. Tegemea mchezo wenye ushindani na muto wa kipee, ambapo Yanga itaendelea kuimarisha nafasi yake kileleni, huku wekundu wa msimbazi wakipambania kuwashusha mabingwa watetezi katika kilele cha msimamo.
Hali za Kikosi Kabla ya Mechi
Yanga itamkosa kiungo wake nyota, Stephane Aziz Ki, ambaye bado hajawa fiti kikamilifu kutokana na majeraha. Hata hivyo, kurejea kwa beki wa kulia Yao Kouassi kunaipa nguvu safu ya ulinzi, ingawa Israel Mwenda anaonekana kuwa chaguo la kwanza kutokana na kiwango kizuri alichoonyesha tangu atue katika kikosi hicho.
Kwa upande wa Simba, kuna mashaka kuhusu hali ya kipa wao namba moja, Moussa Camara, pamoja na beki Che Fondoh Malone, ambao walipata majeraha kwenye mechi dhidi ya Azam FC. Kocha Fadlu Davids anasubiri ripoti ya mwisho ya kitabibu kabla ya kufanya maamuzi ya mwisho kuhusu kikosi chake cha leo.
Wachezaji wa Kutazamiwa Katika Mchezo wa Leo
Kwa upande wa Yanga SC:
- Clement Mzize na Prince Dube wamefunga mabao 10 kila mmoja msimu huu, hivyo wanatarajiwa kuwa tishio kwa safu ya ulinzi ya Simba.
- Pacome Zouzoua na Maxi Nzengeli wameonyesha uwezo mkubwa wa kutengeneza nafasi za mabao.
- Khalid Aucho, akiwa kiungo mkabaji, atakuwa na jukumu la kuhakikisha anavunja mipango ya mashambulizi ya Simba.
Simba SC:
- Jean Charles Ahoua, mshambuliaji kinara wa Simba, ameifungia timu yake mabao 10 na kutoa asisti sita, na atakuwa tegemeo kubwa kwa Wekundu wa Msimbazi.
- Steven Mukwala na Leonel Ateba nao wanaweza kuwa mwiba kwa safu ya ulinzi ya Yanga kutokana na uwezo wao mkubwa wa kufunga mabao.
- Fabrice Ngoma na Yusuph Kagoma, viungo wa Simba, watapambana vikali na safu ya kiungo ya Yanga kuhakikisha wanatawala eneo la kati.
Matarajio ya Mchezo na Mbinu za Makocha
Kocha wa Yanga, Miloud Hamdi, anatafuta ushindi wake wa kwanza dhidi ya Simba akiwa kocha wa Wananchi. Anatarajiwa kutumia mfumo wa kushambulia kwa kasi huku akitegemea ubora wa viungo wake kama Aucho na Zouzoua kuendesha mashambulizi.
Kwa upande wa Simba, Fadlu Davids analenga kulipa kisasi cha michezo iliyopita kwa kuhakikisha timu yake inacheza kwa nidhamu kubwa, hasa kwenye safu ya ulinzi. Atahitaji kuzuia mashambulizi ya haraka ya Yanga na kutumia udhaifu wowote wa wapinzani wao kupata mabao.
Rekodi za Timu Mbili Katika Ligi Kuu
Katika msimu huu wa Ligi Kuu, Yanga imepata ushindi mara 19, wakati Simba wakishinda michezo 17. Katika michezo 113 iliyopita, Yanga imeshinda mara 41, Simba mara 32, huku mechi 40 zikiishia kwa sare. Aidha, Yanga imepata ushindi katika dabi nne mfululizo, huku ushindi wa mwisho wa Simba ukiwa Agosti 13, 2023 kwa changamoto ya mikwaju ya penalti katika Ngao ya Jamii.
Katika michezo mitano ya mwisho kwenye ligi, Yanga imekusanya pointi 13 kwa kushinda mechi nne na kutoka sare moja, wakati Simba wameshinda michezo mitatu na kutoka sare mbili, wakikusanya pointi 11.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Simba Yatangaza Kususia Mechi Dhidi ya Yanga Leo 08/03/2025: Nini Chanzo?
- Vituo Vya Kununua Tiketi za Mechi ya Yanga vs Simba 08/03/2025
- Bei ya Viingilio Mechi ya Yanga Vs Simba Leo 08/03/2025
- Yanga VS Simba Leo 08/03/2025 Saa Ngapi?
- Tabora United Kuwakabili JKT Tanzania CCM Kirumba Machi 7, 2025
- Bodi ya Ligi TPLB Yatangaza Tarehe Mpya ya Mechi ya Simba na Dodoma
- Timu Zilizofuzu 16 Bora Kombe la Shirikisho la CRDB Federation Cup 2024/2025
- Mechi za Yanga Zilizobaki Ligi Kuu NBC 2024/2025
Leave a Reply